Ni hatari sana bei ya mafuta ya taa ikiwa chini sana kuliko bei ya petroli na dizeli

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Nilikuwa nafuatilia kwa karibu bei za mafuta ya petroli, dizeli, na mafuta ya taa zilizotangazwa na EWURA mwezi huu.
Baada ya kuchunguza kwa kina, nimegundua bei ya mafuta ya taa imekuwa chini sana ikilinganishwa na ile ya mafuta ya petroli na dizeli.
Hali hii inanitia wasiwasi sana, kwani inaweza kuvutia uchakachuaji wa mafuta. Watu huenda wakajaribu kuchanganya mafuta ya taa na dizeli ili waweze kuyauza kama dizeli na kupata faida zaidi.

1691224122736.png

Matumizi ya mafuta yasiyo sahihi yanaweza kusababisha uharibifu wa injini za magari na vifaa vingine vya usafirishaji.

Ni muhimu sana kwa EWURA na taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa bei za mafuta zinawekwa kwa uwiano unaofaa na gharama za uzalishaji na usambazaji.

Vilevile, elimu inahitajika kuelimisha umma kuhusu athari za kuchanganya mafuta na umuhimu wa kutumia mafuta sahihi kulingana na aina za injini. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kupunguza hatari za uchakachuaji wa mafuta na kuhakikisha usalama.

REJEA:
EWURA yaunga mkono bei ya mafuta ya taa kuwa kama dizeli, petrol

na Janet Josiah

MAMLAKA ya Udhibiti wa Matumizi ya Nishati na Maji (EWURA), imeunga mkono, mapendekezo ya baadhi ya wadau kutaka kupandishwa kodi mafuta ya taa kuwa sawa na ya diseli na petroli. Akizungumza na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Haruna Masebu, alisema endapo kodi hizo zitakuwa sawa na zingine hatua hiyo itakuwa suluhisho kuondoa tatizo la uchachushaji mafuta.

Mapendekezo ya EWURA na wadau wengine, yamekuja siku chache baada ya tukio la magari matano ya Rais Jakaya Kikwete kujazwa mafuta machafu na kugoma kuwaka wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro.

Masebu alisema ingawa bajeti ya mwaka wa fedha ya 2010/2011, haikuzungumzia suala la mafuta ya taa kupandishwa kodi kutokana na nishati hiyo kutumiwa na watu wa hali ya chini, alisema tatizo hilo halitaweza kuisha kwa kuwa ndilo linalowapa faida wafanyabishara wa mafuta.

Alisema wafanyabishara wamekuwa wakipata faida kubwa katika mafuta wanayoyauza baada ya kuyachakachua kutokana na mafuta ya taa kutozwa kodi ya shilingi 53 kwa lita na dizeli na petroli kutozwa shilingi 490 kwa lita pindi wanapoyaingiza.

Masebu alisema baada ya kufanya zoezi la kuyachakachua na kuanza kuyauza hupata faida ya shilingi 450, hali ambayo alisema endapo serikali haitachukua hatua za kuyapandishia kodi, hali hiyo itaendelea kama ilivyo. Alisema wao kama EWURA hawana uwezo wa kupandisha nishati hiyo kodi bali uwezo huo upo katika Wizara ya Fedha na Uchumi.

Masebu alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na kwamba haliwezi kuisha mara moja kama nishati hiyo haitapandishiwa kodi, EWURA imejipanga kutumia njia za aina mbili ili kupunguza tatizo hilo mojawapo ikiwamo ya kuyawekea mafuta ya taa rangi ambayo itayatofautisha na mafuta ya dizeli na petroli hata kama yatachachuliwa yatagungulika mara moja.

Alisema njia nyingine ambayo EWURA itatumia kukabiliana na tatizo hilo, tayari imeagiza magari maalum yenye maabara Mobile Laboratory yatayoingia mwezi Agosti, ambayo yatazunguka nchi nzima kukagua na kuwachukulia hatua wafanyabiasha watakaokuwa wamefanya hivyo.

Alipoulizwa endapo nishati hiyo itapanda, haoni kama itawaumiza watu wa hali ya chini, alijibu kwamba kama serikali ikifikia muafaka wa kupadisha kodi, wananchi wa hali ya chini watatafutiwa nishati mbadala ya mafuta ya taa ili kukidhi mahitaji yao kama ilivyo katika nchi nyingine.

Wakati huo huo, Masebu alisema kuwa tayari mamlaka hiyo imeshakamilisha ripoti ya uchunguzi wa kituo cha mafuta cha mjini Moshi ambacho kiliyaweka mafuta machafu kwenye magari matano yaliyokuwa katika msafara wa Rais Kikwete.

Alisema kinachosubiwa sasa ni maelezo ya mmiliki wa kituo hicho ili ripoti hiyo itolewe mbele ya vyombo vya habari kesho kutwa (Ijumaa).

Source EWURA yaunga mkono bei ya mafuta ya taa kuwa kama dizeli, petrol
 
Attachments

  • 1691223962828.png
    1691223962828.png
    49.3 KB · Views: 9
Hapa madalali wameingia na wamekaa...

Tuombe tu uzima, hakuna wa kusikiliza sauti yeyote... you either play the game or forever keep your peace.

Time will tell.
 
Nilikuwa nafuatilia kwa karibu bei za mafuta ya petroli, dizeli, na mafuta ya taa zilizotangazwa na EWURA mwezi huu.
Baada ya kuchunguza kwa kina, nimegundua bei ya mafuta ya taa imekuwa chini sana ikilinganishwa na ile ya mafuta ya petroli na dizeli.
Hali hii inanitia wasiwasi sana, kwani inaweza kuvutia uchakachuaji wa mafuta. Watu huenda wakajaribu kuchanganya mafuta ya taa na dizeli ili waweze kuyauza kama dizeli na kupata faida zaidi.

View attachment 2708995

Kupandisha Bei ya mafuta ya taa kama suluhu ya kuzuia uchakachuzi Si sahihi!!

Mamlaka Inatakiwa ihakikishe inadhibiti uhuni wa wachakachuzi,

Kufuta lesseni ya Kampuni ya kituo Cha mafuta kilichothibitika kuchakachua, au kuchukua hatua Kali dhidi ya wachakachuzi ndio njia sahihi.

Mamlaka zitoke kuwajibika,zikishindwa zifutwe!!
 
Wewe unangalia gari lako bali hungalii maisha ya ndugu zetu vijijini wanaotumia mafuta ya taa kwa wingi, huu ni ubinafsi wa fikira bila kuhisi kuna wengine wanapata shida sana kama bei ikiwa juu
 
Nilikuwa nafuatilia kwa karibu bei za mafuta ya petroli, dizeli, na mafuta ya taa zilizotangazwa na EWURA mwezi huu.
Baada ya kuchunguza kwa kina, nimegundua bei ya mafuta ya taa imekuwa chini sana ikilinganishwa na ile ya mafuta ya petroli na dizeli.
Hali hii inanitia wasiwasi sana, kwani inaweza kuvutia uchakachuaji wa mafuta. Watu huenda wakajaribu kuchanganya mafuta ya taa na dizeli ili waweze kuyauza kama dizeli na kupata faida zaidi.

View attachment 2708995

Matumizi ya mafuta yasiyo sahihi yanaweza kusababisha uharibifu wa injini za magari na vifaa vingine vya usafirishaji.

Ni muhimu sana kwa EWURA na taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa bei za mafuta zinawekwa kwa uwiano unaofaa na gharama za uzalishaji na usambazaji.

Vilevile, elimu inahitajika kuelimisha umma kuhusu athari za kuchanganya mafuta na umuhimu wa kutumia mafuta sahihi kulingana na aina za injini. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kupunguza hatari za uchakachuaji wa mafuta na kuhakikisha usalama.

REJEA:
EWURA yaunga mkono bei ya mafuta ya taa kuwa kama dizeli, petrol

na Janet Josiah

MAMLAKA ya Udhibiti wa Matumizi ya Nishati na Maji (EWURA), imeunga mkono, mapendekezo ya baadhi ya wadau kutaka kupandishwa kodi mafuta ya taa kuwa sawa na ya diseli na petroli. Akizungumza na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Haruna Masebu, alisema endapo kodi hizo zitakuwa sawa na zingine hatua hiyo itakuwa suluhisho kuondoa tatizo la uchachushaji mafuta.

Mapendekezo ya EWURA na wadau wengine, yamekuja siku chache baada ya tukio la magari matano ya Rais Jakaya Kikwete kujazwa mafuta machafu na kugoma kuwaka wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro.

