Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,801
- 59,274
- Thread starter
- #61
Asante sana Watu8. . .Kwa jinsi ninavyoelewa, siku zote kuna aina tofauti ya mahusiano baina ya mwanamke na mwanaume.
1.Mahusiano ya kindugu
2.Mahusiano ya kirafiki
3.Mahusiano ya kimapenzi
4.Mahusiano ya kijamii
Sasa mie nitagusa hapo kwenye mahusiano ya KIMAPENZI:
Mahusiano ya kimapenzi nayo huwa yamegawanyika katika namna mbalimbali
1.Kuna mahusiano ambayo hatma yake ni ndoa, haya ni yale ya muda mrefu - Closed relationship
2.Kuna mahusiano ambayo hayana malengo yoyote, mahusiano ya wazi - Open relationship
3.Kuna mahusiano ya kingono tu. - sitaweka neno la kiingeereza kwani hili si jukwaa husika
Sasa basi wakati muhimu ya mahusiano ni mwanzo, hapo ndipo uhusiano uwekwa bayana baina ya wawili...
Break up inayohusu Uhusiano namba 1 bila shaka itakua ni ngumu na itawaumiza wahusika wote
Break up inayohusu uhusiano namba 2 na 3 nadhani haina madhara sana.
Sasa kutoa jibu kwa LIZZY nadhani namna bora ya kubreak up, ni kuzungumza kwa namna ileile ambayo ilitumika katika kuanzisha uhusiano kutegemea na LENGO lile la awali.
Basi inabidi consideration wakati wa kuachana iwepo zaidi iwapo mahusiano yalikua yenye malengo ya mbali kati ya wapenzi/wenzi hao. Zaidi ya hapo ni kiasi tu cha kupeana ruhusa kila mmoja akatafute wakumfaa zaidi.
jr. . .asante JR.. . nakubaliana na wewe.
Last edited by a moderator: