Bunge kusitisha uuzwaji UDA? 270 Milioni zaingizwa akaunti ya Idi Simba

Natamani kulia nikiikumbuka hii kumbakisa

UDA.jpg

Tumeambiwa kuwa huyu Robert Kisena na kampuni yake ya Simon Group nia yao kubwa ni kumiliki fixed assets za UDA, kwa maana ya majengo na ardhi, haswa yard ya UDA kubwa sana kule Kurasini iliyopo karibu kabisa na Bandari ili baadaye waigeuze kuwa Container Terminal. Nakumbuka enzi zangu za shule ya msingi miaka ya 80 kabla ya daladal, ukikamatwa huna tiketi kwenye UDA, basi utapelekwa kwenye hiyo yard yao kule Kurasini kusafisha mabasi. Mimi naombea dili nzima ifie mbali, na hata hizo milioni 270 alizolipa asirudishiwe, na ikibidi aende Mahakamani kudai arudishiwe.

Wamwachie tuu hii ni bahati yake, Sasa hivi Tanzania ni kujizolea upatapo fursa mpaka nchi itakapokuwa na "Viongozi",

Lengo kuu liwe ni kuhakikisha vipanya na vidaladala vinaondolewa Dar usafiri wa mabasi unatolewa na shirika la Umma ambalo pita litasimamia ujenzi wa light rail transit. Wafanyabiashara wengine waachiewe kuingia kwenye biashara ya Taxis, tour transportations, na short distance transportation.

Hapa siungi mkono hoja, Monopoly hatuitaki tena hapa, ilishashindwa! sijaona monopoly hapo Tanesco, DAWASA, na TRL na UDA (hapo zamani) imesaidia nini. waingie wapambane na private, labda tu kuwe na standard ya mabasi yanayotakiwa.

vitu vtatu vifanyike,
1) Iddi Simba atoe maelezo ya malipo hayo, na afikishwe mahakamani mapema
2) Management ya UDA ilio elekeza pesa ziwekwe kwenye private account ya Iddi Simba ichukuliwe hatua za kisheria
3) Mr Kisena wa Simon Group, HAsirudishiwe hizo hela, na uchunguzi ufanyike kujua anafahamu kiasi gani mchezo huu mzima

hii serikali haipo serious, hii UDA si ilikua imekufa muda mrefu tu, hiyo management na board zilikua zinafanya kazi gani miaka yote hii, walikua wanalipwa kwa kazi ipi?

Binafsi nawashukuru wale ambao walituletea hili jambo kwa mara ya kwanza; japo hoja ya awali ilikuwa ni suala la kuuzwa tu kwa sisi wengine kilichotutisha zaidi ni mantiki ya kuuzwa kwake as it relates to DART. Bado hoja haijajengwa vizuri ya kuiunganisha DART na UDA kwa sababu bado - tusipoangalia - watafanya vile walivyofanya kwenye TRL ambapo pamoja na kuibinafsisha vibaya bado wanafikiria kubinafsisha tena!

UDA ni lazima irudishwe mikononi mwa wananchi wa JIji la DAR iwezeshwe na kwa kuanzia ipewe wa kuingiza mabasi mapya makubwa ya UMMA yasiyopungua 150 lengo likiwa ni kuhakikisha ndani ya miaka mitano linafikia kuwa na mabasi yake ya UDA-DART (UDART?) KAMA 2000 Hivi na zaidi. Lengo kuu liwe ni kuhakikisha vipanya na vidaladala vinaondolewa Dar usafiri wa mabasi unatolewa na shirika la Umma ambalo pita litasimamia ujenzi wa light rail transit. Wafanyabiashara wengine waachiewe kuingia kwenye biashara ya Taxis, tour transportations, na short distance transportation.

akipewa huyo SIMON hiyo part haitotimia na VIPANYA watakuwa wanamnunua kila siku ili hasiwekeze zaidi
shughuli ya usafirishaji ni huduma sio biashara

sisi tuna nini? tuige basi huko tunakokwenda safarini kila siku, NEW YORK (metro, london underground na buses zote ni za council na sio hiyo miji tu ni yote ) wenzetu wanamiliki usafiri kama umma

Trust no one,ukiamin hivo mambo yako yatakuwa mazuri,hela kazipeleka PRIDE akawanyonye wajasiriamali wanaoenda kumkopa
Hivi Iddi Simba ni mjinga hivi?? Nilikuwa namuona mtu wa maana na sera zake za uzawa kumbe ana lake! Kweli nimeamini hata kwenye CCM wapinga ufisadi si kweli wanapinga ufisadi bali wana ajenda yao nyingine!