Masebu alisema ingawa bajeti ya mwaka wa fedha ya 2010/2011, haikuzungumzia suala la mafuta ya taa kupandishwa kodi kutokana na nishati hiyo kutumiwa na watu wa hali ya chini, alisema tatizo hilo halitaweza kuisha kwa kuwa ndilo linalowapa faida wafanyabishara wa mafuta.

Alisema wafanyabishara wamekuwa wakipata faida kubwa katika mafuta wanayoyauza baada ya kuyachakachua kutokana na mafuta ya taa kutozwa kodi ya shilingi 53 kwa lita na dizeli na petroli kutozwa shilingi 490 kwa lita pindi wanapoyaingiza.

Masebu alisema baada ya kufanya zoezi la kuyachakachua na kuanza kuyauza hupata faida ya shilingi 450, hali ambayo alisema endapo serikali haitachukua hatua za kuyapandishia kodi, hali hiyo itaendelea kama ilivyo. Alisema wao kama EWURA hawana uwezo wa kupandisha nishati hiyo kodi bali uwezo huo upo katika Wizara ya Fedha na Uchumi.

Masebu alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na kwamba haliwezi kuisha mara moja kama nishati hiyo haitapandishiwa kodi, EWURA imejipanga kutumia njia za aina mbili ili kupunguza tatizo hilo mojawapo ikiwamo ya kuyawekea mafuta ya taa rangi ambayo itayatofautisha na mafuta ya dizeli na petroli hata kama yatachachuliwa yatagungulika mara moja.

Alisema njia nyingine ambayo EWURA itatumia kukabiliana na tatizo hilo, tayari imeagiza magari maalum yenye maabara Mobile Laboratory yatayoingia mwezi Agosti, ambayo yatazunguka nchi nzima kukagua na kuwachukulia hatua wafanyabiasha watakaokuwa wamefanya hivyo.

Alipoulizwa endapo nishati hiyo itapanda, haoni kama itawaumiza watu wa hali ya chini, alijibu kwamba kama serikali ikifikia muafaka wa kupadisha kodi, wananchi wa hali ya chini watatafutiwa nishati mbadala ya mafuta ya taa ili kukidhi mahitaji yao kama ilivyo katika nchi nyingine.

Wakati huo huo, Masebu alisema kuwa tayari mamlaka hiyo imeshakamilisha ripoti ya uchunguzi wa kituo cha mafuta cha mjini Moshi ambacho kiliyaweka mafuta machafu kwenye magari matano yaliyokuwa katika msafara wa Rais Kikwete.

Alisema kinachosubiwa sasa ni maelezo ya mmiliki wa kituo hicho ili ripoti hiyo itolewe mbele ya vyombo vya habari kesho kutwa (Ijumaa).

Source EWURA yaunga mkono bei ya mafuta ya taa kuwa kama dizeli, petrol
Hili jambo lilishakuwa na mjadala mrefu sana miaka ya huko nyuma na likafanyiwa kazi.
Hakukuwa na shida.

Sasa nashangaa hawa EWURA wanarudisha kule kule.

Halafu hii ni makusudi kabisa.

Nimeshawashauri, ibeni lakini mtumie akili.
 
Sijui walikua hawaoni hilo tatizo.
 
mtindo huu wa kuchakachua ulikuwa awamu ya 4 gari nyingi sana ziliharibika watu wakaona bora kuweka mafuta PUMA, puma hawana upuuzi huo au TOTAL
 
Basi toa ushauri nini kifanyike
Tusiwe wanoko wanoko maana sie binadamu tuna utashi na tusiishi Kwa kuzuia zuia Kila kitu maana hii ni dalili mamlaka zimeshindwa kusimamia Sheria (mtu akichakachua Sheria Kali ichukue mkondo wake, tatizo wauza mafuta wanaogopwa sana kiasi kwamba badala Sheria itumike kulinda uchakachuaji, anaumizwa mwananchi na kumtajirisha mtoa huduma na serikali)

Kimsingi bei ya mafuta ya taa ni karibu nusu ya bei ya diseli hata hiyo unavyosema ni ndogo Bado ni kubwa sana maana Kuna miaka kulikuwa na uchakachuaji ndo likaja hilo wazo la kupangisha bei ili kulinda uchakachuaji
 
Back
Top Bottom