syndicate
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 204
- 315
Niendee moja kwa moja kwenye mada husika!
Mkoa wa Tabora hivi sasa ninapoandika uzi huu, uko kwenye taharuki kubwa ya kukosa mafuta!
Hali ni mbaya hapa mjini, petro station moja tu mji mzima inatoa huduma ya mafuta!
Hakuna kiongozi yoyote wa chama (CCM) au serikali ambaye ametoa ufafanuzi wowote!
Mkoa huu wa kishu'shu'shu na KI'CCM hali ni tete..! Mkoa umebaki mtupu hakuna mtetezi!
Nikumbushe kuwa jumatano ijayo ya mwanzo wa mwezi kwa fununu zilizopo EWURA wanatangaza bei mpya za mafuta, kitu ambacho kinatarajiwa, ni mafuta kupaa zaidi bei.
Nikumbushe pia mwezi mmoja uliopita ilitokea taharuki kama hii ya sasa, na kuonekana baadhi ya wafanyabiashara wakificha mafuta na baada ya wiki moja na nusu mafuta yakapaa kwa bei ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa kizazi hiki cha miaka 30 iliyopita!
SHIDA YA MAJI
Maji pia yamekuwa shida, zaidi ya wiki sasa maji hayapatikani...!
Hali ni mbaya tumefika pabaya!!
=============
EWURA YAKIFUNGIA KITUO CHA GBP TABORA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imechukua hatua hiyo kwa kutouza mafuta kwa siku 3 kama kanuni inavyoelekeza wakati kikiwa na akiba ya mafuta kwenye ghala.
Hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai baadhi ya Wafanyabiashara wanaficha Petroli na Dizeli Mkoani hapo wakati wakisubiri #EWURA itangaze bei mpya ambayo kama itakuwa kubwa itawapa faida kubwa.
Taarifa ya EWURA Tabora imeeleza baada ya kukifungia kituo hicho, hatua inayofuata ni kutakiwa kujieleza sababu za kutouza mafuta, baada ya hapo mamlaka itatoa maamuzi kama kukifungulia au kutoa adhabu.