Kama katika Mazoezi ya Kawaida Ndege za Jeshi zinaanguka hivi Ziwani je, zikiwa Vitani si zitaanguka zote na Tanzania Kushambuliwa vilivyo na Adui?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,638
108,998
NDEGE ya Jeshi imeanguka Ziwa Victoria mapema leo Julai 20,2023 karibu na Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

 Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasia Chatanda amesema ndege hiyo ya jeshi yenye namba JW 9127, imeanguka wakati marubani wake wawili walipokuwa kwenye mazoezi ya kawaida.
Chanzo Taarifa: habarileo_tz

Kuna Kitu nataka Kuandika ( kutoa yangu ya Moyoni juu ya Jeshi letu kwa sasa ) ila ngoja ninyamaze na niende zangu DAR SERVICE PARK Kawe ( Ukumbi ulio eneo la Jeshi ) nikatizame Live Band huku nikizitizama Frames nyingi zilizojengwa hovyo hovyo upande wa Pili ( tena zikiwa ndani kabisa ) ya Kambi Kongwe, Kubwa na yenye Historia ya Kipekee ya Lugalo.

OMBI:

Tafadhali JWTZ ikiwapendeza msisahau kutupa Updates za Wanajeshi ( Marubani ) hao Wawili mliowakimbiza Hospitali Kuu ya Mkoa wa Kagera kwa Matibabu zaidi au kama Kesho mtawapakia katika Choppers zenu Kuwaleta Lugalo Military Hospital mtuambie ili GENTAMYCINE niwe wa Kwanza kwenda Kuwatembelea Jioni kuwapa Pole zangu.

Mwisho GENTAMYCINE nitoe tu pongezi Kwenu JWTZ kwa Kitendo chenu cha Kuitoa haraka hiyo Ndege yenu ya Jeshi Majini Ziwa Victoria tofauti na ilivyokuwa ile Ndege ya Precision Air ambayo hamkuwa Fasta kuitoa na badala yake Tapeli ( Samjo Samjo ) Majaliwa Jackson ndiyo akawa Mtawala wa Tukio zima na nyie Wanajeshi mkawa na Jukumu la Kuivuta tu Ndege kwa Kamba huku ( Yeye Muokoaji Samjo Samjo Majaliwa Jackson ) akisema alikuwa chini ya Maji ilikokuwa Cockpit ya Ndege akipungiana mkono na Marubani ambao walikuwa Wameshafariki Kitambo kwa mujibu wa Kifaa cha Kusoma Matukio ya Ndege Kiitwacho Black Box ( kwa Wenzetu Mliosoma) baada ya Uchunguzi kufanyika na wenye Akili Kubwa wa Kwanza duniani waitwao Wazungu.
 
Uwekezaji wa yale mafrem! Hua nikikunja kona pale kuelekea Kawe najisemea aliyeplan hili alikua na akili timamu au ilikuaje? Ni vipi akipanga gaidi frem kama tatu kwa biashara tofauti huku akiandaa mipango miovu ndani ya eneo lile itakuaje? Huo upuuzi huwezi kuukuta kwa General PK kwenye millitary base zake
 
Mama kaweka order... Mzigo upo njiani
B-2_Spirit_(cropped).jpg
Sukhoi_Design_Bureau,_054,_Sukhoi_Su-57_(49581303977).jpg
 
Uwekezaji wa yale mafrem! Hua nikikunja kona pale kuelekea kawe najisemea aliyeplan hili alikua na akili timamu au ilikuaje? Ni vipi akipanga gaidi frem kama tatu kwa biashara tofauti huku akiandaa mipango miovu ndani ya eneo lile itakuaje? Huo upuuzi huwezi kuukuta kwa General PK kwenye millitary base zake
Ulipomtaja tu Rais General Paul Kagame wa Rwanda umenifurahisha mno GENTAMYCINE Mkuu.

Nilihoji Mmoja wa Wakuu wa hapo kwanini wameruhusu huo Ujenzi wa hizo Fremu na nina uhakika nikikupa hapa Jibu nililopewa ( jjnsi lilivyokuwa la Kipumbavu ) utakasirika na hutowabeshimu tena Wapiganaji Vitambi Starehe Wetu.
 