See what I mean ? How does Chadema come into this ! Of course you are very right to call the issue of system crap because the likes of Symbion, like all parasites, cannot survive on their own. If you shelter filth, dont blame the flies and the cockroaches that come for a visit and end up settling permanently because of the comfort and security accorded them. Since you have chosen not to lay any blame on the system that owns the habitat for fisadis to flourish, what more can I say - good luck though not for long young man !
OOh! now it's Symbion?,what's the correlation? You have to take a stance,to privatise or not to privatise and how to go about that stance that you take.
Blaming the system is too general,is like telling the government to lower food prices while advocating for a free market system,it's like advocating for federated states while fighting for three governments in the union.
We have a very different view on how things should be done,your prophets voted for so many bills tha brought us here and today,in the name of peoples' power are acting as if that didn't matter at all!!
Some of your leaders were even trying to sell shares of NMB and Airtel at DSE,saying that would've generated some money for the government.So to me,my brother,all these politicians,no matter what party they represent are a bunch of loonies,they are not as revolutionary as they are supposed to be,we are arguing about UDA and why it's being privatised and not how......WAKE UP!!!

Unamaanisha haya mambo yafanyike kwenye ardhi yetu ya TANZANIA au nchi jirani
vitu vtatu vifanyike,

1) Iddi Simba atoe maelezo ya malipo hayo, na afikishwe mahakamani mapema

2) Management ya UDA ilio elekeza pesa ziwekwe kwenye private account ya Iddi Simba ichukuliwe hatua za kisheria

3) Mr Kisena wa Simon Group, HAsirudishiwe hizo hela, na uchunguzi ufanyike kujua anafahamu kiasi gani mchezo huu mzima

hii serikali haipo serious, hii UDA si ilikua imekufa muda mrefu tu, hiyo management na board zilikua zinafanya kazi gani miaka yote hii, walikua wanalipwa kwa kazi ipi?

IDD SIMBA bado ajakoma tu kuiba? hawa jamaa wote huyo aliyekwenda kuweka hela kwenye account ya IDD SIMBA na mwenyekiti wote ni wezi
uwezi kuweka hela zote hizo kwenye account bila kujua unaweza kwenye account ya nani

walitaka kuchukua shirika bure hiyo hela angerudishiwa SIMON GROUP

Kwa kasi hii ya kuibua ufisadi tanzania nadhani tunaelekea pazuri sana! nimeona hapo nukuu kwamba kuna watu wamejificha ndani ya uoza huu, can it be the one(s) discussed here?, riz1 & co?,

na huyo kisena, mbona wanatofautiana sana na simba kuhusu hizo fedha, ndio kusema tayari mwizi kaibiwa? Mungu ibariki tanzania, Mungu nibariki mimi na familia yangu

Natamani kulia nikiikumbuka hii kumbakisa

duuuh,hii bado ipo???route gani inaenda???

Kwa kasi hii ya kuibua ufisadi tanzania nadhani tunaelekea pazuri sana! nimeona hapo nukuu kwamba kuna watu wamejificha ndani ya uoza huu, can it be the one(s) discussed here?, riz1 & co?,

na huyo kisena, mbona wanatofautiana sana na simba kuhusu hizo fedha, ndio kusema tayari mwizi kaibiwa? Mungu ibariki tanzania, Mungu nibariki mimi na familia yangu

mungu aibariki JF

Nyie ngojeni tu mambo yatafumuka ndio tutajua template ya ufisadi inavyofanya kazi. Simba anasema fedha alizopewa ni za "usafirishaji" na jamaa labda aliamini ndio alikuwa analipia UDA. Kilichoenda kwa mganga kwa kweli hakirudi.. Kisena afungue kesi dhidi ya waliomuuzia.. Masaburi, Milanzi na Simba... sisi wengine tutakaa pembeni kuona jinsi gani tusivyoweza kufanya vitu vya msingi..

Mzee Mwanakijiji,

Hakika habari hizi zinaudhi,zinakera na zinatia kichefuchefu.

Huu ndiyo mfumo unaotumiwa na vigogo wa Serikali waliomo serikalini na waliostaafu. Ni UFISADI kwa kwenda mbele. Ndivyo yalivyobinafisishwa mashirika makubwa au kuingizwa kwenye ubia wa KIFISADI kama TTCL,TRL,NBC Bank,ATCL,TANESCO(NETGROUP SOLUTIONS) na mengine mengi.

Ukifuatilia kwa undani katika kila UBINAFSISHAJI/UGENISHAJI huo utakuta kwamba kuna mkono wa Kigogo wa serikali aliye kazini au retired. Mimi nafikiri umefika wakti sasa wa kuweka SHERIA YA KUNYONGWA KWA KUPIGWA RISASI kwa wote wanaobainika kujihusisha na UFISADI kama huu. Haijalishi mhusika ni RAIS MSTAHAFU,Waziri au Mbunge. Wote twanga risasi ili kuwe na nidhamu kama WANAVYOFANYA wenzetu wa-CHINA!!

Tumeshachoka kuyumbishwa na MAFISADI kila kukicha.

