Bunge lamchunguza, Rais ampa zawadi

Bunge lamchunguza, Rais ampa zawadi

Sioni tatizo lolote kama wote tunafikiri kwa kutumia hayo hayo mananihi (a.k.a Masaburi) aliyoyasema huyo Meya
 
Inawezekana kabisa Mayor Masaburi akawa hana hatia,ni mtu safi, lakini kwa kipindi hiki ambacho yuko kwenye uchunguzi si busara hata kidogo kuonekana kwenye hiyo picha na Rais. Psychologically inampa Mayor Masaburi nguvu kubwa sana.

Kitu kingine ambacho kinanipa shida ni nani analipia hizi futari za kila juma? Nauliza hili kwa nia njema kabisa, na natambua hiki ni kipindi muhimu kwa waislam na nilitegemea Rais angefutarisha watu lakini (LAKINI) sikutegemea angefutarisha kwa kasi hii. Nchi masikini ambavyo inakopa kila kukicha kwa nini Rais anashindwa kutambua concept ya 'kubana matumizi'?.

Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi nusura ikwame kwa sababu ya kukosa fedha, Raisi yeye anazo mpaka za kununua zawadi kwa Watuhumiwa wa rushwa? Umpe mtu chakula na zawadi pia? Washauri wa Rais wanafanya nini? Kwanza mmeona hiyo mifuko ya zawadi? ni kiasi gani mfuko mmoja? Hawa waliofutarishwa wana njaa gani mpaka wapewe chakulana Rais?.

Kama ni lazima kufutarisha kila juma basi wafutarishwe watoto yatima na wasukuma mikokoteni. Hawa ndio wanataka chakula lakini sio wakina Mayor Masaburi.

Sijui tumefikaje hapa. Sijui!
Nisingeweza kuyasema hayo vizuri zaidi.
 
Kama ukiwa na kashfa huna hatia mpaka itakapodhihirika, mbona Katibu Mkuu Jairo kaambiwa asikanyage wizarani?

Issue ya Jairo ina ushahidi wa moja kwa moja kwa kuwa alisaini barua ya kuchangisha zile ngawila, hata sijui wanachunguza nini zaidi ya kucuhukua ile barua na kuipelekeka mahakamani ili aeleze zilikuwa kwa ajili ya nini? Ni tofauiti na huyu mayor ambaye issue inahusu watu wengi.
 
Issue ya Jairo ina ushahidi wa moja kwa moja kwa kuwa ...
lakini bado hana hatia, sivyo? Kwa hiyo inawezekana kuanza kunyimwa haki/mambo fulani hata wakati tunasubiri kuthibitisha hatia.

Kuna vyombo vya haki vya aina mbili, vile rasmi, kama mahakama, kamati za uchunguzi za bunge, TAKUKURU n.k. Halafu kuna mahakama ya wananchi. Hii inakuhukumu hapo hapo, katika jamii Masabiri sasa hivi ameshachafuka. Kikwete ajifunze kuji-distance na viongozi waliochafuka kwenye kijamii.

Rais Kikwete hawezi kubisha kabisa kwamba wakina Rostam Aziz, Lowassa, Hayati Ditopile Mzuzuri, Karamagi, Msabaha, na maswahiba wake wengi wengine ndio wametia doa utawala wake, na ndivyo historia itakavyorekodi. Yabidi ajifunze katika ngwe yake iliyobaki.
 
Nilikuwepo kwenye hafla hii, ni siku aliyofuturisha, wanaume walipewa mifuko hii ikiwa na vikoi na supande wa wanawake mama salma aligawa zawadi ya aina hii ndani kukiwa na vitenge. Ni zawadi ya futuru.. Ila kwangu mimi sioni kama ni sadaka kwani anawaridhisha matajiri amabo hata hata hivyo vitu hawatavitumia, wanaweka makabatini tu.. Ni bora angeamua kufuturisha wale wasiojiweza , wenye shida hata ya kg 1 ya unga kwa siku
Duh, kumbe na wewe tajiri?
 
kwani hamjui Simon group ni geresha na mnunuzi wa kweli ni RIZIWANI????????????????????????
 
