Kiongozi Halisi:

Huu uamuzi umejaa "utata"!

Unaweza "kusitisha leseni" halafu ukaruhusu kuendelea "kuuza mafuta ya ndege" na "..kwa vituo vya rejareja vyenye nembo ya BP"?
HATUA ZINAZOCHUKULIWA
Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:
a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja
b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.
c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.
d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.
e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.
f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).
USIMAMIZI WA MAFUTA
a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.
b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.
Wafanya fujo gani hao wa arusha??? Umesahau serikali na polisi wake waliua watu huko arusha??? Acha mambo ya ajabu siku tukibaini upo hapa arusha basi utatuonyesha hao wafanya fujo ni kina nani... Mulize jk kwanini siku hizi anakuja arusha kimya kimya..Hongera Govt!
Hatua kama hizi ziwaendee pia wale wafanya fujo wa Arusha!
Mchezo wa kuigiza kama ule wa orijino komedi kama jinsi ambavyo joti anakuwa mwanamke na hapohapo anakuwa mwanaume...hahaaa ccm ina shea 50% za bpHang on... Lets get this straight. BP anaweza kuuza mafuta yake, say kwa Oilcom, then outlets za BP zinaweza kununua mafuta hayo hayo, toka kwa Oilcom na kuyauza. Labda kama sijaelewa, kwa hiyo BP kafungiwa nini sasa???
nahisi tumepigwa changa la macho, kwanini vituo vya BP viendelee kuuza mafuta?
Kiongozi Halisi:
Huu uamuzi umejaa "utata"!
Unaweza "kusitisha leseni" halafu ukaruhusu kuendelea "kuuza mafuta ya ndege" na "..kwa vituo vya rejareja vyenye nembo ya BP"?