Bunge kusitisha uuzwaji UDA? 270 Milioni zaingizwa akaunti ya Idi Simba

Wana JF,

Mwl.Nyerere aliwasema sana ile May Mosi 1995 kule mbeya viongozi wa serikali wanauza mashirika ya UMMA alishangaa sana, hii nikutokana viongozi kuwa na tamaaa za ajabu, Kuipinga azimio la Arusha, urafi wa madaraka, kutokuwa waadilifu, wazalendo, kadri siku zinavyo kwenda maozo yote aliyoyasema baba wa Taifa yatajitokeza huyo mzee aliwaachia raana hawa viongozi wetu, tena enzi hizo hawa viongozi walikuwa ni vijana kabisa sasa ndio worse kabisa wanazeeka na watakufa na vitu vyote vya UMMA
 
Amakweli serikali hii imejaa uwuzi na ni watu wasio na huruma nadhani kinachofuata ni kuprivitise hata ule mjengo pale magogoni. Hawa ni manyang'gau kama Hayati baba wa taifa alishawahi kuwaitata " Mabeberu" yenye uchu wa mali za watanzania.
 
Very sad news, sikudhania mzee mkongwe Idd Simba ni machafu to that much..
 
ʞontɹact Sniper;2308937 said:
Tanzania......kati ya nchi rahisi zaidi kuongozeka duniani.

Tatizo ni Viongozi wake ndio kabisa hawajui ni jinsi gani ya kuiongoza Tanzania badala yake wao ni kuifirisi nchi basi
 
Binafsi nawashukuru wale ambao walituletea hili jambo kwa mara ya kwanza; japo hoja ya awali ilikuwa ni suala la kuuzwa tu kwa sisi wengine kilichotutisha zaidi ni mantiki ya kuuzwa kwake as it relates to DART. Bado hoja haijajengwa vizuri ya kuiunganisha DART na UDA kwa sababu bado - tusipoangalia - watafanya vile walivyofanya kwenye TRL ambapo pamoja na kuibinafsisha vibaya bado wanafikiria kubinafsisha tena!

UDA ni lazima irudishwe mikononi mwa wananchi wa JIji la DAR iwezeshwe na kwa kuanzia ipewe wa kuingiza mabasi mapya makubwa ya UMMA yasiyopungua 150 lengo likiwa ni kuhakikisha ndani ya miaka mitano linafikia kuwa na mabasi yake ya UDA-DART (UDART?) KAMA 2000 Hivi na zaidi. Lengo kuu liwe ni kuhakikisha vipanya na vidaladala vinaondolewa Dar usafiri wa mabasi unatolewa na shirika la Umma ambalo pita litasimamia ujenzi wa light rail transit. Wafanyabiashara wengine waachiewe kuingia kwenye biashara ya Taxis, tour transportations, na short distance transportation.

Mwanakijiji hii sinema bado sana na nashauri watanzania wasishangilie.

UDA ni kama EPA wakiingia vibaya ni aibu tupu. Hii kitu pamoja kwamba inamhusisha mtu kwenye 1st family, yumo kigogo toka Tabora amepata kuwa waziri, pia yumo kigogo wa CRDB bank. Waziri wa fedha analifahamu hili kwa karibu sana kuliko mtu mwingine - huyo msajili atahukumiwa bure tu.
Hivi sasa mazungumzo yalikuwa yanaendelea kumshawishi Mkulo aachie hisa za serikali zilizobakia nadhani watatulia kidogo vumbi litulie.

Mwekezaji anashikilia title deeds za UDA kwa sasa na sioni wa kumnyang'anya vinginevyo serikali itaishia kulipa mabilioni.
Leo wanazungumzia kwamba wameshajipanga kuagiza mabus 26 kwa gharama ya Paundi zaidi ya laki moja kwa kila bus (sh6.5 billion) hii yote ni kujiweka kwenye mazingira ya kuramba mapesa pindi mkataba ukivunjwa watadai fidia ya hasara.

Bahati mbaya haya yanafanyika machoni pa mkuu wa nchi hivyo kufanya vita yetu kuwa ngumu zaidi
 
Kaazi kwelikweli. Bw Simon grp aanze na Simba Na Mstahiki yuko wapi tunahitaji neno lake kwenye hili.
 
