Anheuser
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 1,944
- 662
Wabongo mbona mnaingizwa mikenge kirahisi wajameni? Yani unaamini mtu mwenye milioni 270 hana sophistication ya kujua kwamba huwezi kununua hata kiatu, acha kampuni ya milioni 270, viatu vya yebo yebo kwa kuweka hela kwenye akaunti ya mtu binafsi ambae si mmliki hiyo mali? Kweli mnaamini hawa wawili lao si moja?...Iliyobakia hapa ni huyo "kidume cha mbegu" Robert Kisena kumfuata Iddi Simba na kumpa mkong'oto wa kufwa mutu kama alivyomfanyia yule OCD au sijui ODC kule Shinyanga. Maana ni wazi ishatoka hiyoo!! Milioni 270 alizolipa hatarudishiwa. Safi sana!
Na kuingiza hela kwenye akaunti, especially transaction ya magnitude kubwa kama hiyo, ku deposit huwa ni hatua za mwisho kabisa za mikataba ya mauzo, lazima kuna paperwork ndefu ilifanyika na kubadilishana kabla hujampa mtu milioni 270, hizo paperwork zinasemaje, alipewa karatasi gani huyo anaejifanya kaibiwa? Kama hakuna paperwork kwenye transaction ya mil 270 basi ni mchoro tu huu, wanawachezea Watanzania wadanganyika.