Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,718
- 218,266
Nchini Tanzania kwa sheria za sasa , shambani kwako kukikutwa madini , basi haraka sana madini hayo na shamba lako hilo vinageuzwa kuwa mali ya serikali , na baada ya muda mfupi wataletwa wawekezaji wa kiarabu au wa kizungu kuchimba madini hayo , huku wewe ukitimuliwa kwa mijeledi au hata bunduki bila huruma .
Lakini kwenye shamba lako hilo kukikutwa Bangi jua umekwisha , utamilikishwa bangi hiyo na kupigwa pingu .
Sasa leo Tundu Lissu amesema kwamba atakayekuta madini kwenye eneo lake hayo madini yatakuwa yake .mwenyewe , ataamua cha kuyafanya
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lisu ametaja mambo manne yatakayorekebishwa kwenye sheria ya madini pindi chama hicho kitakapoingia madarakani ili kuwanufaisha wachimbaji wadogo nchini.
Lissu amesema hayo leo Jumatano, Septemba 6, 2023 wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni +255 Katiba mpya, eneo la Kinyambiga, Bunda mkoani Mara.
Amesema licha ya sheria ya madini kusema madini yote nchini ni mali ya umma chini ya udhamini wa Rais kwa niaba ya Watanzania lakini amedai kiuhalisia madini ni mali ya Rais.
Lissu amesema suluhisho la kwanza, Chadema itakapoingia madarakani ni kubadilisha sheria hiyo akidai madini yanatakiwa yawe mali kwanza ya wenye ardhi ambaye ataelewana na atakaye yagundua kwenye ardhi yake.
Pili, sheria iseme machimbo ambayo yanatakiwa yawe kwaajili ya wananchi wa kwetu tu na ukweli ni kwamba sheria ndivyo inavyosema ya sasa lakini shida ni CCM...hizi zinazoitwa PMR remaining licence hizi ni leseni zinazotolewa kwaajili ya watanzania," alisema Lissu akihoji wageni wanakujaje mahali hapo.
Alisema wananchi, vijiji, halmashauri na Serikali kuu wanatakiwa kunufaika na rasilimali ya madini yaliyopo kwenye maeneo yao.
Tatu, linalohitaji mabadiliko ni Serikali inapotoa leseni kwa kampuni kubwa lazima kuwe na mgawanyo wa umiliki na faida zake.
Nne, ni kushugulika na mamlaka ya Rais, akidai Katiba iliyopo sasa siyo tu inamfanya Rais amiliki rasilimali za nchi yakiwemo madini, misitu na wanyama pori bali pia inampa nguvu ya kumiliki nchi na watu wake.