Bunge kusitisha uuzwaji UDA? 270 Milioni zaingizwa akaunti ya Idi Simba

Natamani kulia nikiikumbuka hii kumbakisa

UDA.jpg
mimi nimeshaanza kulia....dar ilikuwa dar enzi hizo,,..sio leo fujo tunashindwa hata pa kukanyaga,..
 
wahenga walishasema. Mvunja nchi ni mwananchi. na huu ni mfano mdogo tu wa jinsi tunavyoivunja nchi yetu wenyewe...Iddi vipi hushibi babuu? mpaka lini kupata mishiko?
 
hivi mna imani na CAG?huyu hawezi kumfunga mtu,anaweza kufichua uozo if he wants to..kama hawa mafisadi wameweza kuwalazimisha majaji kupindisha sheria(mgombea binafsi,zombe),watashindwa vipi kuminfluence CAG kwenye hii saga ya UDA(ukichukulia ridhiwan ana maslahi)....hizi presidential appointments is a piece of sh*t
 
Hamna mtu aliyeloose direction,kuna watu wanafikiri kama wewe ni mwanachama wa CCM,basi wewe ni fisadi au unatetea ufisadi.But let's get back to the topic.

Kwahiyo kwako kila anyeipinga serikali na ufisadi ni chadema?? manake mag3 alikuwa anazungumzia serikali na thread hii inazungumzia ufisadi ambao unafanywa na viongozi wa serikali, kwa serikali kushindwa kuuthibiti ni sawa na kusema ndiyo inaupalilia.

Hata kama unaichukia chadema for any reason, unaihusisha na suala hili ambalo linagusa moja kwa moja maslahi ya wananchi lazima tukushangae.

Anyway tuendelee na mjadala.
 
akipewa huyo SIMON hiyo part haitotimia na VIPANYA watakuwa wanamnunua kila siku ili hasiwekeze zaidi
shughuli ya usafirishaji ni huduma sio biashara

sisi tuna nini? tuige basi huko tunakokwenda safarini kila siku, NEW YORK (metro, london underground na buses zote ni za council na sio hiyo miji tu ni yote ) wenzetu wanamiliki usafiri kama umma

Ahsante "Vikwazo"
Hapa ndio mgoto wa fikra za "uongozi" wa nchi yetu....
Tulipowekewa wimbo wa kubinafsisha na "wakubwa wa dunia"

Tukakoma kujiangalia kama sisi pia ni watu na taifa lenye mazingira yake na asili yake,
Ok hiyo sawa basi tumeshindwa hata kuangalia tu wenzetu wanavyofanya katika huo "ubinafsishaji"??
Na bado kila siku tunashinda kwenye nchi hizi za wakubwa na tunaona tafsiri yao ya "huduma za umma" na hatujifunzi kitu!
 
mambo baaaado! tz mambo baaaado, nasema mambo baado! kenya wanazidi kuingia, hata kwa usafiri wa bodaboda wanavuka mipaka, wahindi ndo usiseme, wachina wanaingia makontena kwa makontena utafikiri bidhaa, yote hayo nikukimbilia shamba la bibi, shamba hili jama muda si mrefu litakuwa janga, kila leo linavamiwa na nguruwe pori. looh!
 
Sasa TAKUKURU wanasubiri tuwapelekee ushahidi!! Prosecuter bwana Feleshi Unasubiri nini kesi ipo wazi? Ama kweli Tanzania sheria ni kwa ajili ya Maskini tu na Vibaka wadogo!! Shame on this country!!

Umesahau sarakasi za Takukuru na DPP?
 
Mkwe,hahahahaaa,watasema wao hawafanyi kazi kwa maneno ya magazetini
<font size="4"><font color="#ff0000">Sasa TAKUKURU wanasubiri tuwapelekee ushahidi!! Prosecuter bwana Feleshi Unasubiri nini kesi ipo wazi? Ama kweli Tanzania sheria ni kwa ajili ya Maskini tu na Vibaka wadogo!! Shame on this country!!</font></font>
<br />
<br />
 
So sad,lakin wanasema kelele za mpangaji
mambo baaaado! tz mambo baaaado, nasema mambo baado! kenya wanazidi kuingia, hata kwa usafiri wa bodaboda wanavuka mipaka, wahindi ndo usiseme, wachina wanaingia makontena kwa makontena utafikiri bidhaa, yote hayo nikukimbilia shamba la bibi, shamba hili jama muda si mrefu litakuwa janga, kila leo linavamiwa na nguruwe pori. looh!
<br />
<br />
 
Mali ya umma inauzwa pesa zinakwenda kwa account binafsi ya Mwenyekiti wa Bodi, Duh! kweli ili ni fumbo lenye maswali mengi kuliko majibu.
Huyu Mwenyekiti wa Body Iddi Simba si ndiye aliyeuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na kulazimishwa kujiuzulu mwaka 2002 kwa kashfa ya kutoa vibali vya kuingiza sukari Tanzania?, baadae akapewa Shilrika la Umma la Wakala wa Meli Tanzania (NASACO ) akaliuwa chap-chap. Baada ya hapo kumbe safari iliendelea na kupewa shirika lingine la Umma - UDA. Sasa nalo analiuza na pesa kutia kwapani (akaunti yake binafsi). anyway nitarudi baadae.

