Break up. . .

Kwanini. . .. ?

kwa sababu anayekuacha anakuwa anauma na kupuliza hivyo japo unapoozwa bado unaumia kwa muda mrefu tu ukitumainia labda siku moja maumivu yataisha...ni sawa na kunywa vidongo vichungu kwa muda mrefu badala ya kuchomwa sindano kali kwa muda mfupi yaishe...
 
Kila siku ku break-up,ebu siku moja kuwe na topic ya ku make-up,itasaidia sana watu wengi kutengeneza pale palipoharibika kwenye mahusiano yao!AND mind u hakuna kisicho-expire,BUT Lucky enough mahusiano yana nafasi ya kuboreshwa,JITUME kuboresha ulicho nacho for ur betterment coz hakuna kijitoshelezacho.

GOD BLESS YOU and START NOW

We nawe. . .
Umeangalia humu jukwaani ukakosa? Zipo zimejaa tele. . .mimi binafsi nilishaandika kadhaa.
 
Unamweka chini unamwambia, akiendelea kung'ang'ania unapunguza mawasiliano mwisho unayakata kabisa. Hapo ndio mwisho wa mchezo.
 
Na hapo ndo panaponitatiza mie Canta.
Yani mwenzio ukute hata kashapata pakwenda baada yako au hata alishahamia ila wewe anakuweka akidhani anakusaidia kumbe anakupotezea muda wako na nafasi kwa watu wengine wanaohitaji/taka kuwa na wewe.
Hii hua ni mbaya sana ila km unakua ni mtu wa kumsoma mtu wako vizuri hata changes utazigundua tu,
Ila kwa namna tulivoumbwa sie wanawake hua tunachelewa kugundua hasa unapokua umependa na vinavooumiza ni vile visa hapokei simu,kila mara anakukwepa,anajidai amekua bize siku hizi,msg hajibu kwa wakati

km huna ufahamu wa kutosha na kuanza kufanya utafiti badala yake ndio unaishia kulia na kusononeka wakati wote kwa mda mrefu na mwisho wa siku hata mkikutana hamsalimiani,

Bora kuambiana mapema tu kwa kweli na km akili zilishakomaa kinachofata ni kukubali matokeo na kusonga mbele!

Ila hapa napo inabidi kumsoma na mtu mwenyewe maana kuna wanaume wengine pia hawako strong anaweza maliza hasira kwa kukudunda!!!
 
kwa sababu anayekuacha anakuwa anauma na kupuliza hivyo japo unapoozwa bado unaumia kwa muda mrefu tu ukitumainia labda siku moja maumivu yataisha...ni sawa na kunywa vidongo vichungu kwa muda mrefu badala ya kuchomwa sindano kali kwa muda mfupi yaishe...
Nimekusoma. .
Ila binafsi naprefer sindano nipate maumivu ya muda mfupi kuliko vidonge aisee.
 
No matter how, kuachwa na umpendaye ni kuachwa tu.
Hakuna njia rahisi, wewe unayetaka kuacha fanya upendavyo.

Haipunguzi maumivu.
Konnie mbona umekuwa mkali?
Kama ilivyo kukutana na kuanza mahusiano, hatua inayoweza kufuata ni kuachana. Tukubali tu na tuwe tayari kupata na kupoteza pale inapobidi.
 
Hii hua ni mbaya sana ila km unakua ni mtu wa kumsoma mtu wako vizuri hata changes utazigundua tu,
Ila kwa namna tulivoumbwa sie wanawake hua tunachelewa kugundua hasa unapokua umependa na vinavooumiza ni vile visa hapokei simu,kila mara anakukwepa,anajidai amekua bize siku hizi,msg hajibu kwa wakati

km huna ufahamu wa kutosha na kuanza kufanya utafiti badala yake ndio unaishia kulia na kusononeka wakati wote kwa mda mrefu na mwisho wa siku hata mkikutana hamsalimiani,

Bora kuambiana mapema tu kwa kweli na km akili zilishakomaa kinachofata ni kukubali matokeo na kusonga mbele!

Ila hapa napo inabidi kumsoma na mtu mwenyewe maana kuna wanaume wengine pia hawako strong anaweza maliza hasira kwa kukudunda!!!

Hahahaha. . .unatoa waraka wa kuachana unaambulia kipigo bila maelezo. . .kesho unarudi mwenyewe!!
 
Kuna namna ambayo ni more suitable kuachana na mtu ambae let say hajakukosea zaidi ya kumweka chini siku moja na kumwambia "mimi na wewe hivi au vile. . . "?!? Yani unataka kumwacha kwa sababu zako binafsi (umemchoka, humpendi tena, umepata mwingine, umeona mahusiano yenu hayatoenda popote n.k)???!

