Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Makubwa !!! Ina maana hao wabunge wamemsahau aliyewatuma huko ? Si wameenda kwa kutumwa na sisi wananchi kwa hiyo tunapaswa kuona kama kile tulichowatuma ndicho wanachosema. Basi, kama hiyo hoja ya kutaka sisi tuliowatuma tuwaone live wakituwakilisha, nasi wananchi tupitishe hoja ya kutowaona live wakati wakituomba kura kwa kupiga magoti kama watoto wadogo.
 
Imeharibika siku ya kuanza Bunge?
Kwani Bunge hili ni la zimamoto halikuwa na maandalizi?
Huenda kulikuwa na utambulisho wa hoja tete, ndiyo maana wakacollude na TBC kuwa kitu isiende hewani!

Hivi kumbe wabunge wametimiza azima yao ya kutotuonyesha ni nini wanafanya huko Bungeni? Hawakuonyesha kumbe live. Kama hawataki kuonyesha Bunge nasi tususie kununua magazeti yanayoandika habari za Bunge ili magazeti nayo wasiandike kwa kuwa watakaoandika watakosa wateja. Tuamue kutopata habari za bunge kwa njia yoyote ili wabaki peke yao
 
Kitu nilichokuwa nikijiuliza mara kwa mara eti Tbc mtambo wao wa kurushia matangazo yao wa dodoma umepata itilafu sasa na Itv, na startv je??'? Na wao sare sare!!!!
 
tanzania hiyo. hivi huko bungeni wanamsemea nani. kama siyo sisi ijulikane.
 
Hakika kabisa, hao uliotaja wanahusika moja kwa moja, na amini usiamini lazima ni wa CCM wote!
Hakika hoja hiyo ikifanyiwa kazi wananchi tunapaswa kuonyesha live kuwa hatukubali upopompo huo!...
wale miungu watu wana akili fupi sana.., kama wamedhamiria najua lazima watafanya hivyo, lakini siku zao zinahesabika tu pale
 
Yaani mkuu Arushaone hujamuelewa zumbemkuu au unatania?
amenielewa sema kazuga tu, nawaambia tena huyu Lema hafai kabisa, amevuruga wanachama wote wa CCM vijijini, leo tena karudi Bungeni wanazima mitambo, kwanini huyu Lema? waziri mkuu anamtambua sana, huyu lema anavuruga nchi kabisa....
 
kuongozwa na na spika mwenye maono kama haya ni janga kwa taifa yaani hapa anawadharilisha wanawake sana na kuonyesha hawawezi kuongoza au kupewa nyadhifa nyeti
 
Poor Tanzanian MP's mara hii mumesahau dhamana mliyopewa na wananchi kwamba mkawe wawakilishi wao huko Bungeni badala yake mnataka muabudiwe,vipindi vya bunge hamtaki wawakilishi wenu waangalie,mnataka muendelee kulala tu bila kuonekana kwa wapiga kura wenu,kumbukeni 2015 sio mbali kumbukeni mtarudi tena kuomba ridhaa ya kukaa humo ili mfanye uchafu wenu ambao hamtaki uonekane,Ni nini mnachokificha ambacho hamtaki kionekane? Mbona mnakuwa wachawi nyie? Mmeshasahau kwamba hayo madaraka mliyonayo ni dhamana sasa hivi mnayo lakini wengi2015 hamrudi kwa hiyo msijidanganye na hayo mnayotaka kuyaficha
 
Kwa anayefahamu......Tunaomba majina ya wabunge waliowasilisha hoja........
 
Back
Top Bottom