Tanzania ni kama ndege ambayo iko kwenye auto-pilot.Tukitumia akili zetu kufikiri 2015 tunaweza kupata Rais wa kuiongoza nchi
 
Kwani kuchunguzwa ndio kuwa na kosa?
 
Ndio Kazi Pekee Mweshimiwa anaweza kuoganise na kufanikisha!!
 
Nilikuwepo kwenye hafla hii, ni siku aliyofuturisha, wanaume walipewa mifuko hii ikiwa na vikoi na supande wa wanawake mama salma aligawa zawadi ya aina hii ndani kukiwa na vitenge. Ni zawadi ya futuru.. Ila kwangu mimi sioni kama ni sadaka kwani anawaridhisha matajiri amabo hata hata hivyo vitu hawatavitumia, wanaweka makabatini tu.. Ni bora angeamua kufuturisha wale wasiojiweza , wenye shida hata ya kg 1 ya unga kwa siku

Sijajua sana taratibu za mfungo wa ramadhani na makando kando yake yanatakiwaje.

Mfungo wa Kwaresima wakristo wanatakiwa kupunguza au kutoa kabisa matumizi yasiyo ya lazima na kufunga chakula, na unapofunga chakula kile chakula ambacho ulitakiwa ule wakati umefunga pamoja na mengine ambayo umeyaacha unatakiwa uyatolee sadaka kwa maskini ambao hawana uwezo kama chakula, malazi, nguo nk.

Kikwete anafuturisha wale ambao hanawa dhiki, na uwanja mzima ulijaa magari ya kifahari nini amefanya? Sidhani kama kurani inadai wakati huu kufuturisha matajiri wenye uwezo badala ya maskini.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Unatarajia nini kutoka kwa kiongozi mahiri mzururaji? Wa Tatanzania hiyo ni miaka yenu ya kuumia. mpaka mshike adabu kwa wrong choice ya uprezida

​Rais kikwete priority ni uzururaji na tafrija
 
(Hawa waliofutarishwa wana njaa gani mpaka wapewe chakula na Rais?. Kama ni lazima kufutarisha kila juma basi wafutarishwe watoto yatima na wasukuma mikokoteni. Hawan ndio wanataka chakula lakini sio wakina Mayor Masaburi.)

kweli kabisa,hata mbele za Mungu funga yako itapokelewa.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa kuwa bado anachunguzwa hana hatia, mpaka pale itakapodhihirika kuwa ametenda kosa, kwa maana hiyo yuko huru kukutana na kila mtu hadi pale kosa lake litakapobainika.

Ndugu Kikwete ni Rais, sio Mahakama. Kuna Sheria na Maadili. Ili kujenga maadili na kusisitiza (kwa nafasi yake kama rais) vita dhidi ya ufisadi, rais alitakiwa akae mbali na huyu bwana.
 
(Hawa waliofutarishwa wana njaa gani mpaka wapewe chakula na Rais?. Kama ni lazima kufutarisha kila juma basi wafutarishwe watoto yatima na wasukuma mikokoteni. Hawan ndio wanataka chakula lakini sio wakina Mayor Masaburi.)

kweli kabisa,hata mbele za Mungu funga yako itapokelewa.

Kweli kabisa mkuu mwezi mtukufu Mnyazi Mungu anasema toa moja ya mali zako kuwasaidia wasiojiweza,Lakini yeye anasaidia wenye utitiri wa mali ndio UISLAM HUO?
 
Nilikuwepo kwenye hafla hii, ni siku aliyofuturisha, wanaume walipewa mifuko hii ikiwa na vikoi na supande wa wanawake mama salma aligawa zawadi ya aina hii ndani kukiwa na vitenge. Ni zawadi ya futuru.. Ila kwangu mimi sioni kama ni sadaka kwani anawaridhisha matajiri amabo hata hata hivyo vitu hawatavitumia, wanaweka makabatini tu.. Ni bora angeamua kufuturisha wale wasiojiweza , wenye shida hata ya kg 1 ya unga kwa siku

Sasa wewe ulifuata nini kwenye hiyo futali?? Au hako kazawadi hukukapata??
 
Back
Top Bottom