Bunge lamchunguza, Rais ampa zawadi

Inawezekana kabisa Mayor Masaburi akawa hana hatia,ni mtu safi, lakini kwa kipindi hiki ambacho yuko kwenye uchunguzi si busara hata kidogo kuonekana kwenye hiyo picha na Rais. Psychologically inampa Mayor Masaburi nguvu kubwa sana.

Kitu kingine ambacho kinanipa shida ni nani analipia hizi futari za kila juma? Nauliza hili kwa nia njema kabisa, na natambua hiki ni kipindi muhimu kwa waislam na nilitegemea Rais angefutarisha watu lakini (LAKINI) sikutegemea angefutarisha kwa kasi hii. Nchi masikini ambavyo inakopa kila kukicha kwa nini Rais anashindwa kutambua concept ya 'kubana matumizi'?.

Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi nusura ikwame kwa sababu ya kukosa fedha, Raisi yeye anazo mpaka za kununua zawadi kwa Watuhumiwa wa rushwa? Umpe mtu chakula na zawadi pia? Washauri wa Rais wanafanya nini? Kwanza mmeona hiyo mifuko ya zawadi? ni kiasi gani mfuko mmoja? Hawa waliofutarishwa wana njaa gani mpaka wapewe chakulana Rais?.

Kama ni lazima kufutarisha kila juma basi wafutarishwe watoto yatima na wasukuma mikokoteni. Hawa ndio wanataka chakula lakini sio wakina Mayor Masaburi.

Sijui tumefikaje hapa. Sijui!
mkuu maneno yako sawia lakini unampigia mbuzi gitaa na hii ni kutokana na ujinga wetu watanganyika 1. sisi ni wanafiki 2. hatuna uzalendo 3. wengi wetu ni wachumia tumbo 4. sisi ni wajinga wakutupwa 5. watanganyika wote tunatumia masaburi kufikiri 6..... nakomea hapo maana naweza kutukana bure watu wasiojua kuwa wanatukanwa na wakati huo najitukana mwenyewe
 
wiki ijayo atafuturisha mapacha watatu. Nahisi hii futuru huambatana na kujadili dili zao!! Sijui dini inasemaje kuhusu kufuturisha wengine kwa hisani!!
 
Mkuu haitakii mema nchi hii. Kosa ni la wapiga kura hatuko makini maana uchguzi wa kwanza ulitoa msimamo wa huyu mkuu kuwa hawezi kufanya baadhi ya mambo kwa ujasiri. Serikali inaogopa mafisadi, inaogopa wauza unga, sasa kilichobaki ikulu imekuwa mgahawa, kesho utasikia wapiga box nao wanafuturishwa.
 
Hapa JK alikuwa hana jinsi. Alialika viongozi wazito wa jiji hili. Meya asingekosekana. Kwenye Umeya wa JIji hili JK alimtaka Saggaf. Masaburi akatoa dau kubwa zaidi kwenye uchaguzi wa Meya. Diwani mmoja aliniambia kila mmoja alipewa 1.8m. Saggaf alikuwa ametoa 1m. Ndio maana hata hapo kwenye picha JK anaangalia pembeni kabisa.
 
Kwa kuwa bado anachunguzwa hana hatia, mpaka pale itakapodhihirika kuwa ametenda kosa, kwa maana hiyo yuko huru kukutana na kila mtu hadi pale kosa lake litakapobainika.
Attitude yako ndio inayolea ufisadi hapa nchini. The fact kuwa mtu anachungzwa anatakiwa kusimamishwa kazi hadi hapo matokeo ya uchunguzi yatoke. Sasa ikithibitika kuwa ni kweli alifanya ufisadi ina maana rais wetu ni sehemu ya ufisadi huo. Kumbuka usemi maarufu "Ukitembea na mwizi na wewe ni mwizi
 
Hapa JK alikuwa hana jinsi. Alialika viongozi wazito wa jiji hili. Meya asingekosekana. Kwenye Umeya wa JIji hili JK alimtaka Saggaf. Masaburi akatoa dau kubwa zaidi kwenye uchaguzi wa Meya. Diwani mmoja aliniambia kila mmoja alipewa 1.8m. Saggaf alikuwa ametoa 1m. Ndio maana hata hapo kwenye picha JK anaangalia pembeni kabisa.
kitendo cha JK kmutaka mtoa rushwa kama amabvyo umeanisha nalo ni tatizo. Kutazama pembeni haisaidii, jiulize kama rasii angekuwa ni Nyerere huyo mhuni angekanyaga hata Ikulu?
 
Mods, kwanini wamepitisha hii Thread? Haimaanishi Chochote...