[video]http://www.bbc.co.uk/news/world-middle-east-14384691[/video]
Natamani ingetokea kama hii, lakini watanzania ni waoga na walalamishi, tumeibiwa vya kutosha,, tumedharaulika vya kutosha, tumedangwanywa vyakutosha, na bado tunasema hewala bwana, ni nani aliyetuloga?. Tunalalamika tu.
 
[video]http://www.bbc.co.uk/news/world-middle-east-14384691[/video]
Natamani ingetokea kama hii, lakini watanzania ni waoga na walalamishi, tumeibiwa vya kutosha,, tumedharaulika vya kutosha, tumedangwanywa vyakutosha, na bado tunasema hewala bwana, ni nani aliyetuloga?. Tunalalamika tu.
the saga begins beget war
I draw first blood be the first to set it off
 
hongereni sanaaaaaa EMT (huwa nakukubali sana mkuu unavyojitoaga sadaka kwa ajili ya taifa), Mwanakijiji na wengineo, nasema bila ya nyinyi isingekwenda kwa kasi hii.
 
Wanasiasa wengi bongo wanamikono michafu na sijui pia wanatumia nini kufikiri, yaani mtu akiuza nyumba kariakoo mitaa ya livingstone anapata billioni moja, nyumba yenyewe hata milioni hamsini hafiki lakini wasomi na wasiasa wakiuza kampuni yenye estate za maana na asset za kufa mtu wanapata billioni hiyo hiyo.

Simba alikuwa mzawa alipozuia wakina Manji wasiuziwe UDA, kumbe walikuwa wanatia mikono yao ashakum si matusi hawa wazee kuna kitu wanataka watanzania wawafanyiea manake kila dili majina ni hayo hayo. Kiukweli hata mapato ya Ubungo terminal yalitakiwa kwenda UDA ndio nyumbani kwa maikarusi.

Bravo M. Mwanakijiji kwa kusimamia na kuasisi misingi ya JF kwa facts na details, ila usafiri DSM unahitaji private sector pia kama ilivyo katika miji mingine duniani kufikiria kuondoa daladala ni makosa. Ushindani ni lazima na soko ndio litaamua nani aondoke sio siasa.
 
Jamani ifike sehemu wale wote wanaohusika na mikataba na madili ya ajabu ajabu dhidi ya Taifa hili,wathibitishwe kama kweli ni Raia wa dhati wa Taifa hili.

Ni hofu kwa mtizamo wangu kuwa uenda kuna hujuma za chini kwa chini zinazoendeshwa na wahujumu wa Taifa hili ambao kama wakifatiliwa wanaweza kuwa sio raia wa Taifa hili hivyo wao kufanya hayo pasipo hofu yoyote ya uzalendo.

Naomba walinzi wa Taifa hili waanze kutathimini na kufuatilia watu hao,uenda tukaona jambo fulani kwa jicho jingine.
 
Nadhani mzee Simba anaendeleza sera yake ya UZAWA, lol
 
Hivi hawa viongozi wa mwaka 47 wanashindwa kujua kwamba wakati huu sio wakati ule? Yaani wamekaa na kujadili na kuamua kujiuzia shirika la Umma bila aibu yoyote! Halafu mtu na akili zako unaelekezwa kudeposit pesa kwenye akaunti ya mtu, naye anaweka fedha! Ama kweli kuna watu bado wamelala sana usingizi wa pono.

Kweli tunapaswa kusimama kidete kuhakikisha kuwa UDA inaendelea kubaki mikononi mwa wana Dsm
 
Tatizo sijawasikia wabunge waliokuwa wanapigia kelele fedha za Jairo!!! where are they at!?

Tayari wameamuka Mwanakijiji katika bajeti ya Wizara mama kwa UDA.

