Break up. . .

Wa Tz ni mabingwa wa kujifanyisha na hatutambui kama Dunia ya sasa ni ya uwazi na ukweli. Mimi nikishachukua maamuzi ya kukumwaga nakupa live bila kupoteza muda, tena huku nakutazama usoni, sijui kujifanyisha kupenda, ukinywa sumu hutakuwa mtu wa kwanza kufa hapa Duniani. Isitoshe nimeshafiwa na watu wengi wa karibu kuliko wewe. Huu ni wakati wa kuita jembe, jembe, siyo kuita jembe kifaa cha kulimia.
 
Hiyo maneno haina FOMULA, unachukua maamuzi kulinaga na mazingira ya mahusiano yenu..................
Sidhani kama kuna mtu anaweza kusema hapa kwamba angependa aachweje......................Kwani wengi hawaijui siku wala saa, jambo hilo hutokea kama mwivi wa usiku................LOL
 
Wa Tz ni mabingwa wa kujifanyisha na hatutambui kama Dunia ya sasa ni ya uwazi na ukweli. Mimi nikishachukua maamuzi ya kukumwaga nakupa live bila kupoteza muda, tena huku nakutazama usoni, sijui kujifanyisha kupenda, ukinywa sumu hutakuwa mtu wa kwanza kufa hapa Duniani. Isitoshe nimeshafiwa na watu wengi wa karibu kuliko wewe. Huu ni wakati wa kuita jembe, jembe, siyo kuita jembe kifaa cha kulimia.

Na kweli haya mambo ya kunywa sumu hua tunaendekeza wenyewe. Nadhani watu wangekua wanaonyesha msimamo wa kweli hivyo vitisho visingetumika kuwekana ndani bila ya hiari.
 
My two cents' worth...

Getting jilted is a tough proposition, either way.

The only relief I see is when the decision is mutual.
 
hamna kitu kibaya kama uachwe na mtu unayempenda, ndo mana wengine wanakunywa sumu hivi hivi...kipende roho nyieee:rolleyez:
 
Na kweli haya mambo ya kunywa sumu hua tunaendekeza wenyewe. Nadhani watu wangekua wanaonyesha msimamo wa kweli hivyo vitisho visingetumika kuwekana ndani bila ya hiari.
Mie nadhan tatizo ile watu kutokuaweka wazi dhumun hasa la relation yenyewe na hii inatokea pale watu wala hawajajuana vizuri tayari wanapeana ahadi za ajabu wakishajuana na mmoja kugundua kabugi step ndio hayo mambo ya kujinyonga sijui kunywa sumu yanaanziaga hapo!
 
Kuna namna ambayo ni more suitable kuachana na mtu ambae let say hajakukosea zaidi ya kumweka chini siku moja na kumwambia "mimi na wewe hivi au vile. . . "?!? Yani unataka kumwacha kwa sababu zako binafsi (umemchoka, humpendi tena, umepata mwingine, umeona mahusiano yenu hayatoenda popote n.k)???!

Kama ni wewe mwachwaji. .unaprefer kuachwa mara moja (kashajua anakuacha akwambie mara moja) au kuachwa taratibu(anakutafutia pozz la kukuacha hata kwa miezi huku ukijua bado mpo kama kawaida)??! Kwanini?

Ndo maana ukifa watu wanalia sana
 
Mie nadhan tatizo ile watu kutokuaweka wazi dhumun hasa la relation yenyewe na hii inatokea pale watu wala hawajajuana vizuri tayari wanapeana ahadi za ajabu wakishajuana na mmoja kugundua kabugi step ndio hayo mambo ya kujinyonga sijui kunywa sumu yanaanziaga hapo!

True that. . .
Kuwekana sawa tangu mwanzo ni muhimu kwakweli. .sema watu ni wagumu sana kuwa wakweli. Mtu anaweza akawa hana kabisa malengo na mdada/mkaka wa watu ila anamwaminisha vinginevyo. . .alafu siku ya siku anaambiwa tu kirahisi "sitaki kuwa na wewe tena!!" Khaaa. . .
 
dah mi nikiona hizo dalili naachia ngazi mapema ili ionekane mmi ndo nimeacha na pia iasaidia kupunguza maumivu ati!
 
To be honestly wanajamvi me huwa nina ujasiri wa kifisadi... nikona mambo hayaeleweki namwambua tu "naomba kuanzia leo uhusiano uishe" akiuliza sababu najidai me ndo mwenye makosa ili yaishe.........
 
Wa Tz ni mabingwa wa kujifanyisha na hatutambui kama Dunia ya sasa ni ya uwazi na ukweli. Mimi nikishachukua maamuzi ya kukumwaga nakupa live bila kupoteza muda, tena huku nakutazama usoni, sijui kujifanyisha kupenda, ukinywa sumu hutakuwa mtu wa kwanza kufa hapa Duniani. Isitoshe nimeshafiwa na watu wengi wa karibu kuliko wewe. Huu ni wakati wa kuita jembe, jembe, siyo kuita jembe kifaa cha kulimia.

Mkuu upo kama mimi nakupa za usoni kabisa tena co simu wala sms.... live et
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom