BoT wajitafakari kabla ya kuwatuhumu Bloomberg

Hiyo site haina tofauti na Wikipedia ni site uchwara .kaangalie exchange rate za maduka ya pesa za kigeni na mabenki yote Tanzania hakuna rate kama hiyo
Acheni huu ujinga kama ni Uchwara kwanini BOT wanawasilana nao!
 
Kwa njia sahihi anayefuata Rais Magufuli ndio maana European Union majuzi walitangaza rasmi watamsaidia kufikia 2025 Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati. Hili ni pigo kwa watu wa aina yako.
ila nyie ndugu kwakuishi Kwa matumaini hamjambo! mimi nilifikiri ndio ile Rais kasema Nchi yetu ni Tajiri kumbe tunategemea mifuko ya Wazungu tuko Serious kweli...!
 
Economic slump,,, tatizo fedha wamezikusanya na hawazitoa, maduka yanakufa kodi imekuwa kubwa, mzunguko wa pesa hakuna, mm mwenyewe niko mbioni kufunga biashara maana kodi imekuwa kubwa kuzidi kodi ya pango la nyumba
 
Bandiko la akili sana hata watu wa Lumumba kama hawatalazimishwa kulipinga najua wataliunga mkono. Au siyo jingalao ?
Hili ni bandiko la level ya kijiweni.mimi nimeongelea trend na kuupinga uzushi na uongo wa kimataifa.Hakuna Wild beast mwenye uwezo huo.
 
...mabadiliko yako yapi ndugu yangu unayozungumzia!
Kutoka kwenye uchumi wa Kudanganyana kwenda kwenye uchumi halisi. Maana yangu mkuu lazima ufanye kazi kama unataka ku survive. Hatua nyingine ni kuhakikisha madini na maliasili za watanzania zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote. Hao Bloomberg ni wakala wanaolipwa na Barrick Gold katika kutangaza biashara zao
 
Who is GJ Malisa and what are his credentials??? Mbona kama anarukia fani za watu?
Muhimu tusome [emoji115] [emoji115] [emoji115] kilichoandikwa, ruksa kuchangia hoja kwa afya ya Uchumi wetu...!!,

Mwanabodi, [emoji1] [emoji1] [emoji23] [emoji23] hayo mengine binafsi, wachie mkewe na family yake..
 
Malisa GJ
________
Nimeona taarifa ya BOT ikikanusha kuwa sarafu ya Tanzania haijaporomoka, badala yake ni kwamba kuna watu kwenye financial software ya Bloomberg wameamua kuchezea data kwa makusudi kwa kuweka figure zisizo sahihi ili kupotosha. BOT wanasema kuwa tayari wameshawasiliana na Bloomberg ili kurekebisha makosa hayo.

Utetezi huu wa BOT una kasoro nyingi. Kwanza wanajitetea kuporomoka kwa shilingi dhidi ya Dola, lakini ukweli ni kwamba shilingi imeporomoka dhidi ya sarafu zote za kigeni na sio dola tu. Jana majira kama haya shilingi moja ya Kenya ilikuwa sawa na shilingi 21 za Kitanzania (bei ya kuuza), lakini leo shilingi moja ya Kenya ni sawa na shilingi 24.5.

Yani jana ulihitaji shilingi 21,000/= tu za Kitanzania kupata 1,000/= ya Kenya. Lakini leo ili upate 1,000/= ya Kenya unahitaji 24,500/= za kitanzania. Kwa hiyo shilingi yetu imeporomoka dhidi ya sarafu zote, sio dhidi ya dola tu kama BOT wanavyojaribu kueleza.

Pili nashauri BOT wajielekeze kwenye kiini cha tatizo badala ya kuficha tatizo. Kwanini wanajaribu kuficha? Kwa faida ya nani? Shilingi imeporomoka na hata waliotuma fedha leo ni mashahidi. Kwanini waseme data zimechezewa Bloomberg?
Njia rahisi ya kutatua tatizo ni kwanza kukiri kuwa lipo. Ukikataa tatizo huwezi kamwe kulitatua.

Moja ya sifa ya kuongoza taasisi za fedha ni kuwa mkweli katika kiwango cha juu kabisa, na kufanya mambo kwa nia njema sio kwa nia ya kufurahisha wanasiasa (Honesty and utmost good faith). Moja ya mambo yaliyofanya uchumi wa Uganda kuharibika vibaya na thamani ya sarafu yao kuporomoka sana ni Benki kuu ya nchi hiyo kukubali kutumika kisiasa. Idd Amin alikuwa akimuamuru Gavanor wa benki kuu nchini humo aseme uchumi upo imara hata pale mambo yalipokuwa magumu.

Anyway, kwangu taarifa hii ya kuporomoka kwa sarafu yetu ni jambo nililotegemea kulisikia. Pengine limeshtua watu kwa kuwa imekuwa ghafla sana na kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika historia ya nchi. Ndani ya masaa machache tu dola moja ya kimarekani imepanda kutoka shilingi 2,200/= hadi 2,500/=. Tumepoteza shilingi 300/= kwa kila dola moja ndani ya masaa machache.

Yani kwa mtu aliyetaka kutuma pesa nje ya nchi jana, letz say dola 5000, akachelewa na kutuma leo amepata hasara ya Shilingi milioni moja na nusu. Katika kila dola elfu moja amepata hasara ya laki tatu. Hali hii haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

Zipo sababu kadhaa zinazoweza kuwa zimesababisha mporomoko huu mkubwa kabisa katika historia.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni mfumuko wa bei (Inflation rate). Kwa kaawaida mfumuko wa bei unapokuwa mkubwa, sarafu inapoteza ile nguvu yake ya manunuzi (purchasing power) na matokeo yake inaporomoka dhidi ya sarafu za nje. Hapa nchini mfumuko wa bei umeanza kutishia wanunuzi wa bidhaa mbalimbali. Kwa mfano wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 bei ya sukari ilikuwa shilingi 1,500/= hadi 1,800/= kiwa kilo, lakini leo bei ni kati ya shilingi 2,500/= hadi 3,000/= kwa kilo.

Mfumuko wa bei umekuwa kwa zaidi ya asilimia mia moja kwenye bidhaa ya sukari. Maana yake ni kwamba we are no longer at Moderate inflation, rather tunakaribia kwenye Hyper Inflation from Galloping one. Hali hii inasababisha sarafu yetu kuoporomoka kwa kiasi kikubwa.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuwa na uchumi tegemezi wa knunua zaidi nje kuliko kuuza (import oriented economy). Tunaponunua zaidi nje maaana yake ni kwamba tunahitaji akiba kubwa ya fedha za kigeni. Tunapokuwa na demand kubwa ya fedha za kigeni maana yake pesa za kigeni zinakuwa na thamani kubwa kuliko sarafu yetu (the higher the demand the higher the price), na hivyo sarafu yetu inaporomoka. Na hii inaweza kuwa imecahangia sana kwa sababu ni kweli tunanunua zaidi nje kuliko tunavyouza.

Leo mtu akipata mtaji wa milioni 10, 20 anakimbilia China kwenda kuleta nguo, simu, saa, hereni etc. Thamani tunayouza nje ni ndogo sana kuliko tunayonunua.

Unaponunua zaidi nje unapunguza reserve ya pesa zako za kigeni na hivyo sarafu yako kuporomoka. Lakini unapouza zaidi nje unamaintain reserve ya pesa za kigeni na sarafu yako itapanda kwa sababu wanunuzi wa nje wataitafuta sarafu yako ili waweze kufanya purchase. Kabla BOT hawajabisha waangalie upya thamani tunayouza na kununua nje ya nchi ikoje (Balance of Payments).

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: ni madeni ya serikiali (Government Debt). Serikali inapokopa sana nje inapunguza security ya sarafu yake. Ni sawa na nyumba yako uliyojenga kwa milioni 100, ukitaka mkopo wa haraka bank na wakajua una shida sana wanaweza kuithaminisha hata kwa milioni 70. Na wewe utakubali tu kwa sababu una shida. Mkopoo wowote unaokopa kwa sababu una shida saaana, led to undervalue your capital asset.

Sasa jiulize je Tanzania tumewahi kuwa kwenye shida kubwa saaana kiasi cha kukopa mkopo unaoweza kuwa umepelekea capital asset zetu kuwa undervalued? Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ndugu Zitto Kabwe mwezi September mwaka huu, Taasisi ya fedha ya Credit Suisse ya nchini Uswisi, ilikiri kuikopesha Tanzania dola milioni 500 (karibu shilingi Trilioni 1.2) kwa masharti ya kulipa kwa miaka mitano, kwa riba ya karibu asilimia mia moja.

Mkopo huo ambao Tanzania inadaiwa kukopa kwa siri unatolewa na kundi mabenki (Syndicated loan) kupitia taasisi hiyo ya Credit Suisse uliibuliwa na Ndugu Zitto na Credit Suisse wakakiri kutukopesha, japo serikali ilikataa kutoa majibu ya tuhuma hizo. Kwa hiyo ikiwa taarifa hizi ni za kweli basi hii inaweza kuwa moja ya sababu ya sarafu yetu kuporomoka (A country with higher government debt is less likely to acquire foreign capital, leading to inflation and currency depreciation).

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]; ni masharti ya biashara (Terms of Trade). Kwa kawaida kama masharti yako ya biashara ni magumu maana yake unafukuza wawekezaji na hivyo unapunguza kiasi cha fedha za kigeni ambacho kingekuja kwako. Tanzania tuna masharti magumu sana ya biashara kwa waeekezaji kutoka nje. Hivi majuzi tulitajwa kuwa nchi ya 137 kwa urahisi wa biashara dunian, huku Rwanda wakitajwa kuwa wa 41.

Maana yake ni kwamba wawekezaji wengi watakimbilia kuwekeza Rwanda badala ya Tanzania. Hata ada za usajili kwa wawekezaji Tanzania ni dola 250 wakati Rwanda ni dola 35. Sasa unategemea mwekezaji apeleke mtaji wake wapi? Wawekezaji wakipeleka mitaji yao Rwanda moja ya faida watakayopata wanyarwanda ni sarafu ya nchi yao kuimarika. Kwa hiyo kabla BOT hawajatoa tuhuma Bloomberg wapitie upya mashrti ya uwekezaji nchini.

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]; ni matumizi holela ya fedha za kigeni ndani ya nchi. Unaporuhusu watu kufanya purchase kwa kutumia fedha za kigeni maana yake unapunguza nguvu ya manunuzi kwa sarafu yako, na matokeo yake sarafu yako itaporomoka.

Leo ukienda maduka makubwa utakuta watu wanafanya manunuzi kwa kutumia Dollar, Euro, British Pound etc. Na serikali ipo kimya tu. Inasubiri sarafu yetu iporomoke ije kukanusha kuwa kusema data zimekosewa huko Bloomberg, wakati ilipaswa kuchukua hatua mapema.

Jaribu kutembelea maduka makubwa kama Mlimani city, Rock city mall utakuta baadhi ya bidhaa zinauzwa kwa dollar. Yani mtu amebandika beji ya dola kwenye nguo anayouza na wala haoni ajabu. Ukienda anakwambia hiyo shati dola 20. Na viongozi wetu wanapita kwenye maduka hayo na wanafanya manunuzi wanaona huo ujinga na hawakemei. This is dolarization of Economy.

Nchi makini huwezi kukuta huu ujinga. Nakumbuka nilipokuwa Kenya kwenye hoteli niliyofikia nje kuna kuna duka la kubadilisha fedha. Kama umeenda na dollar zako au shilingi za kitanzania unabadilisha kwanza, unapewa pesa za Kenya ndio unaenda kulipa hotelini. Ukienda reception na pesa za kigeni hawapokei. Wanakushauri ubadili kwanza. Hii inaonesha namna walivyoi serious kulinda uchumi wao.

Hapa kwetu mtu akija dukani kwako akafanya manunuzi kwa dolar ndio unamuona wa maana, na kukenua meno yote bila kujua unaporomosha uchumi na kushusha sarafu ya nchi yako. Kwahiyo kabla BOT haijawasingizia Bloomberg ihakikishe kwanza inadhibiti matumizi holela ya pesa za kigeni kwenye manunuzi ya ndani. Pesa za kigeni zisiruhusiwe kabisa kwenye domestic market.

[HASHTAG]#Sita[/HASHTAG]; Ni hali ya kisiasa ya nchi (Political stability). Hali ya kisiasa inapokuwa nzuri inavutia wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza mitaji yao hapa na hivyo kuimarisha sarafu yetu (Increase in foreign capital, in turn, leads to an appreciation in the value of its domestic currency). Lakini hali ya kisiasa inapokuwa inatilia mashaka, wawekezaji wengi hukimbiza mitaji yao na hivyo kusababisha sarafu ya nchi kuyumba.

Hakuna muwekezaji anayependa kubughudhiwa na vyombo vya dola. Hivi majuzi tumeshuhudia magari ya Dangote yakifungwa cheni, hii inaweza kusababisha Dangote kuamua kufunga uwekezaji wake nchini ambao ni wa zaidi ya Dola Bilioni kadhaa. Ikitokea hivyo maana yake anahamisha mtaji, na moja ya athari zake ni kwenye kuporomoka kwa saraf yetu.

Lakini ukiacha Dangote, je hakuna wawekezaji wengine walibughudhiwa na kuamua kuhamisha mitaji yao? Kama wapo basi wameathiri sarafu yetu. Kwa hiyo kabla BOT hawajatupa tuhuma Bloomberg, ni vizuri wakaangalia hali ya kisiasa nchini kama inafavor wawekezaji na wakashauri serikali ichukue hatua zinaizofaa.

Zipo sababu nyingi, hizi ni baadhiu tu. Lakini hoja yangu ni kwamba BOT watafakari upya kabla ya kutupa tuhuma Bloomberg. Kuna mengi yamechangia kuporomoka kwa sarafu yetu zaidi ya hizo data kuchezewa huko Bloomberg. Tusifiche tatizo, tuliweke bayana na tusaidiane kulitatua. Tanzania ni yetu sote, tushirikiane kuijenga.

Malisa GJ

HABARI,
"Quinine,Hongera kwa post yako iliyojitosheleza mkuu hongera sana ,Mimi binafsi namsubiri kwa hamu sana ZITTO ZUBERI KABWE aweke ya kwake humu jamvini.Nina uhakika atakuwa na mengi muhimu ya kuyasema na mengi yaliokuwa nyuma y pazia kuhusu swala hili.

LUMUMBA
 
Kwa njia sahihi anayefuata Rais Magufuli ndio maana European Union majuzi walitangaza rasmi watamsaidia kufikia 2025 Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati. Hili ni pigo kwa watu wa aina yako.
My Godness, hawa hawa wazungu mnaowaita wezi ndio wameahidi kumsaidia Magufuli kufikia uchumi wa kati by 2025 kweli? Siamini kama haya mawazo ni ya kijana Mtanzania anayejiita mzalendo, OK keep your fingers crossed.
 
"Quinine,
Mfumuko wa bei mkubwa unakuja sasa.

LUMUMBA
 
Hata wewe ni mbumbumbu wa maswala ya kiuchumi...
Huyo unaemtetea nimeacha kusoma aliposema tanzania ilipitia inflation ya sukari????? Inflation inapimwa kutokana na bidhaa nyingi..mchumi kuongelea inflation ya bidhaa moja ni kuonyesha hujui unachosema....Consumer Price Index (CPI) ni 'kikapu' na hakipimwi kwa bidhaa mojamoja in isolation..thats Ecos 101..alafu unadanganya Tanzania inapitia Hyperinflation na kuelekea Galloping inflation...upuuzi mtupu!!!!! niko barabarani nitarudi
Tupe shule jibu hoja vizuri ili tuchangie kuona ni wapi tumekosea, tusimshambulie mtoa hoja ila tujibu hoja zake kwa usahihi.
 
My Godness, hawa hawa wazungu mnaowaita wezi ndio wameahidi kumsaidia Magufuli kufikia uchumi wa kati by 2025 kweli? Siamini kama haya mawazo ni ya kijana Mtanzania anayejiita mzalendo, OK keep your fingers crossed.
Hakuna kwenye community yeyote wanakosekana wezi ama vibaka.
 
Who is GJ Malisa and what are his credentials??? Mbona kama anarukia fani za watu?
NI MTANZANIA RAIA MWEMA, MWENYE UHURU WA KUTOA MAONI BILA KUVUNJA KATIBA., WEWE UNAHOJI KAMA NANI????????????????!!!!!!!! [HASHTAG]#FREENATION[/HASHTAG]
 
Mpaka dakiki hii 1 USD = 2,548.21 TZS. tayari BOT wamekanusha. Wanaobadiri fedha wanatumia kiwango kipya. Sasa hapo ndio utaelewa madhara ya kuingiza siasa kwenye professional issues. www.xe.com/currencyconverter/convert/?Amount=1&From=USD&To=TZS

Muogope Mungu!

The math will always stuck against you!

Mathalani off the topic, kama marekani wangekua wana uwezo wangeweza kuzuia digital money kama bitcoins, ethereum, Lite nk

Sasa mwaka jana mida kama hii

1 Bitcoin = 700USD

Leo 1000% better

1 bitcoin = 7000USD

What are they going to do? Can’t do anything really! people are stashing their hard paper dollars into crypto currency,

Demand Demand drive the numbers up !

Sasa taratibu wanayofanya BOT would only increase the demand, and suffocate the supply, that will crate fake out imbalance, few people would want to trade a low value dollar in their own country while you could get a better exchange in Kenya! As some one commented the price of Kenya shillings also gone up in almost parallel with the dollar ie at 2500 price range to a 1 Dollar, ie 13% increase!

Which probably will be the same to KSH,

Hatari kucheza na hisabati. What you are going to do!

Shoot the math![emoji3] or call it for questioning at central police, in violation of diverging the truthfulness of statistical data! I can’t wait for that day in court !
 
In short, this is a World Wide Web, you can’t live or survive in isolation, the economy are interdependence, we have to concentrate on our core fundamentals and our strength, see what we are doing wrong and fix it, we MUST be CRITiCS to our own self, the economic policy should be leading the way and NOT politics, but unfortunately politics are poisoning the country to the detrimental of the country. The economy fundamentals are always right, you can’t cheat it, fool it or playing around with it, it is just TOO strong, it will bite you!

It is like playing with MATH! How can you stupidly believe yourself than the numbers, the stats, the rules and formulas of MATH, and that’s economy, it is simple as that! You can’t lie to it or worst still lie to yourself.

Or worst still putting people to jail because they question your inadvertently inadequacy on economy fronts.

You can’t be rogue in economy without being smart circumnavigate your way in this ugly ugly world, it needs strong head, smartness and wit! You have to be sharp in your game at get go!

As aspiring trader, I learnt that lesson a while back, I give you an example, I don’t like what acacia mining has done to the economy, it was unfair deal made out of corruption Republic back in the day and Mh Rais is right to angry, he has seen it first hand, it was a bad deal, but fortunately people like myself we are trying to make the best out of it, invest in shares buying low and sell it high, and that’s my smart revenge! I work with economic fundamentals and not with my EMOTIONs!

I guess the government won’t like the Tanzanians buying shares in Acacia mining but the economy say otherwise, and this is just personnel perspective, showing that if you remove emotions and work with FuNDAMENTALS personnel approach and likewise as a country you will get out of the ditch and deep water.

Not other way round, painting a rosy picture, forcing media to roll on , forcing others to bide by your way but No Other way, it has never been a better way of steering the country.

The perfect example, the tweak of numbers punched by lone employee at Bloomberg thousands of miles away, causing tremor in Tanzania, can we all stop and think for a second!, how many people in Tanzania knows Bloomberg and let alone knows what they are jobs are? A just a private institute and not even a government apparatus, but has such a STRONg effect in shores of Tanzania affecting a price of kilo of domestic product like Sembe to an innocent consumer as far as Kigoma, of which probably 99.9% don’t know what the hell Bloomberg is, let alone a lone employee of that company.

And that’s should enough to bring reality to Mh Rais!

It should be a cause of concern! He might be fighting an economic war, but I honestly like my President and I pray everyday he succeed and I believe we all are, but please,
“usitumie bumbuki kuulia Panya ndani ya nyumba” work smart, surround yourself with the real honest people, who can tell you the truth when it hurts, the economists, and less yes sir, not those who are bowing to you! I know the latter is your personnel preference but believe me, they are the ones who are dragging your presidency and the country to a quagmire!

Much love!
Hope someone will understand this advice and act accordingly
 
HABARI,
"Quinine,
Mfumuko wa bei mkubwa unakuja sasa.

LUMUMBA
tanzania-inflation-cpi@2x.png
 
Hili ni bandiko la level ya kijiweni.mimi nimeongelea trend na kuupinga uzushi na uongo wa kimataifa.Hakuna Wild beast mwenye uwezo huo.
Jibu hoja tujenge uchumi wa nchi yetu, tueleweshe kama ni vizuri kutumia dollar kama hela ya Tanzania taja faida na hasara zake. Siasa weka mbali na uchumi
 
Back
Top Bottom