Bukoba: Ndege ndogo yapitiliza na kuingia ziwa Victoria

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,519
86,072
Kwa mujibu wa vyanzo vya mtaani kuna uwepo wa ndege ndogo imepitiliza na kuingia ziwa Victoria

---
Ndege yenye namba za usajili 9127 mali ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imepata ajali na kuanguka maeneo ya uwanja wa ndege manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Akizungumzia juu ya kutokea kwa ajali ya ndege hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera ACP Blasius Chatanda amesema kuwa, tukio hilo limetokea hii leo tarehe 20 Julai mwaka 2023 mnamo majira ya saa 3:30 asubuhi.

Kamanda Chatanda amefafanua kuwa ndege hiyo ilikuwa katika mafunzo yanayoendelea ambapo ndani yake walikuwemo marubani wawili ambao ni Meja Renadi Revokatus Mkundwa Muha mwenye umri wa miaka (45) pamoja naye Luteni Alex Venance Moshi Mchaga umri miaka 30.

Amesema kuwa watu hao wawili wamepelekwa hosptalini na kufanyiwa uchunguzi kiafya hivyo wamebainika kuwa salama na kuruhusiwa.

Hata hivyo ameongeza kuwa chanzo cha ajali ya ndege hiyo hakikufahamika mara moja na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajari hiyo.

Mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amewashukuru jeshi la zima Moto na uokoaji pamoja na wadau wengine waliojitokeza na kuwahi kufika eneo la tukio mapema hatimaye kusaidia kuwaokoa marubani hao.





=====
Zoezi la uokoaji likiendelea huko Bukoba asubuhi ya leo 20, 07, 2023 baada ya Ndege aina ya Jet Fighter kudondoka ndani ya Ziwa Victoria.
 
Poleni kwa waliokua ndani ya ndege hiyo, hopes wote wametoka salama, ndugu zangu watanzania tuache upumbavu huu, hilo ni eneo la ajali sio picnic site, umati wote huo haukutakiwa uwepo hapo,je hiyo ndege ikilipuka hapo hamfikirii maafa yatakayokupata?

Hakuna kuchukua self au video kwenye eneo la ajali,ni vema vikosi vya uokoaji vikafanya kampeni ya kuwaelimisha wapumbavu hawa,stay away from accident/crime scenes for your own safe
 
Bukoba,Tanzania

Kwa kuingalia inaonekana ni ndege vita ya mafunzo yenye nembo ya jeshi la anga katika mkia wake.

1689848435002.png

Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Dr. Erasto Sima amethibitisha hilo. Ndege hiyo ilikuwa na marubani wawili kama zilivyo ndege za kivita.

Habari zaidi kutoka mamlaka husika zitatolewa, amesema mkuu wa wilaya ya Bukoba.

Mamlaka zinazohusika kutoa maelezo zaidi ni TCAA inayoongoza usalama wa anga Tanzania, mamlaka za viwanja TAA na TPDF / JWTZ
 
Back
Top Bottom