BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

sasa subiri DPP atakavyo fungua mashtaka ya kitoto. Mwisho wa kesi hii ni BP kushinda na serikali kudaiwa fidia
 
mwanzo mzuri , ila kwenye kumshtaki huyo mkurugenzi wa BP ,serikali itashinda kweli au ni kupotezeana muda tu ?

Mh! Na lube oil je.....?
Kwa sababu biashara kubwa ya BP ni Jet Oil na lube oil, hayo ya sijui mafuta ya taa, sijui dizeli/petroli kwao si core bussiness na ndo mana walifanya makusudi wakijua wazi kuwa hata mkiwafungia kwa hayo "mafuta ya ewura" bado wataendelea kupeta tu.
Walistahili kufungiwa kwa bidhaa zote sio kubagua bidhaa. Hapo hakuna adhabu.
 
Hii ni 50/50 ,BP Wanajua kwanini wameendelea kuitunishia serikali misuli ,,,tuone mgogoro huu utaishia wapi
 
watanzania tusikubali kudanganyika namna hii! tunadanganywa kama watoto! "pale unapompa mtoto pipi ili aache kulia"
 
Huu ni Uwenda wazimu.

BP ndiyo kampuni kubwa kuliko zote za mafuta hapa Tanzania. Tunapeleka messeji gani kwa dunia?

Hivi watanzania wanafikiri kuwa serikali itaweza kusambaza mafuta kwa ufanisi kama sekta binafsi? Pamoja na matatizo yote yanayolisibu taifa letu leo hii, ni sekta ya mafuta peke yake iliyoweza kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. Mpaka kule kijijini kabisa Kigoma, wananchi wanapata mafuta ya kuendesha pikipiki zao. Unafikiri serikali iliyoshindwa kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa 14% ya watanzania itaweza kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa 100% ya watanzania?

 
Halisi,
Commercially this is too sensitive! Can you enlight us on the source p'se!?
 
this is just stupid... watu wanatufanya kama wote majuha

mantiki ya huo uamuzi wa kipuuzi ni kutaka kutuaminisha kwamba serikali ipo au?

serikali ituambie ni kwa nini BP waligoma kuuza mafuta wakati serikali ina 50% shares na wakati huo huo mafuta yakaendelea kuuzwa kwa wenye migodi na taasisi zingine ambazo wao wanaziita nyeti
 
EWURA hawana meno ya kung'ata BP.

Huu ni mchezo wa kuigiza tu.
 
KWA NINI HII STOPU NI KWA BP PEKE YAKE NA SI KWA KAMPUNI ZA MAFUTA ZA MIARRABU KOKO ZENYE HISA ZA CCM??????

EWURA kweli sasa tumekomaaa ujinga!!! Inamaaana kampuni hii ya Muingereza pekee ndiyo iliyotukosea kwenye kutufichia mafuta au ni pamoja na hizo za Mi-arabu koko mlizowapa tu eti vijibarua vya onyo??????????

Na hiki kitendo cha kuzuia BP isifanye biashara ya rejareja bali iuze stock yake kwa bei ya Jumla tu tena kwa Walanguaji hawa hawa Mi-Arabu Koko ndio kusema BP kapewa adhabu gani hapo sasa na hili lote ni KWA FAIDA YA NANI nchini????????

Haruna Masebu, Ngeleja na Jairo; bure kabisa!!!!!!!!!!!!!!! Acheni hizi janja za nyani kula mahindi mabichi. Wala hatujaridhika kitu na hizi danganya toto!!!!!!!!

Kibodya wa BP hebu tuambie ukweli
isije ikawa ni kwamba BP iliwahi kuinyima CCM fedha za KAMPENI huko nyuma ndio sasa wakawa wamejipatia kijinafasi ya kujilipia kisasasi kwenu nyinyi peke yenu na wala si kwa makampuni ya Waarabu Koko ambao siku zote huchangishwa fedha na Iddi Azza Zungu kwa ajili ya CCM.

Enyi CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi sasa ni muda muafaka kuingilia kati sakata hili la mafuta nchini; kama mnavyojua CCM katika kila tukio ni sharti wajitengenezeee - mchezo MCHAFU ndio huu hapa umeanza kwa STOPU YA 'BP' washindani wake wenye hisa za CCM wakipewa kipindi cha siku 90 kujitengenezea fedha bila kuwepo JABALI WA MAFUTA nchini BP.

Tafakarini sana hili na tuchukue hatua mara moja!!!!!!!!!!!!

HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:

a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja

b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.

d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.

e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.

f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).


USIMAMIZI WA MAFUTA

a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.
b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.
 
Kiongozi Halisi:

Huu uamuzi umejaa 'utata'!

Unaweza 'kusitisha leseni'; halafu ukaruhusu kuendelea 'kuuza mafuta ya ndege'; na '..kwa vituo vya rejareja vyenye nembo ya BP'?
Vituo vyenye nembo ya BP si vya BP Tanzania Ltd wanatumia tu nembo. Wanatakiwa kununua mafuta kwengine
 
Danganya toto,
Hiyo ni ya Vigogo, kuuza kwa wengine na kuuza mwenyewe kuna utofauti gani.
Kuuza kwa jumla ndio dili na sio kwa rejareja.
Kwani kuuza kwa Jumla hakuna Loss yoyote, while rejareja kuna Temperature loss kibao.
wehuu sana hawa,
wajinga ndio wataelewa hii kitu, serikali lazima iwe makini na EWURA, inapotosha wananchi na kufaidika kwa Rushwa
 
Naona wamevuka hatua ya kufanya maamuzi magumu naona sasa tungoje tuone utekelezaji legelege
 
hii danganya toto tangu lini ukachukua leseni hapohapo unasema wenye nembo ya Bp wanunue mafuta kutoka makampuni mengine wauze na Bp iuze mafuta yake kwa makampuni mengine huu ni uongo nani anaelewa haya ni mafuta yametoka kampuni fulani ni si Bp? haina mwelekeo huku nikutufanaya watanzania wajinga kuwa wamefanya maamzi lakini ukweli ni uongo
 
uamuzi wa kisiasa huu kama ni kufungiwa afungiwe kila kitu ili apate hasara ya 100% na iwe fundisho na kwa wengine pia
 
Back
Top Bottom