BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

Kama ni kweli serikali ina hisa BP Tanzania basi hili picha bado reeeeeeeeeefu sana.

1. BP inaigomea serikali ambayo ni mwanahisa.
2. Serikali inaamuru BP kuuza mafuta
3. Serikali inamshitaki M/kiti wa bodi ambaye atatetewa kwa fedha za BP ambako wajumbe wa bodi toka serikalini watajenga utetezi wa M/kiti wao.

Wallah Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo woteee!

Mkuu...good thinking, you have thought at least 5 steps ahead of dem...Big up mzawa
 
Kiongozi Halisi:

Huu uamuzi umejaa "utata"!

Unaweza "kusitisha leseni" halafu ukaruhusu kuendelea "kuuza mafuta ya ndege" na "..kwa vituo vya rejareja vyenye nembo ya BP"?

Ndg ninaungana na wewe asilimia moja kwani unapompa mtuhumiwa adhabu lazima kazi zote zisimame zote na siyo vinginevyo alafu tena ingekuwa ni bora hawa jamaa wafutiwe leseni moja kwa moja na wazawa kupewa hivyo vituo when do u think indigenous wanna rule and enjoy their economy by rising their flag up n thanking CCM that now we are controlling our economy by 90%?
 
HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:

a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja

b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.

d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.

e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.

f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).


USIMAMIZI WA MAFUTA

a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.

b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.
Habari ya Shimbo na trilion tatu AACT SA imeishia wapi mbona serikali haijachukua hatua????????????
 
Yale makampuni manne yaliopewa 24hrs, wangejua kabla adhabu ambayo wangepewa ndio hii,, wangeendelea na mgomo. Wanajuta kwanini waliogopa wakatii amri.

Hivi unafikiri kweli waliogopa adhabu ya serikali. Jamaa waliogopa nguvu ya umma. Walijuwa kuwa wangendelea na mgomo kwa zaidi ya siku mmoja vituo vyote vingewaka moto.
 
I am not so sure if the this decision is meaningfully effective since most of oil businessmen are great sponsors of the ruling CCM.
<br />
<br />
Haya ndo madhara ya kuzeeka vibaya....KUROPOKA KITU USICHOKUA NA USHAHIDI NACHO....UNATAKA TUSEME NI KIASI GANI CHANDIMU WALIPOKEA KUTOKA WIZI WA MAFUTA UNAOFANYIKA TUNDUMA?? WALISEMA HAKUNA HATUA HATUA ZIMECHUKULIWA SASA MNABADILI STORI... NYAMBAFUUUU
 
utangulizi
itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 22 juni 2011 serikali, kupitia kwa waziri wa fedha na uchumi wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12, ilitoa maagizo kwa ewura kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta kwa utaja maeneo mengi kama ifuatavyo (tunanukuu):
A) ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na dola ya marekani (yaani exchange rate);
b) kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
c) kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na taasisi hizo;
d) kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani financing charges); na
e) upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
(mwisho wa kunukuu).
Aidha, mnamo tarehe 4 julai 2011, ewura ilianza mchakato kwa kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kupunguza bei za mafuta. Pia ewura iliandaa dokezo (discussuon paper) lililokuwa na vipengele mbalimbali ambavyo vitapunguzwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwemo wauzaji wa mafuta hapa nchini.
Wadau mbalimbali walichangia dokezo hilo na kuwasilisha ewura kwa maandishi na hatimaye mchakato wa utengenezaji wa kanuni mpya ambayo imepunguza bei za mafuta ulihitimishwa kwa kuitisha mkutano wa taftishi uliofanyika julai 22, 2011 katika ukumbi wa karimjee


ushirikishaji wadau
mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 04 julai 2011 na kukamilika tarehe 26 julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huu ungechukua siku 81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, mamlaka ililazimika kuufupisha hadi siku 23. Wadau walioshirikishwa katika taftishi hiyo ni pamoja na kampuni za mafuta, baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na ewura (consumer consultative council), baraza la ushauri la serikali, taasisi za umma kama vile tra, tbs, wma, tpdc, tpa, sumatra, na tiper.
Matokeo baada maoni mbalimbali ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na timu ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo wizara ya nishati na madini, wizara ya fedha na uchumi, shirika la maendeleo ya mfuta tanzania (tpdc), ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na ewura na katika mfumo mzima wa kufanikisha utayarishaji wa kanuni hii mpya, wadau wote walifahamishwa katika mchakato huu kuwa bei mpya zitatolewa tarehe 1 agosti 2011.

Ya kutangaz bei mpya

baada ya kutangaza bei mpya zilizoanza agosti 3, 2011 kampuni zilianza mgomo baridi wa kutouza mafuta kutoka kwenye magahala yake. Hata hivyo mgomo huo haukufahamika sana kutokana na kutokea wakati kukiwa na siku za mapumziko ya muda mrefu yaani taari 6 hadi tarehe 8 agosti 2011.


Baada ya kugundua hilo, bodi ya wakurugenzi ya ewura ilikaa agosti 9, 2011 na kutoa agizo la kisheria (order) kwa kampuni nne ambazo zilionekana ndizo kinara wa mgomo husika. Kampuni hizo ni bp (t) ltd, oilcom (t) ltd, camel oit (t) ltd na engen petroleum (t) ltd.

Agizo hilo la kisheria lilizitaka kampuni hizotajwa kutekeleza yafuatayo;
a) waanze kuuza mafuta mara moja baada ya kupata agizo la kisheria kutoka ewura
b) waache mara moja vitendo vyovyote vinavyozuia uuzwaji wa mafuta
c) watoe maelezo kwa maandishi katika muda wa saa 24 kwa kuvunja sheria ya petroli ya mwaka 2008 kifungu 24 (1).
Baada ya agizo kutolewa tarehe 9 agosti 2011, kesho yake kampuni zote zilianza kuuza mafuta kwenye maghala ambapo siku ya kwanza tarehe 10, agosti 2011 ziliuzwa lita 8,535,700 kutoka kwenye maghala .
Hata hivyo, pamoja na kuuzwa kwa mafuta kwa wingi, bado bp (t) ltd alionekana kukahidi amri halali ya ewura kwa kuzingatia sheria ya petroli ya mwaka 2008, kifungu 24 (1) kwa kutouzaa mafuta kwenye vituo vyake vyote.

Hatua zinazochukuliwa

baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, bodi ya wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:
A) kuziandikia onyo kali kampuni za oilcom (t) ltd, camel oit (t) ltd na engen petroleum (t) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na sheria za tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja
b) kusitisha leseni ya biashara kwa bp (t) ltd kwa miezi mitatu kuanzia leo kuuza mafuta ya petroli, dizeli na taa.

C) bp (t) ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba ewura haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.
D) pia bp (t) ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa ewura ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.
E) hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (petrol stations) vya vyenye nembo ya bp vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa bp.
F) pia bodi ya wakurugenzi imeeagiza mtendaji mkuu na mwenyekiti wa bp (t) ltd kufikishwa mahakamani kwa kupitia kwa mkurugenzi wa mashitaka jinai (dpp).


Usimamizi wa mafuta

a) kuanzia sasa ewura itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.
B) pia ewura itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

Imesainiwa
haruna masebu
mkurugenzi mkuu

mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati (ewura)


utaifungiaje kampuni kuuza mmafuta alafu unasema anaruhusiwa kuuza mafuta kwenye vituo vyake kwa kutumia mafuta ya wengi embu we pumbafu ewura acheni ujinga na usanii wa kitoto haa mtoto anajua mchezo mchafu mnaotaka kujifanya muonekane mmejivua gamba shame on you funga vituo vyote akuna kuuza easy

shame on you yaani mnakataa ukahaba lakini mnaruhusu ukahaba ikiwa wakikata leseni nakulipa kod i shame on you again
 
Richmond-downs-symbion-wakati kesi iko mahakamani!!!!!!!! siasa za bongo,unanyang'anya leseni au unawafungia kwa miezi mitatu???wakati wao wako mahakamani toka wiki iliyopita??uzoefu unaonyesha serikali ni bingwa wa kushindwa kesi mifano ni mingi lakini katika hili la mtanange wa serikali na hawa wafanya biashara wa mafuta itashindwa.sanasana imejikosha kwa wananchi japo kwa muda tu.
 
Tujiulize,kwa nini BP ambayo ndo yenye share na gvment imeendelee kugoma??? Nadhani kuna jambo apo! Ata ivo adhabu yenyewe naiona ni legelege tu...!
 
Mimi mbona sielewi kabisa. Hii ni adhabu kweli?? Unamzuia mtu kuuza mafuta afu unamwambia aendelee kuyauza kwa jumla yasiharibike. Who cares kama yataharibika or not. Mimi nadhani tuwe na chama cha walaji ili makampuni kama BP yawe yanaadhibiwa na walaji Consumers). TUNATAKIWA KUGOMEA KUNUNUA MAFUTA TOKA VITUO VYA BP. Watafunga virago warudi kwao UK. Watanzania tumezidi upole ndio maana tunasubili sirikali ituamulie kila kitu. Hawa tungewaadhibu wenyewe tuone kama na sisi wangetuonga.
 
napata taabu kidogo ya mantiki...wanasema bp haruhusiwi kuuza mafuta kwa miezi mitatu,wakati huohuo anaruhusiwa kuuza mafuta aliyonayo kwa bei ya jumla kwa kampuni nyingine......maana yake anaweza kuuza kupitia kampuni nyingine...! pili inasemekana serikali inahisa 50% BP je serikali imejigomea na kujiadhibu yenyewe? hii ni usanii tu wa kisiasa.
 
Hii ni danganya toto, yaani serikali inaleta siasa mpaka kwenye masuala ya msingi kama haya, wasitupumbaze! wakubali tu kwamba wao ni legelege ( not serious ) na kwamba hao jamaa wa BP wamewapiga bao na mimi nilijua tu toka mwanzo kwamba hawawezi kufurukuta kugusa maslahi ya mabosi wao. BP=10, Serilkali=0
 
ewura mbona mnatuchnaganya hivo, mmesimisha leseni halafu mnaruhusu kwa ajili ya ndege na vituo vya Bp. sasa hapo mmesimasha leseni ya nani wakati mtu huyohuyo anaendelea kuuza mafuta. au huyu mtu ana leseni mbili ya mafuta ya magari na ya mafuta ya ndege...........ebu kuweni wawazi ili tuwaelewe
 
Mnajua malaya sio lazima awe anauza unyumba wake la hasha hata ukiwa sehemu ya kazi ukajifanya sitaki nataka akuna tofauti na huyu anaejiuza anachofanya ukimtongoza anakukatalia kwanza na badae anakukubalia sina la kusema zaidi
ewura pumbafuuuuuuu kkabisa nasema hii miradi ya ccm ya kupitishia hela za chama zinatutesa sana sana ewura ya anini sasa kama inaweza kufunga na kufungulia ...
Shetan wakubwa kuanzia mkuurgenzi wake na wakurugenzi wote
 
Bado haijakaa viruzi,inawzekana vipi kusimamisha kampuni ambayo ina share na serikali na serikali isiathirike kama mwana hisa?

Kama usimamishwaji ni wa dhati ningeamini hawa jamaa wangezuiiwa kufanya biashara ya aina yeyote kwa mda uliotajwa

Nasema bado!
 
Yaani watu hawaoni mchezo unaopangwa? Hizo asilimia 50 ya hisa za serikali ni jaribu kubwa.
 
nimesikia serikali ina share ya 50% katika BP (T) ltd,sasa kama wamegoma kuuza.imekuwaje serikali wenye share wameshindwa ku-solve hii mambo?au serikali nayo imeshindwa kuwasaidia wananchi wake?au ni usanii tu unaochezwa hapa
 
CHANGA LA MACHO HILO BP WANAMPANGO WAKUONDOKA BONGO


BP Ceases Its Country Operations

It is end of an era for BP Tanzania, a major oil marketing company that has operated in the country for about a century.

