RC Mwassa Awasihi Wananchi Kutochafua Ziwa Victoria Walilinde kwa Wivu Mkubwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
RC MWASSA AWASIHI WANANCHI KUTOCHAFUA ZIWA VICTORIA WALILINDE KWA WIVU MKUBWA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa amewataka Wananchi na wadau wa usafirishaji wanaofanya shughuli ndani ya Ziwa Victoria, kutofanya yale yote yanayoweza Kuathiri au kusababisha uchafuzi wa Ziwa Victoria ili kuendana na mpango wa Taifa wa kupambana na vitendo hivyo ikiwemo Vitendo vya umwagikaji wa Mafuta kwenye Ziwa na Bahari

Mhe. Mwassa ameyasema hayo wakati wa warsha ya mafunzo ya Siku tatu yaliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera Machi 20, 2024 yenye lengo la Kudhibiti Vitendo vya umwagikaji Mafuta ndani ya Ziwa, akiwa Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo, Mhe Mwassa ameeleza kwamba mafunzo haya yana umuhimu mkubwa kwa eneo la Mkoa Kagera kwakuwa pia Ziwa Victoria linagusa Wilaya za Mkoa Kagera, hivyo utunzaji wa Ziwa unagusa sana jamii yetu kwakuwa maji haya hutumika kwa kunywa, kula na shughuli nyingine za kibinadamu, na maji haya yanagusa hadi Mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa.

Mhe. Mwassa amesisitiza kuwa shughuli nyingine za uvuvi zimekuwa zikifanyika humo, hivyo endapo vitendo vya umwagaji mafuta katika Ziwa havitakomeshwa na wala kuchukuliwa hatua za kupambana navyo, itapelekea kukosekana kwa mazao ya Samaki na Samaki wenyewe kama kitoweo, na hii itaathiri upatikanaji wa samaki bora, ikiwa ni Pamoja na kupungua kwa pato la Mtu mmoja mmoja (mvuvi) na pato la Taifa, huku akitolea mfano Wilaya ya Muleba ambayo kwa asilimia kubwa mapato ya Halmashauri hiyo hutegema Shughuli za Uvuvi hasa Dagaa.

Aidha, Mhe. Mwassa amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri wa mapambano hayo na kuwa yale watakayofundishwa na kujifunza yakawe chachu ya kuendelea kudhibiti na kukomesha Pamoja na kushughulikia matendo kama hayo ya uchafuzi na umwagaji mafuta ziwani pale yatakapojitokeza.

Mafunzo haya muhimu kwa masilahi ya Taifa, ambayo ni mpango wa Kitaifa wa kudhibiti uchafuzi wa maziwa na Bahari kwa umwagaji wa mafuta yamekuja wakati ambapo Nchi za Jirani Uganda na Kenya wapo katika mchakato wa hatua za uchimbaji wa Mafuta Ziwani, ambapo Shughuli ikikamilika ya uchimbaji basi mafuta hayo yatasafirishwa
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.36.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.36.jpeg
    27.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.40.jpeg
    42.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.37.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.37.jpeg
    33.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.38(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.38(1).jpeg
    38.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.38(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-24 at 01.24.38(2).jpeg
    42.8 KB · Views: 1
Matumizi ya sumu kwenye uvuvi, imekuwa ni hatari kwa afya ya ziwa na binadamu kwa ujmla.

Samaki wamepungua sana na wengine wametoweka ziwani kiasi kwamba jitihada za ziada zisipochukuliwa kuna hatari ya kubaki na maji tu.
 
Back
Top Bottom