Stendi Kuu ya Arusha kuanza kujengwa ndani ya siku 30 zijazo

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Meya wa Jiji la Arusha, Maxmillian Matle Iranqhe amempongeza na kumshukuru Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geoffrey Pinda kufuatia maelekezo yake aliyoyatoa kuwa Ujenzi wa Stendi Kuu Arusha uanze ndani siku 30 nakuonya kwa yoyote anayekwamisha.

f1db50f6-32e7-4684-bb94-c104c5a37b41.jpg


MABORESHO STENDI YA SASA
Meya wa Jiji la Arusha, Maxmillian Matle Iranqhe amesema “Kuna mchakato wa ujenzi wa Stendi Mpya na pindi utakapokamilika, hiyo stendi ya sasa tutaipeleka katika Mipango Miji watatushauri cha kufanya

"Lakini lazima kuwe na maboresho kwa kuwa eneo lipo katikati ya Mji, siwezi kusema kwa kuwa mambo ya Halmashauri yanaamuriwa na vikao.

“Stendi ni ndogo, tangu wakati wa uhuru, kipindi kile Arusha ilikuwa na watu wachache na ilifaa kwa wakati huo, sasa hivi idadi ya watu ni kubwa na tulichoamua ni kuruhusu baadhi ya makampuni ya mabasi kuegesha nje ya stendi yaani maeneo tofauti.”


Pia soma:
Arusha: Kituo kikuu cha Mabasi ya kwenda mikoani chawa kero kwa watumiaji wake, hakilingani na hadhi ya jiji
 
Back
Top Bottom