BP Africa's Chief Executive Sipho Maseko announced on Tuesday that BP was quitting the Tanzanian market following a strategy review that would see it concentrate all its efforts in strategic countries such as Angola, Mozambique, South Africa, Algeria, Egypt and Libya. Except South Africa, the rest are oil and/or gas producing countries. BP has also ceased operations in Namibia, Malawi, Zambia and Botswana.

"I would like to stress that BP is and will stay committed to Africa," BP Africa's Chief Executive Sipho Maseko said in a statement released on Tuesday. "We have significant operations in Angola, Mozambique and South Africa and in Algeria, Egypt and Libya. We will continue to grow and invest in those markets, especially in the value chain infrastructure," he had added.

The decision is likely to affect Tanzania's petroleum marketing industry as the company has often played a significant and pioneering role. But to what extent that effect will play itself out cannot now be established now. Until recently, BP Tanzania has had a 35 per cent market share in both the retail and service stations and about 70 per cent in aviation. In Zanzibar it has been controlling the aviation fuel market by about 100 per cent.
The director general of the Energy and Water Utilities Regulatory Authority Mr Haruna Masebu declined to comment on how BP's decision would affect the downstream petroleum industry in Tanzania. He said Ewura had not received any notification on BP's decision and until that notification was received it would be premature to say anything. "We will ultimately comment on BP's decision but we have not yet received any official communications on the matter.

Talking about it now would be just speculating," he told The Citizen in an interview yesterday in Dar es Salaam. He however observed that since the company was a joint venture between BP group and the Tanzanian government, their departure would not translate into complete shut down in the country.

Mr Masebu said that BP has already notified the Tanzanian government and other governments included in the pullout but when contacted the Tanzanian government officials said they were still unaware of the issue. Mr Prosper Victus, Head of Petroleum and Gas Section at the ministry of Energy and Minerals, said he had not seen any official documents concerning the issue.
"I am not aware of the issue. The ministry might have been informed already but the information is not yet on our desk," he told The Citizen by phone yesterday. The ministry's acting Permanent Secretary, Mr Invocavit Swai, was in a meeting when reached yesterday and he could not comment on the issue.

The minister of Energy and Minerals Mr William Ngeleja could not be reached as his phone went unanswered and could not reply to a text message sent to him from The Citizen. However, the deputy minister for Energy and Minerals Adam Malima was quoted by a section of the online media saying he was also not aware of the move.

BP Tanzania is among some 40 oil marketing and trading companies in Tanzania with Addax, Mobil, Total, Oryx, Engen, GAPCO, GAPOIL and Oilcom Tanzania Limited being the market leaders.

In the seven southern African countries of Namibia, Botswana, Mozambique, South Africa, Tanzania, Malawi and Zambia, BP's downstream infrastructure includes some 29 depots and terminals, and more than 800 retail sites. Apart from fuel and lubricants, BP Tanzania has also been selling liquefied petroleum gas (LPG) for over forty years. It used to monopolise the market until the entry of Agip after the construction of a refinery, Tipper, in 1964.

To date BP and Agip Tanzania Limited (which has since been sold to ADDAX and operates as Oryx Tanzania Limited) are the leading players. BP Tanzania has also an organisation that deals in solar energy under a project that covers upcountry regions. BP has also had a large stake in the transit petroleum business through the port of Dar es Salaam to Uganda, Rwanda, Burundi, DRC Congo, Zambia and Malawi.

BP Tanzania traces its roots back in 1900 when Smith MacKenzie started importing kerosene to the island of Zanzibar as Shell agent A bulk tank and kerosene-can filling plant was established in 1901, and for a while Zanzibar supplied oil to much of the east coast of Africa and the Indian Ocean islands. Shell expanded to the Mainland and with the formation of the Consolidated Petroleum Corporation in the late 1920s, BP acquired an interest in the company.

In 1970 the Government of Tanzania bought a 50 per cent interest in what was then Shell and BP Tanzania Limited. In March 1982, BP bought out Shell's interests and the company became BP Tanzania Limited. Ends
 
Back
Top Bottom