Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
...........Natoa mwito kwa wananchi wa Dar es salaam kutuunga mkono katika kulifuatilia kwa karibu suala hili na kuchukua hatua zinazostahili kila mmoja kwa nafasi yake.
Wenu katika utumishi wa umma,
John Mnyika (Mb)Bungeni-Dodoma31 Julai 2011
Mh. Mnyika nina mambo mawili tu ningependa kufahamu toka kwako, na bila shaka leo ndio bajeti ya wizara ya uchukuzi inajadiliwa;
Je umejaribu kutafuta nafasi ya kuchangia ili kuliweka wazi suala hili ambalo inaonekana masaburi amejitahidi kuwahi kuwahadaa wananchi ilihali kumbe naye ni mnufaika wa ufisadi huu?
Kama ikitokea serikali imeng'ang'ania msimamo wake wa kuifisadi UDA, mmejiandaaje kukabiliana na uamuzi huo?