Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Jamani msimnukuu huyu mpuuzi Mwanakijiji. Mamluki na kuwadi wa mafisadi. Niliahamblock kitambo. Si mnaziona pumba zake? Anatuharibia mood.
 
hivi nyie kweli hamjafahamu bado MMKJ? Ni mnafiki wa kupindukia - hujidai yuko upande wa wapenda haki/mabadiliko na mnaweza kwenda naye katika kutetea hoja lakini baadaye inapodhihirika wapenda haki wanashinda, basi hugeuka mara moja na kuwatoseni.

Siwezi kumsahau katika sakata la chama cja CCJ miaka minne iliyopita. Anatumia kile kitu kinachoitwa brinkmanship.
 
Nilikuwa sifahamu kuwa Mwanakijiji ni toilet paper.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Kamanda siku mbili hizi sikuelewi kabisa.....nahisi hauko sawa....remember TIA? uko kinadharia zaidi!!
 
Pole sana mkuu!
Kajipange upya there is always tomorrow..!!! rudisha hela zao jamaa
 
rip mzee.... siku nyingine usidandie hoja namna hii, fanya na id yako ya maficho ulioizoea!!!
 
Heshima yako imeshuka sanaaa!! What a shame...........:sad::sad::sad::sad::sad:
 
There's no point kwa Mahakama kuu kuweka injunction ikiwa nia yao ni kuzuia wala rushwa wasinyongwe ama kutajwa hadharani, huu ni ukiukwaji wa sheria. Let bunge lifanye kazi yake then Mahakama iendelee na hukumu Ya kuwanyonga hawa watu. Ikumbukwe hawa ni majambazi/wahujumu uchumi na kama ni raia wana haki Ya kuhukumiwa then wapewe lawyers wa kuwatetea si vinginevyo.
 
- Kwanza ni nani alipeleka hilo zuio?
- Mihimili mikuu ni
1. Serikali Kuu, Chini ya Rais
2. Mahakama Chini ya Jaji Mkuu
3. Bunge Chini ya Spika
​
Hapo kila mhimili una sheria na miongozo yake, siamini kama kuna kutishiana nyau hapo.

Na mwanaume kati ya hao ni nani?
Mbaya zaidi hapa Bonge ni Serikali =Mahakama na ndiyo mchezo ulitaka kuchezwa na ambao Mzee Mzima anaushabikia!

Kumekuwa na Malalamiko dhidi ya Mamlaka makubwa ya Raisi na ndiyo inayosababisha haya yote.
Jaji Mkuu anayedhibitishwa na Bunge hawezi kuleta upuuzi kamaa ule Bungeni ;yaani wezi wa pesa za Umma wanakwenda mahakamani kuomba Court order na bila hata aibu Mahakaama inaridhia kufanya hivyo.

Kama kweli kulikuwa na dhamira njema,hiyo kesi inatakiwa liendelee hata badaa ya Bunge kufanya maamuzi yake.

Bila kumsahau Pasco wa jf naye .

Mkuu mimi sikuzote huyo Pasco hua simchukuliagi serious kama ambavyo nilivyokua naheshimu mada na mitazamo ya MMK/mtoa mada. Nilikua napokea hoja na mitazamo yake wa umakini mkubwa na bila shaka yoyote. Ila siku mbili hizi kwa kweli naweza kusema he broke my heart bila huruma. Nilikua nasoma hoja zake marambilimbili bila kuamini kama kweli ni yeye au kuna mtu kaiba password yake. Hata sijui nisemeje
 
Huyu mtoa maada nahisi sio mtanzania, na kma ni mtanzania basi nae kapewa fungu kuja kupotosha watu humu ndani! Baba siku hizi Tanzania ya leo sio ile ya mwaka wa 47 hatudanganyiki ng'oo!
 
Back
Top Bottom