Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Mwana kijiji nawe walikuvutia ngapi?? Wewe sio wa kutoa hii hoja. Njaa mbaya
 
Nimeamini wazungu wanaharibu akili za watu sana. nikushauri tu achana na hiyo biashara ya udalali wa Iptl. kwanza wewe ni mtanzania jina tu, ulishauza utanzania wako kwa wazungu. tuache sisi watanzania tunaoumia na ufisadi huo. Eti bunge litii amri ya wezi? nimekudharau sana leo
 
Mwanakijiji wewe umelipwa shilingi ngapi mpaka unakuwa upande wa wezi

Kajipange upya sheria ,kinga na mamlaka ya bunge inasomeka hivi.
Madaraka na Haki za Bunge
Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru
wa mawazo, majadiliano nautaratibu
katika Bunge na uhuru huo
hautavunjwa wala kuhojiwana chombo
chochote katika Jamhuri ya
Muungano, au katikaMahakama au
mahali penginepo nje ya Bunge.(2)
Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti
ya sheria nyingineyoyote inayohusika,
Mbunge yeyote hatashtakiwa au
kufunguliwashauri la madai
mahakamani kutokana na jambo lolote
alilolisemaau kulifanya ndani ya
Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia
ya
maombi, muswada, hoja au
vinginevyo.

Huoni kama mahakama inavunja sheria?
 
Mkuu nahisi MMM nae yumo kwenye huu mgao wa Rugemalira.Huoni siku hizi kawa Dalali wa vitabu Duniani,unadhani mtaji katoa wapi!!.?
 
Mzee Mwanakijiji heshima mbele Mkuu... Nakubaliana na kukinzana na mawazo yako kwa wakati mmoja! Katika nchi inayojali na kutii utawala wa sharia Maamuzi ya Mahakama ni ya mwisho na yanaheshimiwa sana! Kwenye nchi ambayo RUSHWA na UFISADI umetamalaki, Haki inanunuliwa kwa wenye fedha, Judiciary system imefeli ile mbaya usitarajie tukubaliane na nadharia yako isiyokuwa na chembe ya uhalisia Mkuu... Bunge lifanye shughuli yake ya kutuwakilisha vema, wananchi wote Watanzania wanataka kujua sintofahamu hii ya ESCROW a/c!!! Watanzania wamechoka kuua Panya RD huku MAJAMBAZI yakitanua kwa fedha zetu!!! Kwani Mwanakijiji Umechukua kiasi Gani?
 
mahakama ndo chombo cha juu kabisa cha kutoa haki.
Bado hauja elewa ninini kinaendelea, hivi na wewe ni wale wale akina chenge? Mbona wakati wa katiba mahakama ilisema haiwezi kuingilia bunge ingawaje Kubenea alikuwa sahihi? Au ni pale tu wanaposhikwa pabaya ndiyo wawe ndumilakuwili? Hii mahakama ni ya ajabu utafikiri ni ya majuha! Pole sana, bunge na lisonge mbele.
 
Watu wanataka kutumia judicial independence kuifanya mahakama kichaka cha kufichia uovu.Hii haitakubalika hata kidogo.

Ni kweli mahakama inahitaji uhuru na upekee ili ifanye kazi zake vizuri,lakini tujiulize,mahakama zetu zina uhuru kweli?
Kwa kuzingatia utegemezi iliyonao kwa serikali kuu,ambapo watendaji wakuu wengi wa mahakama ni wateule wa rais,na budget ya mahakama inategemea maamuzi na utekelezaji wa mihimili mingine ya dola,mahakama yetu haiko huru,hivyo ni rahisi kuwa influenced kimaslahi na maamuzi ya watendaji wa mihimili mingine.

Pili,ile doctrine of separation of powers inataka mihimili yote ya serikali iwe na hadhi sawa kimaamuzi.Inaepusha mamlaka yote ya state kuwa vested sehemu moja,instead,unakuwa na vyombo vitatu(kwa mfumo wetu),bunge,mahakama na serikali kuu.

Mihimili hii mitatu inaendesha nchi na kuwa na mahusiano katika namna inayohakikisha kuwa sheria na maslahi ya state vinafuatwa bila kuwepo abuse of power ya upande wowote ule,iwe mahakama,executive au bunge,kunatakiwa kuwepo "checks & balances".

Kutokana na unyeti wa mahakama,inasemwa kwamba inabidi iwe na "uhuru kamili" ili haki itendeke vizuri.
Hata hivyo,uhuru huo huo unaweza kutumika kuifanya mahakama kuwa superior zaidi ya mihimili mingine ya dola,na hivyo kuondoa kabisa separation of powers.

Hii ni hatari iliyopo hapa nchini.

Mahakama inataka kufanywa kuwa superior kuliko bunge,huku watendaji wa mahakama wakiwa wateule wa executive,na issue iliyo mezani ikiwa inahusu misconducts ndani ya executive,baadhi ya watendaji walioguswa wakiwa ni wale wale wanaoteua watendaji wakuu wa mahakama,kukiwa na madai ya rushwa yanayohusisha hadi majaji wa mahakama,na kashfa yenyewe kwa kiasi kikubwa ikitokana na a very controversial court rulling.

Kwa muktadha huu,naona bunge lina haki ya kuendelea na kumalizia ushughulikiaji wa suala la escrow,kazi ambayo liliianza mapema hata kabla ya hao PAP kufungua kesi,na kutaka kuitumia mahakama kuingilia kati jambo ambalo lilishaanzishwa bungeni.Huu utakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa the doctrine of separation of powers,na pia executive ikitumia influence yake ndani ya mahakama kwa makusudi itakuwa inatumia mahakama kulizima bunge pale linaposimama kidete kuisimamia serikali,na hii ni abuse of power na italeta shida sana katika utendaji wa pamoja wa kiserikali kwa maendeleo ya taifa.

My take;

-bunge liendelee kuwashughulikia hawa wezi,

-Ni vema suala la constitutional economics likapewa kipaumbele katika mchakato huu wa katiba ili kutafuta uwezekano wa kuipa mahakama uhuru kiuchumi pia,

-Watanzania tudai rasimu ya Warioba.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Off point, washout, out of context! Siyo kila kitu unaweza kukitungia hadithi. Yaonekana jambo hili kwako ni elephant.

PAP inahusika vipi na uchunguzi wa Escrow? Bunge liliomba uchunguzi wa matumizi ya pesa iliyokuwa chini ya escrow, wala halikuchunguza PAP. i hope nawe hujalambishwa eti ujaribu kutubadili watu wa JF. Hakuna uhusiano wowote wa kusema Bunge na mahakama vinaingiliana, wapi? Kama ni hivyo mahakama ndo imeingilia uhuru wa bunge, kwani hawakujua kwamba kuna uchunguzi uliitishwa na bunge?

Another nonsense!
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.
Upo sahihi sana mkuu. Mahakama, ukizingatia principle of separation of powers, ndicho chombo kikuu cha kutoa haki. Ila mahakama zetu hapa Tanzania haziaminiki na tumeshuhudia mara nyingi zikitumika vibaya. Rushwa imekidhiri mno!
Besides, ninachokijua mimi ni kuwa Tanzania haifuati strictly trias politica, na ndio maana serikali inaundwa kutokana na wabunge. Tusijitie leo eti mahakama na bunge siziingiliane. Nchi zingine kama UK bunge ndio mwamuzi wa mwisho hata juu ya mahakama zote!
 
Kitu kimoja lazima kielewek vizuri. Katika Escrow mahakama imeguswa (Conflict of interest). Kama kuna majaji wamepata mgao wa Escrow kwa nini tuamini kuwa mahakama haina lengo la kuwalinda majaji hao. Bunge nalo linauhuru wake kadiri ya katiba na sheria zake. Halizuiwi kujadili ufisadi ulioigusa mahakama.

Pwenti!
 
Upo sahihi sana mkuu. Mahakama, ukizingatia principle of separation of powers, ndicho chombo kikuu cha kutoa haki. Ila mahakama zetu hapa Tanzania haziaminiki na tumeshuhudia mara nyingi zikitumika vibaya. Rushwa imekidhiri mno!
Besides, ninachokijua mimi ni kuwa Tanzania haifuati strictly trias politica, na ndio maana serikali inaundwa kutokana na wabunge. Tusijitie leo eti mahakama na bunge siziingiliane. Nchi zingine kama UK bunge ndio mwamuzi wa mwisho hata juu ya mahakama zote!

Vipi,do you see any trias politica kwenye rasimu ya Warioba?
 
Show show thé parliament checks thé judiciary organ with thé référence to checks and balance in Tanzania.Il swali nilipewa kama assignment ya CW mzee mwanakijiji karibu.
 
Mzee Mwanakijiji umepotea kwa muda mrefu then umekuja na pumba nzito nzito...ofcourse it is a sound rubbish,
Hii nchi ni lini imeanza kuendeshwa kwa sheria?, any way lakini hata mahakama haipo juu ya sheria, so ifanye kazi zake bila kuingilia mihimili mingine, bunge halitoi hukumu bali linajadili ile riport....
By the way I was thinking out of tank nkadhani bunge ni wananchi, sisi, tuna nguvu kuliko mahakama, ...

So we upo kwenye payroll ya Rugemalila au SingaSinga? nataka nkaangalie fungu lako, maana you came in unexpected way, while we got some saga before and you were so cold...
 
Last edited by a moderator:
Nilisoma makala moja kwenye gazeti la daily news(Gazeti la serikali) baadaye kuna mkuu aliweka makala hiyo hapa jamvini. Makala hiyo iliandaliwa na VIP Engineering ya Ruge. Katika andishi lile VIP wanasistiza kuwa ela iliyokuwa Escrow account, ilikuwa halali kuchukuliwa na wamiliki wa IPTL yaani PAP. Na wakasema Standard C Bank waache kuwasumbua wateja wao yaani PAP(waliowauzia hisa 30% za IPTL)...maana deni walilokuwa wana dai (hao Standard C Bank) tayari walishalipwa kabla ya 2006.

