Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,488
- 7,937
Pamoja na ukubwa na umaarufu wa Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla, mji ule hauna stendi inayoendana na jina lake, kuna eneo la wazi lenye vichochoro lukuki huku kukiwa hakuna urasmi wapi kwa kuingilia na kutokea pia nyakati za mvua hali ni mbaya.
Leo bungeni, mbunge wa viti maalum, Neema Lugangira amehoji ahadi iliyotolewa na makamu wa Rais kwa niaba Rais Samia Suluhu kujenga stendi ya kisasa mji wa Bukoba.
Majibu ya Silinde kwa niaba ya wizara ni kwamba wameainisha vipaumbele kwenye ahadi za viongozi na jukumu lao sasa ni kutafuta fedha kuhakikisha ahadi zinatekelezwa.
Najiuliza kwa hawa viongozi, unatoaje ahadi kumbe fedha za kutimiza ahadi hujui hata utazipata lini na utazitolea wapi! Yaani watu wachague katika ahadi sasa ndio waanze kutafuta fedha.