Bunge lamchunguza, Rais ampa zawadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge lamchunguza, Rais ampa zawadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bu'yaka, Aug 15, 2011.

 1. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 695
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 80
  [​IMG]

  Msahiki Meya wa Dar-es-Salaa, Didas Masaburi.
   
 2. BABU CHONDO

  BABU CHONDO JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 860
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nini hicho
   
 3. M

  MWananyati Senior Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inategemea ni zawadi ya nini. Fafanua, Ila nakushauri 'Acha vipofu waongozane', mwisho wake tutauona.
   
 4. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  duh hii kali zaidi
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yaani ina maana kwamba Bunge liache kumchunguza huyo swahiba wake katika madili waliyofanya au wanataka kufanya jijini Dar.
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,670
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Bila kujali ni zawadi gani anayopewa huyu hakupaswa hata kukanyaga ikulu. Mbali ya tuhuma za ufisadi,juzi pia katutukana watanzania wote kupitia kwa wawakilisha wetu leo tunamwona kwenye ofisi yetu ya juu kabisa nchini akipeana mkono na mkuu wa nchi, is he being rewarded kwa kutuibia na kutuinsult?. Huu upuuzi I'm sure huwezi kuuona mahali pengine popote duniani zaidi ya Tanzania.
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Barua za kufukuzwa kutoka kwenye chama...Lowassa nae alipewa
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,378
  Likes Received: 791
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa bado anachunguzwa hana hatia, mpaka pale itakapodhihirika kuwa ametenda kosa, kwa maana hiyo yuko huru kukutana na kila mtu hadi pale kosa lake litakapobainika.
   
 9. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilikuwepo kwenye hafla hii, ni siku aliyofuturisha, wanaume walipewa mifuko hii ikiwa na vikoi na supande wa wanawake mama salma aligawa zawadi ya aina hii ndani kukiwa na vitenge. Ni zawadi ya futuru.. Ila kwangu mimi sioni kama ni sadaka kwani anawaridhisha matajiri amabo hata hata hivyo vitu hawatavitumia, wanaweka makabatini tu.. Ni bora angeamua kufuturisha wale wasiojiweza , wenye shida hata ya kg 1 ya unga kwa siku
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,040
  Trophy Points: 280
  senkyu ticha
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,040
  Trophy Points: 280
  acha mchezo na rafiki mnafiki
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,422
  Likes Received: 677
  Trophy Points: 280
  Hapa naona Masaburi yanatumika kufikiri.
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 4,841
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hamkuelewa kile alichomaanisha Hosea wa takukuru mbele ya balozi wa Marekani bado?
  .
   
 14. C

  CBN Member

  #14
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa wa kumlaumu nan masaburi au aliyempa zawadi masaburi kwa kufikiria kupitia masaburi?
   
 15. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 1,954
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Unatarajia nini kutoka kwa kiongozi mahiri mzururaji? Wa Tatanzania hiyo ni miaka yenu ya kuumia. mpaka mshike adabu kwa wrong choice ya uprezida
   
 16. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #16
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 3,810
  Likes Received: 1,047
  Trophy Points: 280
  Vipi na wewe ulipewa?
   
 17. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 695
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 80
  Kama ukiwa na kashfa huna hatia mpaka itakapodhihirika, mbona Katibu Mkuu Jairo kaambiwa asikanyage wizarani?
   
 18. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 3,079
  Likes Received: 1,955
  Trophy Points: 280
  MASA BURI bado ni Meya na anawakilisha jamii. HAFLA hiyo ilikuwa jijini dar so kama meya lazima aalikwe ikulu that is protocal; angekuwa amepewa barua ya likizo ili kupisha uchunguzi kisha mr president akampa mwaliko hiyo ni kesi ingine. msimamisheni kwanza!!!!

  "DONT MAKE OTHER PEOPLE LAUGH AT YOUR BACK"
   
 19. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,422
  Likes Received: 677
  Trophy Points: 280
  Jairo wizarani ni kazini kwake na amesimamishwa kazi, vipi ukiacha kutumia Masaburi yako kufikiri unadhani Masaburi amesimamishwa kazi yake au Ikulu ni ofisini kwa Masaburi?
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Inawezekana kabisa Mayor Masaburi akawa hana hatia,ni mtu safi, lakini kwa kipindi hiki ambacho yuko kwenye uchunguzi si busara hata kidogo kuonekana kwenye hiyo picha na Rais. Psychologically inampa Mayor Masaburi nguvu kubwa sana.

  Kitu kingine ambacho kinanipa shida ni nani analipia hizi futari za kila juma? Nauliza hili kwa nia njema kabisa, na natambua hiki ni kipindi muhimu kwa waislam na nilitegemea Rais angefutarisha watu lakini (LAKINI) sikutegemea angefutarisha kwa kasi hii. Nchi masikini ambavyo inakopa kila kukicha kwa nini Rais anashindwa kutambua concept ya 'kubana matumizi'?.

  Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi nusura ikwame kwa sababu ya kukosa fedha, Raisi yeye anazo mpaka za kununua zawadi kwa Watuhumiwa wa rushwa? Umpe mtu chakula na zawadi pia? Washauri wa Rais wanafanya nini? Kwanza mmeona hiyo mifuko ya zawadi? ni kiasi gani mfuko mmoja? Hawa waliofutarishwa wana njaa gani mpaka wapewe chakulana Rais?.

  Kama ni lazima kufutarisha kila juma basi wafutarishwe watoto yatima na wasukuma mikokoteni. Hawa ndio wanataka chakula lakini sio wakina Mayor Masaburi.

  Sijui tumefikaje hapa. Sijui!
   
Loading...