Paul Makonda amuweka Afisa Madini wa Katavi kikaangoni

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amemtaka Afisa Madini Mkoa wa Katavi, Mhandisi Andrew Mwalugaja kuhakikisha anafuata sheria na taratibu za kuhakikisha utoaji leseni za uchimbaji madini unazingatia uzalendo huku uongozi wa mkoa ukisisitizwa kumaliza mgogoro ambao umedumu kwa muda mrefu.

Hayo yametokea katika mkutano wa hadhara ambapo wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Dilifu, kata ya Magamba wamesema Mlima Dilifu ambao ndio wenye machimbo ya dhahabu ni mali ya Wananchi wa kijiji hicho, ambapo wanakerwa na kupangiwa muwekezaji na kudai kunyimwa haki na uhuru wa uchimbaji huku wakidai wanapokonywa leseni ya uchimbaji katika machimbo yaliyoko ndani ya kijiji chao.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusufu amesema mbali na maridhiano kufanyika katika mgogoro huo lakini bado kuna baadhi ya watu wanakwamisha maridhiano ambayo yamekuwa yakifanyika.
 
Ni usanii mtupu!! Hakuna chochote Makonda atafanikisha. Anyway nchi ya wajinga waache wamfuate kama panya walivyomfuata mpiga filimbi wa Hamelin
 
Makongoroschunya kabisa wewe! inamaana ambao sio wajinga ni wachache kiasi hiko?

Kama ndivyo, kiongozi ataanzaje kusema ahudumie na kujali wasomi ambao hata theruthi kati ya wote hawafiki?

Chadema hicho ndo kinachowaangusha, kupuuza hao mnaowaita wajinga ili hali ndio wanaopiga kura kwa wingi

Wewe hata ukiulizwa umefanya nini popote pale huna jibu, kanyaboi mkubwa

Pumbavu kabisa
 
Wajinga kwani ndiyo wanapiga kura kumchagua Rais? Wajinga hata wakiwa milioni 59 hawawezi kuwazidi wenye akili Milioni 1.
 
Back
Top Bottom