Nadhani Bunge linapaswa kuiga mtindo wa USA na UK ambapo Kamati za Bunge za Kudumu zinakuwa chini ya Katibu wa Kamati hiyo ambayo ni Mtaalam aliyebobea katika sekta husika na kunakuwepo na secretariet ya hiyo kamati ambayo ipo chini ya katibu ambayo ni timu ya wataalam wa fani hizo (Hawa wanakuwa siyo wafanyakazi wa Serikali kabisa wataalam wa Bunge, kwa sasa wabunge wetu wanategemea wataalam hao hao waliotengeneza uozo serikali ndio waje kuwapa ufundi wa swala fulani); UK Katibu na secretariet ya Kamati za kudumu za House of Commons ni wataalam waliobobea kabisa na makatibu wengi ni Wahadhiri katika vyuo vyao vikuu wanavyoviamini sana kwa taaluma husika.

Kwa maana hiyo tulitegemea kamati ya kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge letu liwe na Katibu wake na secretariet yake ambayo imejaa wataalam wa madini, sheria na Umeme na labda Katibu angekuwa Professior au Dr mmoja wa University of Dar es Salaam, sasa mtu kama January hawezi kujuwa lolote katika fani hiyo na hata akija kujuwa kupitia JF unakuta tatizo limekomaa; au hili swala la UDa kama anavyosema Mwanakijiji kama Kamati za Kudumu za Bunge zingekuwa na secretariet huru ya wataalam waliobobea labda maneno ya Mwanakijiji kuwa hili swala la UDA kuuzwa lina uhusiano na DARTS!?

Nashauri Chedema waweke hii kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2015 maana pamoja na kuleta tija katika maamuzi ya Bunge lakini kwanza itatowa nafasi kwa Wataalam wetu katika vyuo vikuu kuitumikia nchni yao moja kwa moja na pili kuongeza nafasi za ajira kwa wataalam wetu ambao labda wapo nje ya nchni au wapo mtaani bila kazi. Nina uhakika kama kamati ya kudumu ya Kilimo na Mifugo ya Bunge ingekuwa chini ya wataalam wetu wa SUA pale Morogoro mambo yangekuwa sawa sawa kabisa
 
Hapa siungi mkono hoja, Monopoly hatuitaki tena hapa, ilishashindwa! sijaona monopoly hapo Tanesco, DAWASA, na TRL na UDA (hapo zamani) imesaidia nini. waingie wapambane na private, labda tu kuwe na standard ya mabasi yanayotakiwa.

Nadhani ni busara kuunga au kutokuunga mkono kwa jambo unalolijuwa! Kama hulijui alafu unatoa ushauri lazima ujikute unapotosha swala husika
 
Mkuu, hiyo Point ya kuwatumia wataalamu kutoka Vyuo Vikuu nayo ni mhimu sana. Ila tatizo ni hawa wataalamu waliosoma PhD kwa miezi 6 utashangaa ndiyo eti watawekwa kwenye hizo kamati kama wataalamu.

Nafikiri la muhimu ni nchi kuwa inafuata SHERIA. Ukiboronga basi wanaku-CHINA.

Tayari wameamuka Mwanakijiji katika bajeti ya Wizara mama kwa UDA.

Nadhani Bunge linapaswa kuiga mtindo wa USA na UK ambapo Kamati za Bunge za Kudumu zinakuwa chini ya Katibu wa Kamati hiyo ambayo ni Mtaalam aliyebobea katika sekta husika na kunakuwepo na secretariet ya hiyo kamati ambayo ipo chini ya katibu ambayo ni timu ya wataalam wa fani hizo (Hawa wanakuwa siyo wafanyakazi wa Serikali kabisa wataalam wa Bunge, kwa sasa wabunge wetu wanategemea wataalam hao hao waliotengeneza uozo serikali ndio waje kuwapa ufundi wa swala fulani); UK Katibu na secretariet ya Kamati za kudumu za House of Commons ni wataalam waliobobea kabisa na makatibu wengi ni Wahadhiri katika vyuo vyao vikuu wanavyoviamini sana kwa taaluma husika.

Kwa maana hiyo tulitegemea kamati ya kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge letu liwe na Katibu wake na secretariet yake ambayo imejaa wataalam wa madini, sheria na Umeme na labda Katibu angekuwa Professior au Dr mmoja wa University of Dar es Salaam, sasa mtu kama January hawezi kujuwa lolote katika fani hiyo na hata akija kujuwa kupitia JF unakuta tatizo limekomaa; au hili swala la UDa kama anavyosema Mwanakijiji kama Kamati za Kudumu za Bunge zingekuwa na secretariet huru ya wataalam waliobobea labda maneno ya Mwanakijiji kuwa hili swala la UDA kuuzwa lina uhusiano na DARTS!?

Nashauri Chedema waweke hii kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2015 maana pamoja na kuleta tija katika maamuzi ya Bunge lakini kwanza itatowa nafasi kwa Wataalam wetu katika vyuo vikuu kuitumikia nchni yao moja kwa moja na pili kuongeza nafasi za ajira kwa wataalam wetu ambao labda wapo nje ya nchni au wapo mtaani bila kazi. Nina uhakika kama kamati ya kudumu ya Kilimo na Mifugo ya Bunge ingekuwa chini ya wataalam wetu wa SUA pale Morogoro mambo yangekuwa sawa sawa kabisa
 
Tarehe 27 Julai 2011 vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Meya Wa Jiji la Dar es salaam Dkt. Didas Masaburi akieleza kilichoitwa maamuzi ya Baraza la Madiwani wa Jiji kuhusu kuvunja uongozi wa Shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) na kuunda kamati ya kuchunguza matatizo katika shirika hilo.

Tarehe 28 Julai 2011 vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Meneja wa UDA, Victor Milanzi akimjibu Meya Masaburi kwa pamoja na mambo mengine kugoma kuondoka katika nafasi hiyo na kukanusha tuhuma zilizoelekezwa juu yake kuhusu ubadhirifu wa fedha za mauzo ya hisa za shirika hilo.Kwa nafasi yangu ya ubunge ni mjumbe katika Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es salaam ambalo lina hisa 51% katika Shirika hilo na pia nawajibika kushiriki kuisimamia serikali kuu ambayo ina hisa 49% katika kampuni hivyo inanibidi kutoa kauli kuhusu upotoshaji unaondelea kufanywa na Meya Masaburi pamoja Meneja Milanzi kuhusu kashfa hii kupitia vyombo vya habari.Naomba wakazi wa Dar es salaam na wananchi watanzania kwa ujumla wafahamu kwamba Meya Masaburi na Meneja Milanzi wote wawili ni sehemu ya matatizo ya UDA kwa kushiriki kwa kiwango kikubwa katika kukiuka sheria, kanuni na taratibu kwenye uendeshaji wa shirika bila kuzingatia kwa ukamilifu maslahi ya wasafiri na walipa kodi.Meya Masaburi na Meneja Milanzi wote kwa nyakati mbalimbali wameshiriki katika kuachia maamuzi ya kifisadi ya kuuzwa kwa bei chee kwa hisa za kampuni ya UDA bila ya kuzingatiwa kwa sheria, kanuni na taratibu.

Meneja Milanzi ameshiriki kuanzia hatua za mwanzo za mkataba kati ya UDA na Kampuni ya Simon Group mwaka 2009 wakati Meya Masaburi ameshiriki katika kubariki utekelezaji wa mkataba huo wa kifisadi mwaka 2011 bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi wa Dar es salaam.
Meneja Milanzi na bodi ya Wakurugenzi chini ya uenyekiti wa Iddi Simba wameshiriki katika kuingia mkataba mbovu na wa kifisadi wa mauzo ya kampuni hiyo huku sehemu ya fedha za malipo zikiingizwa kwenye akaunti za watu binafsi. Meya Masaburi ametekeleza mkataba huo kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya umma kwa yeye binafsi kuhamisha umiliki wa kampuni ya UDA kwa Simon Group baada ya malipo ya milioni 285 tu sawa na asilimia 12.5 ya mauzo ya hisa hizo kupitia maamuzi yake ya tarehe 10 Juni 2011 wakati UDA ina mali zenye thamani ya zaidi ya bilioni 12.Baada ya kufanya maamuzi hayo kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya wananchi Meya Masaburi amejaribu kujikosha kwa maamuzi batili ya vikao haramu vya kamati ya fedha na uongozi cha tarehe 29 Juni 2011 na Baraza la Madiwani la tarehe 20 Julai 2011.