Sasa leo ninajiuliza tena kwa 'kudadisi'...kama maelezo ya VIP yako sahihi inakuwaje tena PAP wawe na wasiwasi tena kiasi cha kushika kiguu na njia kwenda mahakamani kupinga suala pesa zao 'halali' lisijadiliwe bungeni ?

Mnh! Kweli hapa pana namna...!? Hii namna lazima izamishe ....yeyote aliyehusika kuchukua kisicho halali.
 
Mzee Mwanakijiji heshima mbele Mkuu... Nakubaliana na kukinzana na mawazo yako kwa wakati mmoja! Katika nchi inayojali na kutii utawala wa sharia Maamuzi ya Mahakama ni ya mwisho na yanaheshimiwa sana! Kwenye nchi ambayo RUSHWA na UFISADI umetamalaki, Haki inanunuliwa kwa wenye fedha, Judiciary system imefeli ile mbaya usitarajie tukubaliane na nadharia yako isiyokuwa na chembe ya uhalisia Mkuu... Bunge lifanye shughuli yake ya kutuwakilisha vema, wananchi wote Watanzania wanataka kujua sintofahamu hii ya ESCROW a/c!!! Watanzania wamechoka kuua Panya RD huku MAJAMBAZI yakitanua kwa fedha zetu!!! Kwani Mwanakijiji Umechukua kiasi Gani?

Mwanajiji umejikita tu kwenye séparation of power lkn umejifanya kipofu kwenye mambo haya checks and balance of power. Parliament should ne thé mouthpiece of thé people with all guts bro.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.
Tanzania taasisi pekee zilizobaki na kuheshimika ni bunge na JWTZ tuu,nani asiyejua kuwa mahakama ni kichaka cha rushwa?
 
Mzee mwenzangu hapa kidogo umefuka. Bunge alifanyi judgement, linafanya majadiliano kuhusu report. Ni sawa tumwambie rahisi huwezi fanya kitu fulani sababu kipo mahakamani. Bunge, Rahisi na Mahakama ni mihili mitatu tofauti isiyoingiliana kazi. Mahakama iendelee na kazi yake na bunge liendelee na kazi yake. Kusema mahakama ipo juu zaidi ya bunge sio sawa.

Yani bongo poa sana kitu ambacho hakiwezekani bongo watu wanakifanya kinawezekana na wanakijengea hoja na kinakubarika, ajabu hili la nane la dunia(Tz) mbona haliwekwi
 
Kwanini mahakama hio hio iliachia bunge uchwara lakatiba liendelee wakati baadhi ya wabunge wakiiomba isitishe mjadala hadi liwasikilize? Takataka hii ni kwenye nchi ya matakataka pekee! Bora wavunje bunge nchi iendeshwe ki-freestyle tu.

mkuu umebakiza wakivunja bunge wakaacha mahakama ibakuwaje na mahakama ifumuliwe isukwe upya na tume ya utumishi wa mahakama
 
MM,
Nakubaliana na hoja zaako. zina mantiki sana. Ila katika hili sakata...

  • Bunge linatakiwa kupima maslahi ya Taifa na hali ya hewa ya kisiasa kwa sasa ilivyo nchini. Nadhani itakuwa hekima ikajadiliwa ili kuleta amani mioyoni mwa watanzania
  • Hatari ya kutii amri ya mahakama katika hili ni kuwa watanzania watalishwa hata yale yasiyo ya kweli katika sakata hili na hata ikija kujadiliwa baadaye...itaonekana imekuwa diluted au kuchakachuliwa. Inaweza ikawaponza hata wale waliokuwa hawahusiki na sakata hili.
  • Kila kukicha majina yanaongezeka na hatujui ni kweli au la...Bora hekima itumike katika kuruhusu Bunge lijadili sakata lote ili ukweli halisi ujulikane

Absolutly true
 
Mzee mwenzangu hapa kidogo umefuka. Bunge alifanyi judgement, linafanya majadiliano kuhusu report. Ni sawa tumwambie rahisi huwezi fanya kitu fulani sababu kipo mahakamani. Bunge, Rahisi na Mahakama ni mihili mitatu tofauti isiyoingiliana kazi. Mahakama iendelee na kazi yake na bunge liendelee na kazi yake. Kusema mahakama ipo juu zaidi ya bunge sio sawa.

Nakubaliana nawewe Mkuu.

Ya kwamba inachofanya fanya bunge ni kujadili na kutoa mapendekezo nn kifanyike na ndiyo hasa kazi ya bunge.

Kitu kingine kilichopo tukiwapa wahalifu loophole kama hii basi utakuwa ndiyo mchezo wao yaani wa kufanya frauds kisha kukimbilia mahakamani kuweka vizuizi.

Safaru hii hawana pa kutokea.

Tunao hawa wezi wetu.

Arobaini zao zishafika.
 
Back
Top Bottom