NDEGE ya Jeshi imeanguka Ziwa Victoria mapema leo Julai 20,2023 karibu na Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

 Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasia Chatanda amesema
mbao walikuwa Wameshafariki Kitambo kwa mujibu wa Kifaa cha Kusoma Matukio ya Ndege Kiitwacho Black Box ( kwa Wenzetu Mliosoma) baada ya Uchunguzi kufanyika na wenye Akili Kubwa wa Kwanza duniani waitwao Wazungu.
Kenya helkopta to a jeshi leo jioni imeanguka ikiwa na maafisa wa jeshi. Take it easy brother
 
Ulipomtaja tu Rais General Paul Kagame wa Rwanda umenifurahisha mno GENTAMYCINE Mkuu.

Nilihoji Mmoja wa Wakuu wa hapo kwanini wameruhusu huo Ujenzi wa hizo Fremu na nina uhakika nikikupa hapa Jibu nililopewa ( jjnsi lilivyokuwa la Kipumbavu ) utakasirika na hutowabeshimu tena Wapiganaji Vitambi Starehe Wetu.

Wakati Mwalimu anaanzisha Leaders Club, ilikua viongozi mbalimbali wakanywe pale na waburudike sehemu ambayo watakua salama, na ili kulinda hadhi ya viongozi, na asilimia kubwa ya wahudumu pale waliwekwa watu wa kitengo, sasa ulikua ukilewa chakari ukaanza kuropoka kama kesho unaitwa msasani kwenda kupewa maneno yako, hapo sababu ya kuanzisha leaders ilikuepo vipi hizo fremu au vibanda tena wamejenga vidogovidogo ili wapate milango mingi sababu ya msingi ni ipi?
 
Waongeze bajeti kwenye wizara ya ulinzi iwe kwa kukopa na kuongeza maden lkn wajaribu kuongeza na kuiboresha bajeti ya jeshi letu jmn tunatia aibu.

Hii nchi kubwa sana ilitakiwa tumiliki au basi wasije sema nakosa uzalendo.

Anyway wanasema hii nchi jeshi letu huficha sana Mambo yake lkn ukweli ni kuwa tuko nyuma sana, tuko nyuma kitechnolojia mpaka kiakili yaan bado tunaishi ktk falsafa za majeshi ya miaka ya 90 huko ambako walitegemea nguvu ya kijeshi kwa idadi ya wanajeshi, minguvu na mikwara ya kuvunja mawe, leo hii ni tofauti,

Kinachohitajika ni Developed military tools za kurahisisha mapambano dhidi ya maadui, kuanzia Tools za angan kama Jets, Drones, pia za majini kama submarine, boti za uokozi, meli za kijeshi za kutungua makombora na kurusha makombora, tools za ardhini kama vifaru vya kisasa, magari ya kisasa, Radar na Vizuia makombora.

La mwisho Ufahamu/ujuzi wa kupata habari kwa haraka dhidi ya adui hili jambo linatakiwa kuzingatiwa sana na jeshi letu kwa nyakati za sasa pia mafunzo ya kisasa ya mbinu za upambanaji na adui yeyote mwenye mafunzo ya aina yoyote dunian, nina hakika uvamizi wa mrusi ungefanyika Bongo mpaka wale majamaa wenye zile jezi za Jeshi tungeongozana kujificha mapangoni(UTANI)

Nisiandike mengi kiufupi Viongoz wetu kama wanania njema na hii nchi Jeshi letu lilifaa kuboreshwa kuwa mfano bora wa kuigwa baran afrika kwa kila nyanja,

Au hii amani fake inatudanganya tujisahau kuboresha hizi changamoto?
 
Waongeze bajeti kwenye wizara ya ulinzi iwe kwa kukopa na kuongeza maden lkn wajaribu kuongeza na kuiboresha bajeti ya jeshi letu jmn tunatia aibu.

Nisiandike mengi kiufupi Viongoz wetu kama wanania njema na hii nchi Jeshi letu lilifaa kuboreshwa kuwa mfano bora wa kuigwa baran afrika kwa kila nyanja,

Au hii amani fake inatudanganya tujisahau kuboresha hizi changamoto?
Waongeze bajeti kutoka ngapi kwenda ngapi?
 
Wakati Mwalimu anaanzisha Leaders Club, ilikua viongozi mbalimbali wakanywe pale na waburudike sehemu ambayo watakua salama, na ili kulinda hadhi ya viongozi, na asilimia kubwa ya wahudumu pale waliwekwa watu wa kitengo, sasa ulikua ukilewa chakari ukaanza kuropoka kama kesho unaitwa msasani kwenda kupewa maneno yako, hapo sababu ya kuanzisha leaders ilikuepo vipi hizo fremu au vibanda tena wamejenga vidogovidogo ili wapate milango mingi sababu ya msingi ni ipi?
Mtani nionee Huruma nakaa nao Jirani.
 
Back
Top Bottom