BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

hii kitu itakuja kuleta mambo mazito sana huko serikalini

naamini hawa watu wa mafuta wana ushahidi mzito sana wa rushwa EWURA, WIZARA, TPA, TRA na kwingineko

the question is je serikali hii inaweza kuvumilia hizi tuhuma nzito toka kwa hawa watu wa mafuta?

my answer is no they wont stomach any criticisms
 
Yale makampuni manne yaliopewa 24hrs, wangejua kabla adhabu ambayo wangepewa ndio hii,, wangeendelea na mgomo. Wanajuta kwanini waliogopa wakatii amri.
 
Hili ni changa la macho kwa sababu ninachojua mimi ni kuwa serekali ina share BP (T)
 
Naanza kuwa na shaka kwamba issue nzima ilipangwa na serikali ikifikiri itacheza vizuri mwishoni na ionekane inamaamuzi magumu, kumbe wamejimaliza, sijaona adhabu hata moja hapo, ukisikia kiini macho ndicho hiki, kwa waliokaribu na hawa watu waambieni wajaribu njia nyingine WTZ hawadanganyiki siku hizi uelewa wao uko juu mno.
 
habari inachanganya ...............yaani unasema nguruwe haramu asiuzwe reja reja uzwe kwa jumla ..........hapa pana namna ...

kiini macho tu , yan ccm maamuzi yao kama nguvu za giza.
Wanatapatapa tu , na kama kweli ni maamuzi yenye tija kwa nn wasifanye ktk mambo yote yanayosumbua wananchi , wanasubiri mpaka wasikilizie upepo vp?

"WOTE SEMA -MWISHO WA CCM NI 2015"
 
Hivi wakuu tumeshawahi kujiuliza ni kwanini bei elekezi za EWURA hua ziko juu kuliko bei za rejareja za makmpuni mengi tu ya mafuta hapa nchini?
Hivi wakuu tumeshawahi kujiuliza kuwa pamoja na bei elekezi kuwa juu ya zile za makampuni mengi tu ya mafuta bado bei za makapuni hizo zinabeba asilimia tatu (3%) kama tozo ya EWURA?

Hivi wakuu tunajua athari ya makampuni makubwa ya mafuta kuwekewa mazingira magumu ya kibiashara kwakuwa hayatoi rushwa kwa mamlaka za serikali kama EWURA

Hivi wakuu tunajua athari za makampuni makubwa ya nishati kushindwa kufanya biashara na kuondoka nchini kama vile shell, BP, Agip nakdhalika? tunajua athari zake wakuu

Hivi leo hii bigbon akipewa kazi ya kupeleka mafuta ya jet kwenye viwanja vyetu vya ndege kama afanyavyo BP, tunajua nini kitatokea?
 
Hamna wanachofanya,
Hapa inanikumbusha kisa kimoja hivi wakati tuko Sekondari,
Wanafunzi wote tuligoma kutokana na uongozi mbaya wa shule,
Katika vinara wa ule mgomo alikuwako mtoto wa mwenye shule.

Basi katika waliofukuzwa nae akawepo,
But eti baba yake ndie alieandika barua ya kumuombea mwanae uhamsiho aende shule ingine.

Hapo mzazi alijua kua mwanae akikosa shule hata yeye angekua matatizoni kama mzazi.
Hapa hata kama BP wasipouza wakapata hasara, mwisho wa siku shareholders (akiwemo Serikali) ndio watakaopata hiyo hasara,
Pili mia tano za kila lita nazo watazikosa pia.

Mnaweza kusifia lakini ki ukweli haisaidii hata kidogo,
Nafanya kazi katika mojawapo ya vituo vinne vilivyooewa onyo,
Ukweli watu wanauza Petrol tu ambayo mgogoro wake ni wa "Old Stock" tu kwani kodi haijashuka,
wakati Diesel hatuuzi kwani inahusisha pia na mgogoro mwingine wa "Price Calculation", so bado tumegoma.
 
Haki ya mungu tanzania patakuwa kama tunisia au misri,

mimi napata hasira kuona serikali imegoma kuuza mafuta, kwani bp inamilikiwa na serikali nusu kwa nusu, cha msingi serikali ingeuza mafuta yake na kuishitaki bp 50% sasa wote wamegoma ndio nini, unaweza je kumshitaki mtu wakati maamuzi yanafanyika mkiwa wote wawili.

Kama bp puma energy wamegoma, basi bp tanzania (serikali iuze mafuta) kwani wote wanamiliki kwa uwezo sawa, all of them are majority shareholder, they are equal in power.


Hakuna mtanzania atakaye kuwa na akili mbovu kama hii kuwa bp imegoma while anujua bp ni 50% serikali
mweeeeeee kabisa, nitatoboa kibodi yangu bure sheeeeetap
 
EWURA yenyewe ni double standard,wanawezaje kusimamia petrol,diesel na kerosine na kuacha mafuta ya ndege bila usimamizi wake!?
 
mbona mi naona kama wameruhusiwa kuuza mafuta...katika maelezo hayo sioni usitishwaji wowote wa kutouza mafuta
 
Haki ya mungu tanzania patakuwa kama tunisia au misri,
mimi napata hasira kuona serikali imegoma kuuza mafuta, kwani bp inamilikiwa na serikali nusu kwa nusu, cha msingi serikali ingeuza mafuta yake na kuishitaki bp 50% sasa wote wamegoma ndio nini, unaweza je kumshitaki mtu wakati maamuzi yanafanyika mkiwa wote wawili.
Kama bp puma energy wamegoma, basi bp tanzania (serikali iuze mafuta) kwani wote wanamiliki kwa uwezo sawa, all of them are majority shareholder, they are equal in power.
Hakuna mtanzania atakaye kuwa na akili mbovu kama hii kuwa bp imegoma while anujua bp ni 50% serikali
mweeeeeee kabisa, nitatoboa kibodi yangu bure sheeeeetap

Unasahau kua JK aliiongoza CC ya Chama chake kuiambia Serikali anayoiongoza mwenyewe ishushe bei ya Mafuta?
Ukistaajabu ya Magamba utayaona ya Ewura!!!
 
Back
Top Bottom