Mambo kama haya ndiyo yaliyoifisha nnchi hii hapa ilipo leo!!! Mtu ana haribu hapa anapelekwa kule, anauwa kule anahamishiwa pale...mifano hai anagalia ATC nani wameifisha hapa ilipo leo...rudi nyuma jiulize kabla ya huyo Jamaa kuja ATC alitokea wapi...je huku kulikuwaje...twende Shirika la Bima la taifa.....twende RTC....yapo mengi tuuu...Twende TSA (Tanzania Sisal authority) leo hii imebadilishwa jina inaitwa KATANI LTD....na etc etc ....huu ufisadi wa siku hizi amin usiamini ni urithi wa hawa wa leo ndani ya lizee CCM...kutoka kwa watangulizi wao..Hata leo siunaona Mtu anatuhuma wazi wazi ushahidi wazi wazi wa barua...anapewa likizo ya malipo (kulindana)
 
Watu wanaturushia vumbi pamoja na tope kwa gari za kifahari yaliyonunuliwa kwa pesa zetu.
 
huyu kisena nae chizi tu.iweje aweke pesa kwenye akaunt ya mtu binafs bila kudadisi eti kisa management ya UDA imesema!!!!

halafu huyu kisema ni rafiki mkubwa sana na ridhiwan kweli wameingizwa choo cha kike......huyu huyu idd simba ni mwizi toka zaman hata hiyo pride tanzania anaiendesha kiwizi wizi tu
Huyu bwana Mdogo mbona mambo yake ya mashaka mashaka, rafiki zake nao wa mashaka mashaka? Mie nadhani kuwa mtoto wa rais kisha kujiingiza kwenye deal za mashaka mashaka au kuwa na marafiki wenye records chafu ni jambo ambalo linastahili kukemewa sana na hasa na BABA YAKE (Rais mwenyewe).
Tumeyaona nchi nyingi kama kule kwa Saddam na wanae, Mubarak hata Gaddafi jinsi inavyokuwa ngumu sheria kuchukua mkondo wake pale watoto wa viongozi wanapoachiwa wajiingize kwenye vitendo vya uvunjifu wa sheria. Kinachojitokeza zaidi kwa hali hiyo ni raia kuongeza chuki juu ya Baba yake (Rais).
 
Binafsi nawashukuru wale ambao walituletea hili jambo kwa mara ya kwanza; japo hoja ya awali ilikuwa ni suala la kuuzwa tu kwa sisi wengine kilichotutisha zaidi ni mantiki ya kuuzwa kwake as it relates to DART. Bado hoja haijajengwa vizuri ya kuiunganisha DART na UDA kwa sababu bado - tusipoangalia - watafanya vile walivyofanya kwenye TRL ambapo pamoja na kuibinafsisha vibaya bado wanafikiria kubinafsisha tena!

UDA ni lazima irudishwe mikononi mwa wananchi wa JIji la DAR iwezeshwe na kwa kuanzia ipewe wa kuingiza mabasi mapya makubwa ya UMMA yasiyopungua 150 lengo likiwa ni kuhakikisha ndani ya miaka mitano linafikia kuwa na mabasi yake ya UDA-DART (UDART?) KAMA 2000 Hivi na zaidi. Lengo kuu liwe ni kuhakikisha vipanya na vidaladala vinaondolewa Dar usafiri wa mabasi unatolewa na shirika la Umma ambalo pita litasimamia ujenzi wa light rail transit. Wafanyabiashara wengine waachiewe kuingia kwenye biashara ya Taxis, tour transportations, na short distance transportation.

YAANI, YAANI! Huu ndio ufumbuzi wa usafirishaji abiria katika jiji! Hivi ndivyo wenzetu wanavyofanya kama kule Sweden! Ukiwa na Shirika (na tuna uzoefu na haya kama mnakumbukwa enzi za VIDECO - Kwa mliokuwa Moshi, au SHIMAWIMO) moja la jiji, ni rahisi kupanga ticketing - mnatoa ticket za msimu na kila bus unapanda kwenda popote, kama ni ruzuku ya usafiri inaweza ikafanywa kwa kupitia shirika hilo. Kazi kubwa iwe ni kuthibiti shirika kama hilo- KUFYEKA WATU KAMA HAO SIMON NA SIMBA, WAKAE MBALI SANA NA SHIRIKA KAMA HILO.

MZEE NAKUVULIA KOFIA
 
Back
Top Bottom