Kwa nafasi yangu ya ubunge ni mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi na pia ni mjumbe wa baraza la Madiwani na tarehe 20 Julai 2011 nilieleza mbele ya waandishi wa habari kwamba vikao hivyo vyote viwili vilikuwa batili kwa kuwa viliitishwa bila kuzingatia sheria na kanuni pia vilifanya maamuzi haramu ambayo hayakuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi wa Dar es salaam.Kama nilivyoelekeza kusudio siku hiyo, nitatoa waraka kwa wananchi wa Dar es salaam na mamlaka husika wenye kueleza msingi wa kupiga kura ya HAPANA siku hiyo kwa maamuzi yote haramu yaliyofanywa na vikao hivyo batili na kueleza kwa kina vifungu vya sheria, kanuni, mkataba na taratibu zilizokiukwa pamoja na kuwataja wa majina wahusika na kiwango cha fedha kilichotolewa. Hata hivyo, kabla ya kutoa waraka huo nimeona nitoe taarifa hii kwa umma ili mamlaka zote zinazohusika ziingilie kati na kuchukua hatua za haraka kunusuru mali na mwelekeo wa shirika la UDA.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kuingilia kwa kuchukua hatua stahiki za kuingoza serikali kupitia upya mkataba ulioingiwa na kutekelezwa kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya wananchi kati ya Jiji, UDA na Simon Group Limited. Maamuzi yaliyofanywa na Meya Masaburi na vikao vyake haramu vya jiji na vya UDA yanapaswa kubatilishwa. Aidha maamuzi ya bodi ya UDA chini ya uenyekiti wa Iddi Simba kwa miaka kadhaa yanapaswa kupitiwa upya kwa kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya umma.Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo anapaswa kuingilia kati kupitia Msajili wa Hazina na CHC ili kunusuru hisa za serikali kuu katika UDA pamoja na mali za shirika kwa ujumla wake.

Izingatiwe kwamba tarehe 28 Februari 2011 ofisi ya Waziri Mkuu iliandika barua yenye kumbukumbu namba CAB. 185/295/01/27 ambayo Katibu Mkuu Hazina anayo nakala yake yenye kueleza bayana kwamba uuzwaji wa hisa ambazo hazijagawiwa (unallocated shares) uliokuwa ukifanywa na UDA haukuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma na kuagiza mchakato huo usitishwe na CHC kushirikishwa. Izingatiwe kwamba katika maamuzi haramu yaliyofanywa na Meya Masaburi tarehe 10 Juni 2011 Wizara ya Fedha (hazina) na CHC wote hawakushiriki kwenye kikao kilichoitwa cha wana hisa wa UDA wakati serikali kuu imekuwa na hisa 49%.
Kamati husika za Bunge hususani ya Miundo mbinu na ya Hesabu za Mashirika ya Umma ziingilie kati kwa haraka kwa kushirikiana na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi ya Umma(PPRA) na wabunge wa mkoa wa Dar es salaam.

Hatua hizo za haraka zitaokoa mali za umma, kuweka msingi wa kuboresha usafiri katika mkoa wa Dar es salaam na kuwezesha hatua za kisheria na kinidhamu kuchukuliwa kwa wahusika wote waliofikisha jiji na taifa katika hali hiyo.Ikumbukwe kwamba masuala ya Mashirika na Makampuni yaliyo chini ya jiji la Dar es salaam nilianza kuyahoji katika vikao hususani vya kamati ya fedha na uongozi mara baada ya kuingia katika utumishi wa umma kwenye Halmashauri ya Jiji kupitia mikutano ya mwezi Machi na Mei 2011.Hata hivyo, badala ya Mstahiki Meya Masaburi kuchukua hatua stahiki kama ilivyoazimiwa katika vikao hivyo akaenda kufanya maamuzi binafsi ambayo yameongeza ukubwa wa matatizo badala ya kuyapunguza.Kutokana na hali hiyo mwezi Juni nikaamua kutumia fursa za kibunge katika kushughulikia hatma ya UDA na usafiri mkoani Dar es salaam kwa ujumla wake.