Rais kama kiongozi kawaalika Madiwani na Wabunge na Viongozi wote wa Mkoa kula futari na kugawa zawadi ...

Even if Masaburi ni mwizi bado hukumu kwahiyo ni bado Diwani na Meya... na sio yeye pekee aliyepata hizo zawadi kila mtu aliyealikwa alipewa na hii ni Common kwa Waislamu wakati wa Mfungo wa Ramadhani kuwa Wakarimu na kutoa Zawadi.

SO EVEN IF WE DON'T Like Masaburi and The President... Hii topic does not hold water...

The plain truth is that there is nothing to discuss about this Picture... We need more Critical Threads!!!
 
Nachokifahamu mimi ni kwamba Futari wanakula wale walio kwenye mfungo, sasa huyu masaburi alifunga siku hiyo?
hata kama alifunga, Mfungo tunaouzungumzia ni special kwa waislamu, huyu Masaburi ni Muislamu?

Hivyo Basi, ni makafiri wangapi walikaribishwa kwenye takio hili hadhimu kabisa kwa waislamu?
mwenye list kamili ya makafiri waliohudhuria atapatie hapa jamani.

Kama makafiri walihudhuria, ni ushahidi gani ndugu zetu waislamu wanasubiri ili kujihakikishia
kwamba porojo za kidini zilizobarikiwa ikulu hazina masilahi ya aina yoyote ile kwao?

Hapa Jakaya amethibitisha kwa dhati kabisa kwamba yeye si muislamu wa kweli.
kama hata kwa kitendo hiki ndugu zetu waislamu fulani wataendelea kumkumbatia huyu
jamaa basi watufariji watanzania wote kwa ujumla kwa kuyaunga mkono mapambano
dhidi ya ufisadi na chama dhalimu cha mapinduzi kutoka katika utawala wa nchi yetu.

Waislamu hawa fulani japo kuanzia hapa basi watambue kwamba kwa kwa kadiri
watanzania wengine tunavyotambua kwamba Chama cha Mapanduzi kama taasisi,
na wanachama wake mmoja mmoja kama Ben Mkapa, Edward Lowasa, Philip Mangula,
Rostamu Azizi, David Jairo nk ndio moja ya chanzo cha watanzania kuishi katika lindi la
umasikini katikati ya utajiri mkubwa na hivyo kuanzisha harakati mbali mbali katika kuhakisha
kwamba wanaondoka madarakani na kuchukuliwa hatua stahiki ndio hivyo hivyo tunavyomtambua
na kunuia kwa rafiki, kipenzi cha roho zao Jakaya Mrisho Kikwete.
 
tunashauriwa tuwakarimu mafukara na si wenye uwezo.kwa mujibu wa maandiko
matakatifu
 
Unachoshangaa nini sasa?
Tuhuma za masaburi haziwezi kua kubwa kuliko za Mramba, EL, RA, ACh,
Labda umesahau jinsi mtu huyuhuyu alivyowapigia debe kwenye uchaguzi watajwa hapo juu ikiwa walikua na tuhuma/kesi kubwa tu za ufisadi!!
 
IK+(22).jpg


Msahiki Meya wa Dar-es-Salaa, Didas Masaburi.
Kwani si huyo huyo JK alimshika mkono Lowasa kule Monduli alidai kuwa ni SAAAAFIII ...........!!! ............. Nini kilifuata...??? Ghafra Lowasa akawa GAMBA.......... HIVYO HUYO ALIYESEMA WATU WANAFIKIRI KWA KTUMIA MASABURI NAYE ASUBIRI............. Yeye hatakuwa gamba........bari shina la la MAGAMBA
 
MASA BURI bado ni Meya na anawakilisha jamii. HAFLA hiyo ilikuwa jijini dar so kama meya lazima aalikwe ikulu that is protocal; angekuwa amepewa barua ya likizo ili kupisha uchunguzi kisha mr president akampa mwaliko hiyo ni kesi ingine. msimamisheni kwanza!!!!

"DONT MAKE OTHER PEOPLE LAUGH AT YOUR BACK"
Wewe unasema nini? huyo mkuu haishi vituko, Rombo alimsimamisha Mramba na kumwita shoka lisilokwisha makali ilihali ana kesi mahakamani ya matumizi mabaya ya ofisi. Ahh! bora ninyamaze tuu maana tukisema sana tutachafua thread bure!
 
Ee Mungu utusaidie watanzania tufikie mwaka 2015 kwa amani bila machafuko. Kwa JK kilichobaki ni sala tu, ushauri haumsaidii au hana washauri.
 
Back
Top Bottom