Kama ni wewe mwachwaji. .unaprefer kuachwa mara moja (kashajua anakuacha akwambie mara moja) au kuachwa taratibu(anakutafutia pozz la kukuacha hata kwa miezi huku ukijua bado mpo kama kawaida)??! Kwanini?
Namna yoyote ile ya kumuacha mtu anayekupenda inaumiza, iwe ya papo kwa hapo au ya kuchukua mwaka mzima. Kitu kikubwa kinachomuumiza muachwaji mara nyingi ni regrets anazokuwa nazo kama;
  • Am i not a man/woman enough?
  • What did i do wrong?
  • Na kama atagundua tayari una mwingine, ataanza kujilinganisha na huyo mwingine na mara nyingi hujikuta anajipa mapungufu mengi sana yeye mwenyewe.
Sababu hizi ndizo zinazosababisha mtu anayeachwa kuumia. Sasa papo kwa papo au taratibu ipi ni namna bora?
Kwa mtizamo wangu kuachwa kunapochukua muda mrefu kunaweza kuwa na maumivu zaidi kwasababu katika mchakato wa kuachana kuna mambo na matukio mengi yatakayojitokeza ikiwa pamoja na ugomvi na kila namna ya ghasia ambazo kwa namna moja au nyingine zitatengeneza maumivu zaidi ila kwa pande zote mbili.

Pili muachwaji hupata wakati mgumu sana katika kipindi hicho kujaribu kunusuru kuachwa hivyo jitihada zake zinapoonekana kushindwa hutengeneza maumivu mengine makubwa zaidi. Ingawa maelezo yangu bado hayasemi kuwa papo kwa papo ni nzuri zaidi maana mwisho wa siku kama muachwaji alikuwa anapenda kwa dhati ni lazima ataumia tu.

Ushauri wangu, kama muachaji anaona mahusiano hayo hayana future ni bora akayamaliza mapema kabla ya wote wawili kujenga hisia kali (pamoja na kuacha bado muachaji pia huumia)
 
Kwa jinsi ninavyoelewa, siku zote kuna aina tofauti ya mahusiano baina ya mwanamke na mwanaume.

1.Mahusiano ya kindugu
2.Mahusiano ya kirafiki
3.Mahusiano ya kimapenzi
4.Mahusiano ya kijamii

Sasa mie nitagusa hapo kwenye mahusiano ya KIMAPENZI:
Mahusiano ya kimapenzi nayo huwa yamegawanyika katika namna mbalimbali
1.Kuna mahusiano ambayo hatma yake ni ndoa, haya ni yale ya muda mrefu - Closed relationship
2.Kuna mahusiano ambayo hayana malengo yoyote, mahusiano ya wazi - Open relationship
3.Kuna mahusiano ya kingono tu. - sitaweka neno la kiingeereza kwani hili si jukwaa husika

Sasa basi wakati muhimu ya mahusiano ni mwanzo, hapo ndipo uhusiano uwekwa bayana baina ya wawili...
Break up inayohusu Uhusiano namba 1 bila shaka itakua ni ngumu na itawaumiza wahusika wote
Break up inayohusu uhusiano namba 2 na 3 nadhani haina madhara sana.

Sasa kutoa jibu kwa LIZZY nadhani namna bora ya kubreak up, ni kuzungumza kwa namna ileile ambayo ilitumika katika kuanzisha uhusiano kutegemea na LENGO lile la awali.
 
Hahahaha. . .unatoa waraka wa kuachana unaambulia kipigo bila maelezo. . .kesho unarudi mwenyewe!!

Yani nimekumbuka kuna mdada wakati tuko chuo jamaa yake alikua anamdunda yani km kamuoa siju asa ikafika siku mdada akachoka alafu akawa keshapata jamaa mwingine anajua kucare na anayemuheshimu eti akamwita jamaa na kumwambia kuazia leo mimi na wewe basi nimepata mwingine!

Hahaha hahah ahah alipigwa mpaka akalazwa na alipotoka huko jamaaa akasema akimjua huyo anayetaka kumnyang'anya atakiona cha moto mdada akaogopa ikabidi aendelee naye tu mpaka tulipomaliza chuo!
 
Hataaaaaa!!
Wengine hua tunasubiri anaetoka atoke, kudekiwe, vyakufuliwa vifuliwe, vyakuoshwa vioshwe, hewa safi iingine, air freshner ipulizwe alafu ndo mgeni mwingine akaribishwe!!!
Lizzy ....you are special! Heri yake atakayekuoa!
 
Sijawahi kuwacha na sitakuja wacha....poleni sana mnao penda penda kila kukicha.

Therefore mtu kama mimi, ni vigumu kuwachwaaaa.

Afu kwenye mila zetu wanawake hawawachi wanaume ni aibu....yani vigumu sana mwanamke kuniwacha mimi.

Shaaaaa.
 
Kila siku ku break-up,ebu siku moja kuwe na topic ya ku make-up,itasaidia sana watu wengi kutengeneza pale palipoharibika kwenye mahusiano yao!AND mind u hakuna kisicho-expire,BUT Lucky enough mahusiano yana nafasi ya kuboreshwa,JITUME kuboresha ulicho nacho for ur betterment coz hakuna kijitoshelezacho.

GOD BLESS YOU and START NOW
Super,katika tasnia ya media wanasema......'dog bite man no story,man bite dog big story'. Usicheze na story za heartbreak.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom