BoT wajitafakari kabla ya kuwatuhumu Bloomberg

Ukiingiza.pesa zako kwenye kazi sasa inakuja inasoma.negative....very fragile. Leo bei hii ukienda chukua mzigo ukirudi bei imebadilika...Watu wameamua.kubaki na pesa yao..wanadraw na kula taratibu
 
Who is GJ Malisa and what are his credentials??? Mbona kama anarukia fani za watu?
Huyu ni walewale chagadema at work,ameandika meengi lakini tumuulize bei ya dola Leo ni shilingi ngapi?
Je ni hiyo bei ya bloomberg?
Then ndio angeanza kampeni yake humu.
 
Malisa GJ
________
Nimeona taarifa ya BOT ikikanusha kuwa sarafu ya Tanzania haijaporomoka, badala yake ni kwamba kuna watu kwenye financial software ya Bloomberg wameamua kuchezea data kwa makusudi kwa kuweka figure zisizo sahihi ili kupotosha. BOT wanasema kuwa tayari wameshawasiliana na Bloomberg ili kurekebisha makosa hayo.

Utetezi huu wa BOT una kasoro nyingi. Kwanza wanajitetea kuporomoka kwa shilingi dhidi ya Dola, lakini ukweli ni kwamba shilingi imeporomoka dhidi ya sarafu zote za kigeni na sio dola tu. Jana majira kama haya shilingi moja ya Kenya ilikuwa sawa na shilingi 21 za Kitanzania (bei ya kuuza), lakini leo shilingi moja ya Kenya ni sawa na shilingi 24.5.

Yani jana ulihitaji shilingi 21,000/= tu za Kitanzania kupata 1,000/= ya Kenya. Lakini leo ili upate 1,000/= ya Kenya unahitaji 24,500/= za kitanzania. Kwa hiyo shilingi yetu imeporomoka dhidi ya sarafu zote, sio dhidi ya dola tu kama BOT wanavyojaribu kueleza.

Pili nashauri BOT wajielekeze kwenye kiini cha tatizo badala ya kuficha tatizo. Kwanini wanajaribu kuficha? Kwa faida ya nani? Shilingi imeporomoka na hata waliotuma fedha leo ni mashahidi. Kwanini waseme data zimechezewa Bloomberg?
Njia rahisi ya kutatua tatizo ni kwanza kukiri kuwa lipo. Ukikataa tatizo huwezi kamwe kulitatua.

Moja ya sifa ya kuongoza taasisi za fedha ni kuwa mkweli katika kiwango cha juu kabisa, na kufanya mambo kwa nia njema sio kwa nia ya kufurahisha wanasiasa (Honesty and utmost good faith). Moja ya mambo yaliyofanya uchumi wa Uganda kuharibika vibaya na thamani ya sarafu yao kuporomoka sana ni Benki kuu ya nchi hiyo kukubali kutumika kisiasa. Idd Amin alikuwa akimuamuru Gavanor wa benki kuu nchini humo aseme uchumi upo imara hata pale mambo yalipokuwa magumu.

Anyway, kwangu taarifa hii ya kuporomoka kwa sarafu yetu ni jambo nililotegemea kulisikia. Pengine limeshtua watu kwa kuwa imekuwa ghafla sana na kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika historia ya nchi. Ndani ya masaa machache tu dola moja ya kimarekani imepanda kutoka shilingi 2,200/= hadi 2,500/=. Tumepoteza shilingi 300/= kwa kila dola moja ndani ya masaa machache.

Yani kwa mtu aliyetaka kutuma pesa nje ya nchi jana, letz say dola 5000, akachelewa na kutuma leo amepata hasara ya Shilingi milioni moja na nusu. Katika kila dola elfu moja amepata hasara ya laki tatu. Hali hii haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

Zipo sababu kadhaa zinazoweza kuwa zimesababisha mporomoko huu mkubwa kabisa katika historia.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni mfumuko wa bei (Inflation rate). Kwa kaawaida mfumuko wa bei unapokuwa mkubwa, sarafu inapoteza ile nguvu yake ya manunuzi (purchasing power) na matokeo yake inaporomoka dhidi ya sarafu za nje. Hapa nchini mfumuko wa bei umeanza kutishia wanunuzi wa bidhaa mbalimbali. Kwa mfano wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 bei ya sukari ilikuwa shilingi 1,500/= hadi 1,800/= kiwa kilo, lakini leo bei ni kati ya shilingi 2,500/= hadi 3,000/= kwa kilo.

Mfumuko wa bei umekuwa kwa zaidi ya asilimia mia moja kwenye bidhaa ya sukari. Maana yake ni kwamba we are no longer at Moderate inflation, rather tunakaribia kwenye Hyper Inflation from Galloping one. Hali hii inasababisha sarafu yetu kuoporomoka kwa kiasi kikubwa.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuwa na uchumi tegemezi wa knunua zaidi nje kuliko kuuza (import oriented economy). Tunaponunua zaidi nje maaana yake ni kwamba tunahitaji akiba kubwa ya fedha za kigeni. Tunapokuwa na demand kubwa ya fedha za kigeni maana yake pesa za kigeni zinakuwa na thamani kubwa kuliko sarafu yetu (the higher the demand the higher the price), na hivyo sarafu yetu inaporomoka. Na hii inaweza kuwa imecahangia sana kwa sababu ni kweli tunanunua zaidi nje kuliko tunavyouza.

Leo mtu akipata mtaji wa milioni 10, 20 anakimbilia China kwenda kuleta nguo, simu, saa, hereni etc. Thamani tunayouza nje ni ndogo sana kuliko tunayonunua.

Unaponunua zaidi nje unapunguza reserve ya pesa zako za kigeni na hivyo sarafu yako kuporomoka. Lakini unapouza zaidi nje unamaintain reserve ya pesa za kigeni na sarafu yako itapanda kwa sababu wanunuzi wa nje wataitafuta sarafu yako ili waweze kufanya purchase. Kabla BOT hawajabisha waangalie upya thamani tunayouza na kununua nje ya nchi ikoje (Balance of Payments).

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: ni madeni ya serikiali (Government Debt). Serikali inapokopa sana nje inapunguza security ya sarafu yake. Ni sawa na nyumba yako uliyojenga kwa milioni 100, ukitaka mkopo wa haraka bank na wakajua una shida sana wanaweza kuithaminisha hata kwa milioni 70. Na wewe utakubali tu kwa sababu una shida. Mkopoo wowote unaokopa kwa sababu una shida saaana, led to undervalue your capital asset.

Sasa jiulize je Tanzania tumewahi kuwa kwenye shida kubwa saaana kiasi cha kukopa mkopo unaoweza kuwa umepelekea capital asset zetu kuwa undervalued? Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ndugu Zitto Kabwe mwezi September mwaka huu, Taasisi ya fedha ya Credit Suisse ya nchini Uswisi, ilikiri kuikopesha Tanzania dola milioni 500 (karibu shilingi Trilioni 1.2) kwa masharti ya kulipa kwa miaka mitano, kwa riba ya karibu asilimia mia moja.

Mkopo huo ambao Tanzania inadaiwa kukopa kwa siri unatolewa na kundi mabenki (Syndicated loan) kupitia taasisi hiyo ya Credit Suisse uliibuliwa na Ndugu Zitto na Credit Suisse wakakiri kutukopesha, japo serikali ilikataa kutoa majibu ya tuhuma hizo. Kwa hiyo ikiwa taarifa hizi ni za kweli basi hii inaweza kuwa moja ya sababu ya sarafu yetu kuporomoka (A country with higher government debt is less likely to acquire foreign capital, leading to inflation and currency depreciation).

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]; ni masharti ya biashara (Terms of Trade). Kwa kawaida kama masharti yako ya biashara ni magumu maana yake unafukuza wawekezaji na hivyo unapunguza kiasi cha fedha za kigeni ambacho kingekuja kwako. Tanzania tuna masharti magumu sana ya biashara kwa waeekezaji kutoka nje. Hivi majuzi tulitajwa kuwa nchi ya 137 kwa urahisi wa biashara dunian, huku Rwanda wakitajwa kuwa wa 41.

Maana yake ni kwamba wawekezaji wengi watakimbilia kuwekeza Rwanda badala ya Tanzania. Hata ada za usajili kwa wawekezaji Tanzania ni dola 250 wakati Rwanda ni dola 35. Sasa unategemea mwekezaji apeleke mtaji wake wapi? Wawekezaji wakipeleka mitaji yao Rwanda moja ya faida watakayopata wanyarwanda ni sarafu ya nchi yao kuimarika. Kwa hiyo kabla BOT hawajatoa tuhuma Bloomberg wapitie upya mashrti ya uwekezaji nchini.

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]; ni matumizi holela ya fedha za kigeni ndani ya nchi. Unaporuhusu watu kufanya purchase kwa kutumia fedha za kigeni maana yake unapunguza nguvu ya manunuzi kwa sarafu yako, na matokeo yake sarafu yako itaporomoka.

Leo ukienda maduka makubwa utakuta watu wanafanya manunuzi kwa kutumia Dollar, Euro, British Pound etc. Na serikali ipo kimya tu. Inasubiri sarafu yetu iporomoke ije kukanusha kuwa kusema data zimekosewa huko Bloomberg, wakati ilipaswa kuchukua hatua mapema.

Jaribu kutembelea maduka makubwa kama Mlimani city, Rock city mall utakuta baadhi ya bidhaa zinauzwa kwa dollar. Yani mtu amebandika beji ya dola kwenye nguo anayouza na wala haoni ajabu. Ukienda anakwambia hiyo shati dola 20. Na viongozi wetu wanapita kwenye maduka hayo na wanafanya manunuzi wanaona huo ujinga na hawakemei. This is dolarization of Economy.

Nchi makini huwezi kukuta huu ujinga. Nakumbuka nilipokuwa Kenya kwenye hoteli niliyofikia nje kuna kuna duka la kubadilisha fedha. Kama umeenda na dollar zako au shilingi za kitanzania unabadilisha kwanza, unapewa pesa za Kenya ndio unaenda kulipa hotelini. Ukienda reception na pesa za kigeni hawapokei. Wanakushauri ubadili kwanza. Hii inaonesha namna walivyoi serious kulinda uchumi wao.

Hapa kwetu mtu akija dukani kwako akafanya manunuzi kwa dolar ndio unamuona wa maana, na kukenua meno yote bila kujua unaporomosha uchumi na kushusha sarafu ya nchi yako. Kwahiyo kabla BOT haijawasingizia Bloomberg ihakikishe kwanza inadhibiti matumizi holela ya pesa za kigeni kwenye manunuzi ya ndani. Pesa za kigeni zisiruhusiwe kabisa kwenye domestic market.

[HASHTAG]#Sita[/HASHTAG]; Ni hali ya kisiasa ya nchi (Political stability). Hali ya kisiasa inapokuwa nzuri inavutia wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza mitaji yao hapa na hivyo kuimarisha sarafu yetu (Increase in foreign capital, in turn, leads to an appreciation in the value of its domestic currency). Lakini hali ya kisiasa inapokuwa inatilia mashaka, wawekezaji wengi hukimbiza mitaji yao na hivyo kusababisha sarafu ya nchi kuyumba.

Hakuna muwekezaji anayependa kubughudhiwa na vyombo vya dola. Hivi majuzi tumeshuhudia magari ya Dangote yakifungwa cheni, hii inaweza kusababisha Dangote kuamua kufunga uwekezaji wake nchini ambao ni wa zaidi ya Dola Bilioni kadhaa. Ikitokea hivyo maana yake anahamisha mtaji, na moja ya athari zake ni kwenye kuporomoka kwa saraf yetu.

Lakini ukiacha Dangote, je hakuna wawekezaji wengine walibughudhiwa na kuamua kuhamisha mitaji yao? Kama wapo basi wameathiri sarafu yetu. Kwa hiyo kabla BOT hawajatupa tuhuma Bloomberg, ni vizuri wakaangalia hali ya kisiasa nchini kama inafavor wawekezaji na wakashauri serikali ichukue hatua zinaizofaa.

Zipo sababu nyingi, hizi ni baadhiu tu. Lakini hoja yangu ni kwamba BOT watafakari upya kabla ya kutupa tuhuma Bloomberg. Kuna mengi yamechangia kuporomoka kwa sarafu yetu zaidi ya hizo data kuchezewa huko Bloomberg. Tusifiche tatizo, tuliweke bayana na tusaidiane kulitatua. Tanzania ni yetu sote, tushirikiane kuijenga.

Malisa GJ

Thank you Malisa, nimejifunza uchumi kwako bila gharama, ingefaa elimu hii iwe endelevu ili wengi wanufaike nayo na ikawa kichocheo katika kuimarisha sarafu yetu
 
Just off the topic

For those who want to get into the crypo currency, the juice keep on giving it has never been too late,

Some expert predicts the bitcoin will hit higher up to 50,000 USD

But for the time being the market, it is still bullish, the exponential moving average is at 50, the bitcoin is still trading above that line.

ed034d6f2ccd5187536ab6706546aa55.jpg

To cut the crap and technical analysis, I won’t be surprised to see bitcoin hit 10,000 USD by end of this month! That’s a very modest and prudent analysis from me!

For those who are interested, it has never been too late to get onto the bandwagon, it is like saying you are too late to get onto internet!

You can buy a portion of bitcoin that simple $500, $700 it is really up to you !

The currency was created simply to get off the bias of central banks, etc just like What BOT is doing now!

And it is taking off like a rocket !

Hisabati tu hapo!
 
My Godness, hawa hawa wazungu mnaowaita wezi ndio wameahidi kumsaidia Magufuli kufikia uchumi wa kati by 2025 kweli? Siamini kama haya mawazo ni ya kijana Mtanzania anayejiita mzalendo, OK keep your fingers crossed.
Hiyo Bloomberg unayoiamini ni Mainstream Media. Ni chombo Kinachotumika tumika kwa maslahi ya makampuni makubwa kama Barrick Gold. Hatua iliyochukua serikali ya Tanzania imeitia aibu kubwa Acacia kiasi ambacho uongozi wa juu umejiuzulu. Lazima muwe na tahadhari na hizi Propoganda,
 
Thank you Malisa, nimejifunza uchumi kwako bila gharama, ingefaa elimu hii iwe endelevu ili wengi wanufaike nayo na ikawa kichocheo katika kuimarisha sarafu yetu

Nawauliza nyinyi kina Mangi sijui malisa and so many of the type.
Bei ya exchange rate leo shilingi kwa dola ya us ni iipi ya bloomberg au ya BOT?.

Kwa nini machagadema yoote hukimbilia kuaminisha watu kila kisemwacho na wazungu?.

Je ndio kutimza lengo la mtei kuanzisha chama chenu?
Ikumbukwe kwamba mtei alikosana na Baba wa taifa baada ya kukubali masharti ya IMF bila kupata baraka za Baba wa taifa na kibarua chake kikaishia uwanja wa ndege DSM wakati akirudi nchini toka IMF.

By the way ebu tujulisheni hili
Je chadema mnafuata mlengo gani wa kisiasa?
 
Hata wewe ni mbumbumbu wa maswala ya kiuchumi...
Huyo unaemtetea nimeacha kusoma aliposema tanzania ilipitia inflation ya sukari????? Inflation inapimwa kutokana na bidhaa nyingi..mchumi kuongelea inflation ya bidhaa moja ni kuonyesha hujui unachosema....Consumer Price Index (CPI) ni 'kikapu' na hakipimwi kwa bidhaa mojamoja in isolation..thats Ecos 101..alafu unadanganya Tanzania inapitia Hyperinflation na kuelekea Galloping inflation...upuuzi mtupu!!!!! niko barabarani nitarudi
lukala
 
Who is GJ Malisa and what are his credentials??? Mbona kama anarukia fani za watu?
Hivyo ndivyo Great Thinker anavyopaswa kujadili hoja, kweli? Kama Malisa ameandika hoja za msingi itoshe kumpongeza na kujadili hoja badala ya kuhoji credentials zake! Eti ".... anarukia fani za watu"! Kwani wewe ndo mwenye monopoly ya uelewa wa uchumi?
 
Hiyo Bloomberg unayoiamini ni Mainstream Media. Ni chombo Kinachotumika tumika kwa maslahi ya makampuni makubwa kama Barrick Gold. Hatua iliyochukua serikali ya Tanzania imeitia aibu kubwa Acacia kiasi ambacho uongozi wa juu umejiuzulu. Lazima muwe na tahadhari na hizi Propoganda,

Kwa hio je wewe unashauri vipi tupigane kwa hali yetu!

Aibu yao, udanganyifu wao, ulaji wao kwa maslahi yao!

Yaani nikisoma comment yako unarushia wengine vidole wao! wao!, yule yule!, wewe wewe!, lakini sijaona viashiria mimi! Mimi! ni hivi na hivi na nitajipanga hivi na vile au tufunge mkanda tu! Ndio tumemaliza!

Tupe mpango Mkuu!
 
Nawauliza nyinyi kina Mangi sijui malisa and so many of the type.
Bei ya exchange rate leo shilingi kwa dola ya us ni iipi ya bloomberg au ya BOT?.

Kwa nini machagadema yoote hukimbilia kuaminisha watu kila kisemwacho na wazungu?.

Je ndio kutimza lengo la mtei kuanzisha chama chenu?
Ikumbukwe kwamba mtei alikosana na Baba wa taifa baada ya kukubali masharti ya IMF bila kupata baraka za Baba wa taifa na kibarua chake kikaishia uwanja wa ndege DSM wakati akirudi nchini toka IMF.

By the way ebu tujulisheni hili
Je chadema mnafuata mlengo gani wa kisiasa?

Hongera sana kwa uchambuzi!!
 
Malisa GJ
________
Nimeona taarifa ya BOT ikikanusha kuwa sarafu ya Tanzania haijaporomoka, badala yake ni kwamba kuna watu kwenye financial software ya Bloomberg wameamua kuchezea data kwa makusudi kwa kuweka figure zisizo sahihi ili kupotosha. BOT wanasema kuwa tayari wameshawasiliana na Bloomberg ili kurekebisha makosa hayo.

Utetezi huu wa BOT una kasoro nyingi. Kwanza wanajitetea kuporomoka kwa shilingi dhidi ya Dola, lakini ukweli ni kwamba shilingi imeporomoka dhidi ya sarafu zote za kigeni na sio dola tu. Jana majira kama haya shilingi moja ya Kenya ilikuwa sawa na shilingi 21 za Kitanzania (bei ya kuuza), lakini leo shilingi moja ya Kenya ni sawa na shilingi 24.5.

Yani jana ulihitaji shilingi 21,000/= tu za Kitanzania kupata 1,000/= ya Kenya. Lakini leo ili upate 1,000/= ya Kenya unahitaji 24,500/= za kitanzania. Kwa hiyo shilingi yetu imeporomoka dhidi ya sarafu zote, sio dhidi ya dola tu kama BOT wanavyojaribu kueleza.

Pili nashauri BOT wajielekeze kwenye kiini cha tatizo badala ya kuficha tatizo. Kwanini wanajaribu kuficha? Kwa faida ya nani? Shilingi imeporomoka na hata waliotuma fedha leo ni mashahidi. Kwanini waseme data zimechezewa Bloomberg?
Njia rahisi ya kutatua tatizo ni kwanza kukiri kuwa lipo. Ukikataa tatizo huwezi kamwe kulitatua.

Moja ya sifa ya kuongoza taasisi za fedha ni kuwa mkweli katika kiwango cha juu kabisa, na kufanya mambo kwa nia njema sio kwa nia ya kufurahisha wanasiasa (Honesty and utmost good faith). Moja ya mambo yaliyofanya uchumi wa Uganda kuharibika vibaya na thamani ya sarafu yao kuporomoka sana ni Benki kuu ya nchi hiyo kukubali kutumika kisiasa. Idd Amin alikuwa akimuamuru Gavanor wa benki kuu nchini humo aseme uchumi upo imara hata pale mambo yalipokuwa magumu.

Anyway, kwangu taarifa hii ya kuporomoka kwa sarafu yetu ni jambo nililotegemea kulisikia. Pengine limeshtua watu kwa kuwa imekuwa ghafla sana na kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika historia ya nchi. Ndani ya masaa machache tu dola moja ya kimarekani imepanda kutoka shilingi 2,200/= hadi 2,500/=. Tumepoteza shilingi 300/= kwa kila dola moja ndani ya masaa machache.

Yani kwa mtu aliyetaka kutuma pesa nje ya nchi jana, letz say dola 5000, akachelewa na kutuma leo amepata hasara ya Shilingi milioni moja na nusu. Katika kila dola elfu moja amepata hasara ya laki tatu. Hali hii haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

Zipo sababu kadhaa zinazoweza kuwa zimesababisha mporomoko huu mkubwa kabisa katika historia.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni mfumuko wa bei (Inflation rate). Kwa kaawaida mfumuko wa bei unapokuwa mkubwa, sarafu inapoteza ile nguvu yake ya manunuzi (purchasing power) na matokeo yake inaporomoka dhidi ya sarafu za nje. Hapa nchini mfumuko wa bei umeanza kutishia wanunuzi wa bidhaa mbalimbali. Kwa mfano wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 bei ya sukari ilikuwa shilingi 1,500/= hadi 1,800/= kiwa kilo, lakini leo bei ni kati ya shilingi 2,500/= hadi 3,000/= kwa kilo.

Mfumuko wa bei umekuwa kwa zaidi ya asilimia mia moja kwenye bidhaa ya sukari. Maana yake ni kwamba we are no longer at Moderate inflation, rather tunakaribia kwenye Hyper Inflation from Galloping one. Hali hii inasababisha sarafu yetu kuoporomoka kwa kiasi kikubwa.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuwa na uchumi tegemezi wa knunua zaidi nje kuliko kuuza (import oriented economy). Tunaponunua zaidi nje maaana yake ni kwamba tunahitaji akiba kubwa ya fedha za kigeni. Tunapokuwa na demand kubwa ya fedha za kigeni maana yake pesa za kigeni zinakuwa na thamani kubwa kuliko sarafu yetu (the higher the demand the higher the price), na hivyo sarafu yetu inaporomoka. Na hii inaweza kuwa imecahangia sana kwa sababu ni kweli tunanunua zaidi nje kuliko tunavyouza.

Leo mtu akipata mtaji wa milioni 10, 20 anakimbilia China kwenda kuleta nguo, simu, saa, hereni etc. Thamani tunayouza nje ni ndogo sana kuliko tunayonunua.

Unaponunua zaidi nje unapunguza reserve ya pesa zako za kigeni na hivyo sarafu yako kuporomoka. Lakini unapouza zaidi nje unamaintain reserve ya pesa za kigeni na sarafu yako itapanda kwa sababu wanunuzi wa nje wataitafuta sarafu yako ili waweze kufanya purchase. Kabla BOT hawajabisha waangalie upya thamani tunayouza na kununua nje ya nchi ikoje (Balance of Payments).

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: ni madeni ya serikiali (Government Debt). Serikali inapokopa sana nje inapunguza security ya sarafu yake. Ni sawa na nyumba yako uliyojenga kwa milioni 100, ukitaka mkopo wa haraka bank na wakajua una shida sana wanaweza kuithaminisha hata kwa milioni 70. Na wewe utakubali tu kwa sababu una shida. Mkopoo wowote unaokopa kwa sababu una shida saaana, led to undervalue your capital asset.

Sasa jiulize je Tanzania tumewahi kuwa kwenye shida kubwa saaana kiasi cha kukopa mkopo unaoweza kuwa umepelekea capital asset zetu kuwa undervalued? Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ndugu Zitto Kabwe mwezi September mwaka huu, Taasisi ya fedha ya Credit Suisse ya nchini Uswisi, ilikiri kuikopesha Tanzania dola milioni 500 (karibu shilingi Trilioni 1.2) kwa masharti ya kulipa kwa miaka mitano, kwa riba ya karibu asilimia mia moja.

Mkopo huo ambao Tanzania inadaiwa kukopa kwa siri unatolewa na kundi mabenki (Syndicated loan) kupitia taasisi hiyo ya Credit Suisse uliibuliwa na Ndugu Zitto na Credit Suisse wakakiri kutukopesha, japo serikali ilikataa kutoa majibu ya tuhuma hizo. Kwa hiyo ikiwa taarifa hizi ni za kweli basi hii inaweza kuwa moja ya sababu ya sarafu yetu kuporomoka (A country with higher government debt is less likely to acquire foreign capital, leading to inflation and currency depreciation).

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]; ni masharti ya biashara (Terms of Trade). Kwa kawaida kama masharti yako ya biashara ni magumu maana yake unafukuza wawekezaji na hivyo unapunguza kiasi cha fedha za kigeni ambacho kingekuja kwako. Tanzania tuna masharti magumu sana ya biashara kwa waeekezaji kutoka nje. Hivi majuzi tulitajwa kuwa nchi ya 137 kwa urahisi wa biashara dunian, huku Rwanda wakitajwa kuwa wa 41.

Maana yake ni kwamba wawekezaji wengi watakimbilia kuwekeza Rwanda badala ya Tanzania. Hata ada za usajili kwa wawekezaji Tanzania ni dola 250 wakati Rwanda ni dola 35. Sasa unategemea mwekezaji apeleke mtaji wake wapi? Wawekezaji wakipeleka mitaji yao Rwanda moja ya faida watakayopata wanyarwanda ni sarafu ya nchi yao kuimarika. Kwa hiyo kabla BOT hawajatoa tuhuma Bloomberg wapitie upya mashrti ya uwekezaji nchini.

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]; ni matumizi holela ya fedha za kigeni ndani ya nchi. Unaporuhusu watu kufanya purchase kwa kutumia fedha za kigeni maana yake unapunguza nguvu ya manunuzi kwa sarafu yako, na matokeo yake sarafu yako itaporomoka.

Leo ukienda maduka makubwa utakuta watu wanafanya manunuzi kwa kutumia Dollar, Euro, British Pound etc. Na serikali ipo kimya tu. Inasubiri sarafu yetu iporomoke ije kukanusha kuwa kusema data zimekosewa huko Bloomberg, wakati ilipaswa kuchukua hatua mapema.

Jaribu kutembelea maduka makubwa kama Mlimani city, Rock city mall utakuta baadhi ya bidhaa zinauzwa kwa dollar. Yani mtu amebandika beji ya dola kwenye nguo anayouza na wala haoni ajabu. Ukienda anakwambia hiyo shati dola 20. Na viongozi wetu wanapita kwenye maduka hayo na wanafanya manunuzi wanaona huo ujinga na hawakemei. This is dolarization of Economy.

Nchi makini huwezi kukuta huu ujinga. Nakumbuka nilipokuwa Kenya kwenye hoteli niliyofikia nje kuna kuna duka la kubadilisha fedha. Kama umeenda na dollar zako au shilingi za kitanzania unabadilisha kwanza, unapewa pesa za Kenya ndio unaenda kulipa hotelini. Ukienda reception na pesa za kigeni hawapokei. Wanakushauri ubadili kwanza. Hii inaonesha namna walivyoi serious kulinda uchumi wao.

Hapa kwetu mtu akija dukani kwako akafanya manunuzi kwa dolar ndio unamuona wa maana, na kukenua meno yote bila kujua unaporomosha uchumi na kushusha sarafu ya nchi yako. Kwahiyo kabla BOT haijawasingizia Bloomberg ihakikishe kwanza inadhibiti matumizi holela ya pesa za kigeni kwenye manunuzi ya ndani. Pesa za kigeni zisiruhusiwe kabisa kwenye domestic market.

[HASHTAG]#Sita[/HASHTAG]; Ni hali ya kisiasa ya nchi (Political stability). Hali ya kisiasa inapokuwa nzuri inavutia wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza mitaji yao hapa na hivyo kuimarisha sarafu yetu (Increase in foreign capital, in turn, leads to an appreciation in the value of its domestic currency). Lakini hali ya kisiasa inapokuwa inatilia mashaka, wawekezaji wengi hukimbiza mitaji yao na hivyo kusababisha sarafu ya nchi kuyumba.

Hakuna muwekezaji anayependa kubughudhiwa na vyombo vya dola. Hivi majuzi tumeshuhudia magari ya Dangote yakifungwa cheni, hii inaweza kusababisha Dangote kuamua kufunga uwekezaji wake nchini ambao ni wa zaidi ya Dola Bilioni kadhaa. Ikitokea hivyo maana yake anahamisha mtaji, na moja ya athari zake ni kwenye kuporomoka kwa saraf yetu.

Lakini ukiacha Dangote, je hakuna wawekezaji wengine walibughudhiwa na kuamua kuhamisha mitaji yao? Kama wapo basi wameathiri sarafu yetu. Kwa hiyo kabla BOT hawajatupa tuhuma Bloomberg, ni vizuri wakaangalia hali ya kisiasa nchini kama inafavor wawekezaji na wakashauri serikali ichukue hatua zinaizofaa.

Zipo sababu nyingi, hizi ni baadhiu tu. Lakini hoja yangu ni kwamba BOT watafakari upya kabla ya kutupa tuhuma Bloomberg. Kuna mengi yamechangia kuporomoka kwa sarafu yetu zaidi ya hizo data kuchezewa huko Bloomberg. Tusifiche tatizo, tuliweke bayana na tusaidiane kulitatua. Tanzania ni yetu sote, tushirikiane kuijenga.

Malisa GJ
This is a monument of rubbish! Unatengeneza hisia zako halafu unajadili na kuhitimisha as if hisia zako ndio real world economy! Andiko halina credible empirical data/evidence, so wicked! Bloomberg siyo authority ya global forex arbitrage, unaleta stories za uongo kuhusu utawala wa Idd Amini aliyetawala hata kabla hujazaliwa, halafu unataka kutuaminisha. So wicked so cynical thinking! Unawezaje kuamini makosa ya Bloomberg kuwa ndio ukweli, lakini usiamini ukweli wa BoT ambayo ni authority katika monetary na fiscal policy za nchi? So sad for such awkward brain!
 
Hiyo Bloomberg unayoiamini ni Mainstream Media. Ni chombo Kinachotumika tumika kwa maslahi ya makampuni makubwa kama Barrick Gold. Hatua iliyochukua serikali ya Tanzania imeitia aibu kubwa Acacia kiasi ambacho uongozi wa juu umejiuzulu. Lazima muwe na tahadhari na hizi Propoganda,
Siyo ninayoiamini bali inaaminika na nchi nyingi duniani ndio maana hata BOT wamewasiliana nayo wanajua influence yake kwenye uchumi.

Tanzania hatuwezi kujitenga na global market, inawezekana ni propaganda yes, je tumejipanga vipi ku overcome hizo propaganda za makampuni makubwa kama hayo Bloomberg, Barrick kama bado tunawategemea hao hao watusaidie kufikia uchumi wa kati.
 
Kwa hio je wewe unashauri vipi tupigane kwa hali yetu!

Aibu yao, udanganyifu wao, ulaji wao kwa maslahi yao!

Yaani nikisoma comment yako unarushia wengine vidole wao! wao!, yule yule!, wewe wewe!, lakini sijaona viashiria mimi! Mimi! ni hivi na hivi na nitajipanga hivi na vile au tufunge mkanda tu! Ndio tumemaliza!

Tupe mpango Mkuu!
Mkuu mipango tuache kuibeza serikali katika harakati zake za kujenga uchumi. Rais Magufuli watanzania wataamua ifikapo 2020 katika uchaguzi mkuu.
 
hongera malisa kwa taarifa
ushauri tu BOT wajipange upya kwann taarifa yetu itolewe na bloomber inamaana hakuna msemaj wa BOT wakuwapa taarifa waTanzania ili kuwa updates kila kinachoendelea mpka mwenzio aseme ww uje ukanushe.
hamjui vizur vita ya kiuchume eh
BOT anza kutoka ww manake usipotoka wenzio watakutokea
 
Ametumia lugha nyepesi na laini sana kuelezea, kwa kifupi anaeleweka hata layman mwenye kuushughulisha ubongo wake kufikiri atamuelewa kuliko like bandiko la BoT
 
This is a monument of rubbish! Unatengeneza hisia zako halafu unajadili na kuhitimisha as if hisia zako ndio real world economy! Andiko halina credible empirical data/evidence, so wicked! Bloomberg siyo authority ya global forex arbitrage, unaleta stories za uongo kuhusu utawala wa Idd Amini aliyetawala hata kabla hujazaliwa, halafu unataka kutuaminisha. So wicked so cynical thinking! Unawezaje kuamini makosa ya Bloomberg kuwa ndio ukweli, lakini usiamini ukweli wa BoT ambayo ni authority katika monetary na fiscal policy za nchi? So sad for such awkward brain!
Punguza presha haya ni majadiliano tu, ukijadili jambo kwa mihemuko you won't achieve anything.

Ishu ni kwamba je yupi aliye sahihi kutokana na uimara wa shilingi yetu against USD, Bloomberg au BOT, ni grounds zipi zimetumiwa na Bloomberg kutoa figure hiyo, ni kweli shilingi yetu imeshuka thamani au ni propaganda za nchi tajiri tu, jadili.
 
Hayo ndio mambo yakujadili. Watu wajikite kwenye hoja.
 
Back
Top Bottom