Hivyo, wakati wa mjadala wa Azimio la kuliongezea muda Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) tarehe 23 Juni 2011 nilihoji kwa maandishi kuhusu mauzo ya hisa na mali za kampuni ya UDA na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa kwa kurejea pia ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) . Hata hivyo, Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo kwenye majumuisho yake hakutoa kauli wala kuchukua hatua za haraka pamoja na kuwa hatma ya hisa 51% za shirika hilo zinahusu Wizara yake kupitia Msajili wa Hazina.Nikarudia tena kuhoji kwa maandishi wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa tarehe 23 Juni 2011 nikipinga uuzwaji wa hisa za UDA bila maslahi ya usafiri wa wananchi wa Dar es salaam kuzingatiwa na kutaka kuwe na uhusiano baina ya hatma ya UDA na Mradi wa Mabasi yaendayo kwa Haraka (DART) ambao unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Nilihoji suala hilo kama sehemu ya hitaji la kuwa na mfumo thabiti wa Usafiri wa Halaiki wa Umma (Mass Public Transit) ambao utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza adha ya usafiri katika jiji la Dar es salaam.
Hatahivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika majumuisho ya bajeti yake tarehe 1 Julai 2011 hakutoa kauli wala kuchukua hatua za haraka za kunusuru hali ya mambo pamoja na kuwa yeye ndiye mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hivyo ana wajibu wa kufuatilia masuala ya kisheria, kinanuni na kimikataba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kama ilivyo kwa halmashauri zingine.

Baada ya hapo ndipo kashfa ya UDA ikaanza kujitokeza kwenye vyombo vya habari tarehe 11 Julai 2011 ikiwa katika sura ya mzozo baina ya Meneja Milanzi na Mkurugenzi Kisena wa Simon Group Limited katika hatua za kulazimishana kuondoka ofisini.Kufuatia hali hiyo tarehe 15 Julai 2011 baada ya majibu ya swali la msingi nililouliza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ukaguzi maalum wa mahesabu na ufisadi katika kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) niliuliza swali la nyongeza kuhusu kashfa ya kampuni ya UDA kutokana na uhusiano wake na mradi wa DART ambapo maeneo ya UBT na UDA yatahusika. Katika swali langu nilitaka hatua za haraka kuchukuliwa na serikali kutokana na mauzo hayo kuendelea bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi hata hivyo Naibu Waziri Aggrey Mwanri hakutoa majibu ya kuridhisha wala kuchukua hatua zinazostahili kufuatia suala hilo hali ambayo ilitoa mwanya kwa Meya Masaburi kuendelea na mchakato haramu. Katika muktadha huo nitaendelea kushirikiana na madiwani wenzangu wenye kutanguliza mbele maslahi ya umma ikiwemo wabunge wa mkoa wa Dar es salaam ambao mimi ni katibu wao pamoja na mamlaka zingine za kiserikali na kibunge katika kushughulikia suala hili.

Natoa mwito kwa wananchi wa Dar es salaam kutuunga mkono katika kulifuatilia kwa karibu suala hili na kuchukua hatua zinazostahili kila mmoja kwa nafasi yake.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (Mb)Bungeni-Dodoma31 Julai 2011
 
hongera kamanda mnyika kwa kuchokonoa ufisadi huu japo kwenye baraza la madiwani wa jiji walikuchakachua coz mlikuwa wawili tu wajumbe kutoka upinzani, bt juhudi zako sasa zinaonekana na jamii inajua nini kimefanyika hapo UDA. Na c masaburi anajifanya anasimamia haki wakati yeye mwenyewe ni muhusika.
 
wahenga walishasema. Mvunja nchi ni mwananchi. na huu ni mfano mdogo tu wa jinsi tunavyoivunja nchi yetu wenyewe...Iddi vipi hushibi babuu? mpaka lini kupata mishiko?

Halafu Si ndo huyu IDD Simba amabaye alikomalia Uzawa huyu? Kumbe alimaanisha ajichukulie vitu vya umma kwa uzawa wake?
I wapi NICCO aliyoiendesha kiunjanja ujanja akaiua? Lakini naamini hapa mwisho wake umefika.....like always CRIME Never pays in the long run.....
 
Back
Top Bottom