BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Aug 12, 2011.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  HATUA ZINAZOCHUKULIWA

  Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:

  a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja

  b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

  c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.

  d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.

  e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.

  f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).


  USIMAMIZI WA MAFUTA

  a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.

  b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Funika kombe mwanaharamu apite
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  UTANGULIZI
  Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha na Uchumi wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, ilitoa maagizo kwa EWURA kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta kwa utaja maeneo mengi kama ifuatavyo (tunanukuu):
  a) Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);
  b) Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
  c) kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
  d) kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financing Charges); na
  e) Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
  (mwisho wa kunukuu).
  Aidha, mnamo tarehe 4 Julai 2011, EWURA ilianza mchakato kwa kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kupunguza bei za mafuta. Pia EWURA iliandaa dokezo (discussuon paper) lililokuwa na vipengele mbalimbali ambavyo vitapunguzwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwemo wauzaji wa mafuta hapa nchini.
  Wadau mbalimbali walichangia dokezo hilo na kuwasilisha EWURA kwa maandishi na hatimaye mchakato wa utengenezaji wa Kanuni mpya ambayo imepunguza bei za mafuta ulihitimishwa kwa kuitisha Mkutano wa TAFTISHI uliofanyika Julai 22, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee


  USHIRIKISHAJI WADAU
  Mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 04 Julai 2011 na kukamilika tarehe 26 Julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huu ungechukua siku 81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, Mamlaka ililazimika kuufupisha hadi siku 23. Wadau walioshirikishwa katika taftishi hiyo ni pamoja na kampuni za mafuta, Baraza la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (Consumer Consultative Council), Baraza la Ushauri la Serikali, Taasisi za Umma kama vile TRA, TBS, WMA, TPDC, TPA, SUMATRA, na TIPER.
  MATOKEO BAADA Maoni mbalimbali ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na timu ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Uchumi, Shirika la Maendeleo ya Mfuta Tanzania (TPDC), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na EWURA na katika mfumo mzima wa kufanikisha utayarishaji wa kanuni hii mpya, wadau wote walifahamishwa katika mchakato huu kuwa bei mpya zitatolewa tarehe 1 Agosti 2011.

  YA KUTANGAZ BEI MPYA

  Baada ya kutangaza bei mpya zilizoanza Agosti 3, 2011 kampuni zilianza mgomo baridi wa kutouza mafuta kutoka kwenye magahala yake. Hata hivyo mgomo huo haukufahamika sana kutokana na kutokea wakati kukiwa na siku za mapumziko ya muda mrefu yaani taari 6 hadi tarehe 8 Agosti 2011.


  Baada ya kugundua hilo, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilikaa Agosti 9, 2011 na kutoa AGIZO LA KISHERIA (ORDER) kwa kampuni nne ambazo zilionekana ndizo kinara wa mgomo husika. Kampuni hizo ni BP (T) Ltd, Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd.

  Agizo hilo la kisheria lilizitaka kampuni hizotajwa kutekeleza yafuatayo;
  a) Waanze kuuza mafuta mara moja baada ya kupata agizo la kisheria kutoka EWURA
  b) Waache mara moja vitendo vyovyote vinavyozuia uuzwaji wa mafuta
  c) Watoe maelezo kwa maandishi katika muda wa saa 24 kwa kuvunja Sheria ya Petroli ya mwaka 2008 kifungu 24 (1).
  Baada ya agizo kutolewa tarehe 9 Agosti 2011, kesho yake kampuni zote zilianza kuuza mafuta kwenye maghala ambapo siku ya kwanza tarehe 10, Agosti 2011 ziliuzwa lita 8,535,700 kutoka kwenye maghala .
  Hata hivyo, pamoja na kuuzwa kwa mafuta kwa wingi, bado BP (T) Ltd alionekana kukahidi amri halali ya EWURA kwa kuzingatia Sheria ya Petroli ya mwaka 2008, kifungu 24 (1) kwa kutouzaa mafuta kwenye vituo vyake vyote.

  HATUA ZINAZOCHUKULIWA

  Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:
  a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja
  b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

  c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.
  d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.
  e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.
  f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).


  USIMAMIZI WA MAFUTA

  a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.
  b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

  IMESAINIWA
  Haruna Masebu
  MKURUGENZI MKUU

  MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI (EWURA)
   
 4. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hongera Govt!
  Hatua kama hizi ziwaendee pia wale wafanya fujo wa Arusha!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  nahisi tumepigwa changa la macho, kwanini vituo vya BP viendelee kuuza mafuta?
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,743
  Trophy Points: 280
  EWURA inatwanga maji kwenye kinu, infact inaadhibu kivuli. mbona BP tayari imeuzwa kwa Puma Energy (subsidiary of Trafigura)!!!
   
 7. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nini maana ya kusimamisha? Nahisi ban inaninyemelea. Ngoja nikae kimya kwanza niangalie upepo unaelekea wapi.
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kiongozi Halisi:

  Huu uamuzi umejaa "utata"!

  Unaweza "kusitisha leseni" halafu ukaruhusu kuendelea "kuuza mafuta ya ndege" na "..kwa vituo vya rejareja vyenye nembo ya BP"?
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  danganya toto
  Akawaeleze huu upuuzi watoto wa chekechea
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Good but not enough
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  nimekuwekea picha click hapa
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Damu yako inanuka siasa kila mahali.
   
 13. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I am not so sure if the this decision is meaningfully effective since most of oil businessmen are great sponsors of the ruling CCM.
   
 14. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kama ni kweli serikali ina hisa BP Tanzania basi hili picha bado reeeeeeeeeefu sana.

  1. BP inaigomea serikali ambayo ni mwanahisa.
  2. Serikali inaamuru BP kuuza mafuta
  3. Serikali inamshitaki M/kiti wa bodi ambaye atatetewa kwa fedha za BP ambako wajumbe wa bodi toka serikalini watajenga utetezi wa M/kiti wao.

  Wallah Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo woteee!
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Carol my LV wangu ni PM nikufahamishe maana yake pia tunaweza kuandaa semina elekezi.
   
 16. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,143
  Likes Received: 1,711
  Trophy Points: 280
  mwanzo mzuri , ila kwenye kumshtaki huyo mkurugenzi wa BP ,serikali itashinda kweli au ni kupotezeana muda tu ?
   
 17. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  RICHMOND KUWA DOWANS NA KUUZWA SYMBION POWER. Kweli nyoka hawezi kufanana na chura.
   
 18. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona hujatupa source. Anyway ni hatua nzuri na serikali inpaswa kuendelea kuonesha makucha yake kwa wale wengine wote wenye viburi.
   
 19. F

  FUSO JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  hatudanganyiki n'gooo!!!!....
   
 20. M

  Mutu JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  habari inachanganya ...............yaani unasema nguruwe haramu asiuzwe reja reja uzwe kwa jumla ..........hapa pana namna ...
   
Loading...