Yaani the Public Private Partnership Act itakuwa na nguvu zaidi ya hiyo ya Maliasili.
Ukizingatia TPA ni Public na DPW ni private,
Sheria hii ya Ushirikiano wa Kampuni binafsi na Kampuni za Umma au kwa kimombo The Public Private Partnership Act, iliongezewa kifungu kinachotamka kuhusu Inconsistencies au Kutokubaliana kwa sheria nyingine(ikumbukwe hiyo ya maliasili ya 2017) hazikubaliani, kimesema:
Ambapo kuna kutofautiana na sheria nyingine yeyote iliyoandikwa kuhusiana na maendeleo, ununuzi, na utekelezaji wa ushirikiano wa kibinafsi wa umma, masharti ya sheria hii yatakuwa juu. (in essence the provisions of the PPP act shall prevail) Sasa nipo tayari kusahihishwa kuhusu "shall prevail".
Siyo hiyo tu kuna sehemu katika marekebisho ya PPPAct ambapo maneno yamefutwa na yameongezwa maneno yanayosema,
masharti ya sheria hii hyaathiri utekelezaji wa makubaliano ambayo hutoa mpangilio maalum(special arrangement)wa mradi wa kimakati katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo makubaliano hayo yameidhinishwa na baraza la mawaziri.
Tafuta PDF ujiridhie hapa
Public Private Partnership(Amendment) Act, 2023