Bukoba: Rais Magufuli ashuhudia utiaji saini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya LZ Nickel. 'Multipurpose Smelter' kujengwa Kahama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,947
141,927
Tukio liko mubashara TBC na Upendo tv.

Karibu.

Up dates;

=======

10:19 Asubuhi: Kinachoendelea kwa sasa ni sala na dua kutoka kwa viongozi wa dini, kabla uliimbwa wimbo wa Taifa.

Katibu Mkuu- Wizara ya Madini: Mheshimiwa wa Rais kwa heshima kubwa naomba kukukaribisha katika hafla hii ya utiaji saini mikataba baina ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kampuni ya LZ Nickel Limited.

Utiaji saini wa mikataba hii leo utawezesha kuanzisha kampuni ya pamoja yaani Tembo Nickel Corporation ambayo ni kampuni ya ubia ambayo itakuwa na wajibu wa kusimamia kampuni mbili ambazo nazo zinazaliwa leo kwa utiaji saini yaani LZ NICKEL MININGI LIMITED itakayoshughulika na uchimbaji wa nickel kule Kabanga wilayani Ngara na LZ nickel refining limited itakayohusika na ujenzi na uendeshaji wa kiwanda cha kuyeyusha madini mbalimbali yaani 'multi purpose minaral smelting industry' kitakachojengwa kule Kahama.

Utiaji saini wa leo ni muendelezo wa kazi nzuri na ngumu inayofanywa na timu ya serikali ya majadiliano, naomba pamoja na kwamba waziri wangu ataongea hapa, niwapongeze sana timu hii kwa kazi nzuri wanayofanya, hongereni sana.

Mkuu wa Mkoa-Kagera(Brig General Mark Gaguti): Kipekee na kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Kagera nikupongeze kwa ujasiri wako na dhamira yako ya kuzitetea rasilimali za Taifa hili Inawezekana ulipoanza na uperesheni makinikia wengi hatukukuelewa lakini naamini baada ya muda huu sasa, watanzania wengi wanakuelewa na wanakuunga mkono katika ddhamira hii ya kutetea rasilimali za Taifa.

SERIKALI YASAINI MKATABA NA KAMPUNI YA LZ NICKEL LIMITED

Hafla ya utiaji saini Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na Kampuni hiyo ya uchimbaji wa madini aina ya 'Nickel' kutoka Uingereza imefanyika Bukoba Mkoani Kagera leo Januari 19, 2021

Tukio hilo limeshuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliongozwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi amesema, mradi huo wa Kabanga uligunduliwa kutokana na utafiti uliofanywa na Serikali ya JMT kupitia uhisani wa UNDP kuanzia mwaka 1976-1979 ambao ulibainisha uwepo wa Madini ya 'Nickel'

Ametaja baadhi ya faida za mradi huo kuwa ni pamoja na mapato mrabaha, kodi, gawio. Pia, Waziri Kabudi amesema fedha zote zitakazotokana na mauzo ya Madini hayo zitahifadhiwa katika akaunti za Benki zilizopo Tanzania

RAIS MAGUFULI AAGIZA MRADI ULIOSAINIWA LEO KUANZA MARA MOJA

Dkt. John Magufuli ameagiza mradi wa madini ambao mkataba wake umesainiwa leo Mkoani Kagera kuanza mara moja akisema Watanzania wamesubiri mradi huo tangu mwaka 1976 na wamechoka na michakato

Amesema, anatumaini Mgodi huo wa madini ya Nickel ukianza kufanya kazi mapema mwaka huu, watakuwa na uhakika Ajira za Watu Milioni 8 zitapatikana kama walivyoahidi. Ameitaka Wizara ya Madini kuharakisha kwakuwa hakuna sababu ya kuchelewa

Aidha, amesema Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji hivyo Wawekezaje waje Nchini kwani kuna madini ya kila aina
 
Mbona nawaona mabeberu tena?

IMG_8413.JPG
 
Tukio liko mubashara TBC na Upendo tv.

Karibu.

Up dates;

=======

10:19 Asubuhi: Kinachoendelea kwa sasa ni sala na dua kutoka kwa viongozi wa dini, kabla uliimbwa wimbo wa Taifa.

Katibu Mkuu- Wizara ya Madini: Mheshimiwa wa Rais kwa heshima kubwa naomba kukukaribisha katika hafla hii ya utiaji saini mikataba baina ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kampuni ya LZ Nickel Limited.

Utiaji saini wa mikataba hii leo utawezesha kuanzisha kampuni ya pamoja yaani Tembo Nickel Corporation ambayo ni kampuni ya ubia ambayo itakuwa na wajibu wa kusimamia kampuni mbili ambazo nazo zinazaliwa leo kwa utiaji saini yaani LZ NICKEL MININGI LIMITED itakayoshughulika na uchimbaji wa nickel kule Kabanga wilayani Ngara na LZ nickel refining limited itakayohusika na ujenzi na uendeshaji wa kiwanda cha kuyeyusha madini mbalimbali yaani 'multi purpose minaral smelting industry' kitakachojengwa kule Kahama.

Utiaji saini wa leo ni muendelezo wa kazi nzuri na ngumu inayofanywa na timu ya serikali ya majadiliano, naomba pamoja na kwamba waziri wangu ataongea hapa, niwapongeze sana timu hii kwa kazi nzuri wanayofanya, hongereni sana.

Mkuu wa Mkoa-Kagera(Brig General Mark Gaguti): Kipekee na kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Kagera nikupongeze kwa ujasiri wako na dhamira yako ya kuzitetea rasilimali za Taifa hili Inawezekana ulipoanza na uperesheni makinikia wengi hatukukuelewa lakini naamini baada ya muda huu sasa, watanzania wengi wanakuelewa na wanakuunga mkono katika ddhamira hii ya kutetea rasilimali za Taifa.
Tutamuongezea muda huyu mzee
 
.....".Mh. JPM rais wa Tanzania amekomesha kuhomolwa kwa madini Tanzania....." by Prof. P. Kabudi

kuhomola = (neno jipya la kiswahili Tanzania) lenye maana ya kukwapua kiujanja ujanja mali ya mtu huku mwenye mali akishangaa tu!
Hahahaaaa..... Kiswahili kimekopa kutoka Ugogoni!
 
Tuipongeze kwa dhati serikali awamu ya tano kwa kuondoa unyonge na maslahi madogo binafsi ya wachache kuingia mikataba makini yenye tija.

Nimeilewa vizuri plan ya smelter ya madini, italeta mapinduzi makubwa ya uchumi kwa viwanda vya high tech karibuni.

Vyuo vikuu vyetu vifikiri mitaala ya sayansi kuunda accessories kadiri aina za madini batteries nk.
 
Back
Top Bottom