Idd Simba aliondoka Serikalini kwa kashfa ya Sukar. Sasa sijui ni vigezo gani wametumia hawa wakubwa kumpa uenyekiti wa bodi ya UDA maana hana historia ya uadilifu. Na anavyosema kuwa hizo milioni 270 zimeenda kwenye account yake kwa ajili ya 'usafirishaji, anaweza kusema tangu hela iingie 2009 amesafirisha nini?

Tukumbuke kwenye bunge la sasa issue ya CHC iliibua mjadala bungeni baada ya Mkulo kuiweka kwenye orodha ya 'kufutwa'! Ina maana kama CHC ingefutwa kumbukumbu za huu uzwaji wa UDA ungepotea vilevile maana hazina iliyotajwa kuchukua mikoba ya CHC haina record zozote!

Kinachonishangaza na kunipa hasira ni kwamba tangu badi Mzee Simba anashikilia hii nafasi ya Uenyekiti huku serikali imekaa kimya. Hata kama uchunguzi utafanyika kuwepo kwake ofisini kunampa nafasi kubwa ya kuvuruga uchunguzi. Mimi nilifiki la kwanza kabisa Meya, Mwenyekiti wa bodi na Accountant wasimamishwe kwanza kupisha uchunguzi huru.

Sasa TAKUKURU wanasubiri tuwapelekee ushahidi!! Prosecuter bwana Feleshi Unasubiri nini kesi ipo wazi? Ama kweli Tanzania sheria ni kwa ajili ya Maskini tu na Vibaka wadogo!! Shame on this country!!

• Thanks
Reactions: FJM
Tanzania inaangamizwa na kundi la watu wachache mno na wengine hawataki hata kujionesha usoni mwa watu. Inakuwaje issue nyingi chafu zinafanywa na mtu mmoja lakini Serikali haitoi tamko lolote bali ni kukaa kimya ama kushabikia. Mfano kwenye issue hii ya UDA Iddi Simba ameingia kwa kigezo cha kutatua tatizo la usafiri Dar. Idd Simba huyo huyo ndiye kinara wa uimilikishaji wa ardhi zaidi ya ekari laki saba huko Katavi kwa Kampuni ya Agrisol Energy ya Marekeni kwa kigezo cha kutekeleza azma ya Serikali ya Kilimo Kwanza.

Swali la kujiuliza ni kuwa Je! Watu kama Iddi Simba wanafanya mambo haya kwa baraka na masilahi ya Viongozi wa Juu Serikalini ama wanafanya mambo hayo kutokana na udhaifu wa viongozi wetu na Serikali kwa ujumla. Kama wanafanya mambo hayo kutokana na udhaifu wa Serikali na Viongozi wake; mbona pale mambo haya yanapogundulika Serikali inaamua kukaa kimya bila kuchukua hatua zozote?

Ama kweli Tanzania ni Shamba la Bibi ambalo kila mja anajitafunia atakavyo

That's where you lost the direction.

Chadema inaingiaje tena hapa?? watu mnaiogopa chadema kiasi kwamba kila kitu lazima mki-associate nayo??
Hamna mtu aliyeloose direction,kuna watu wanafikiri kama wewe ni mwanachama wa CCM,basi wewe ni fisadi au unatetea ufisadi.But let's get back to the topic.

IDD SIMBA fisadi wa kutupwa na sera yake ya uzawa kumbe yeye anatunyonya walalahoi!ndie alisababisha sukari ipande bei toka sh 450 kwa kg toka brazil mpaka sh 700 kisa kazuia importation huko yeye anaingiza kupitia mgongo wa jwtz.pia ametapeli kupitia kampuni feki ya NICOL

Sasa TAKUKURU wanasubiri tuwapelekee ushahidi!! Prosecuter bwana Feleshi Unasubiri nini kesi ipo wazi? Ama kweli Tanzania sheria ni kwa ajili ya Maskini tu na Vibaka wadogo!! Shame on this country!!

Ufanyaji wa kazi wa TAKUKURU wanaweza kutoa majibu mepesi mepsi kuwa hakuna aliyepeleka malamiko. As if kuwa hasomi na kuona taarifa kwenye vyanzo mbali mbali vya habari.

BTN

Yaaani kweli tanzania kuwa watu ufisadi umeshakuwa kama sysstem ya mzunguo wa damu. Yaani nimuhimu kwa maisha yao pamja na mali zote walizonanzo. Sasa mtu inakuwaje anaona mwamko wa watu kuamka usingizini na bado anapata ujasiri wa upiga madili ya kifisadi.

Ukipima kila ambacho kimekuwa kikiendelea katika hii "uza uza" ya mashirika yetu,

Ni wazi sana kuwa mwisho wa kufikiri kwa mfumo unaotawala na kusimamia mambo yetu kama nchi....

Na hii ni mbaya sana katika mustakabali wa kujenga "Taifa"

Sijawahi kumuangalia Simba kama shujaa, hivyo sishtushwi na hili.

Back
Top Bottom