BoT wajitafakari kabla ya kuwatuhumu Bloomberg

BoT wajitafakari kabla ya kuwatuhumu Bloomberg

Malisa GJ
________
Nimeona taarifa ya BOT ikikanusha kuwa sarafu ya Tanzania haijaporomoka, badala yake ni kwamba kuna watu kwenye financial software ya Bloomberg wameamua kuchezea data kwa makusudi kwa kuweka figure zisizo sahihi ili kupotosha. BOT wanasema kuwa tayari wameshawasiliana na Bloomberg ili kurekebisha makosa hayo.

Utetezi huu wa BOT una kasoro nyingi. Kwanza wanajitetea kuporomoka kwa shilingi dhidi ya Dola, lakini ukweli ni kwamba shilingi imeporomoka dhidi ya sarafu zote za kigeni na sio dola tu. Jana majira kama haya shilingi moja ya Kenya ilikuwa sawa na shilingi 21 za Kitanzania (bei ya kuuza), lakini leo shilingi moja ya Kenya ni sawa na shilingi 24.5.

Yani jana ulihitaji shilingi 21,000/= tu za Kitanzania kupata 1,000/= ya Kenya. Lakini leo ili upate 1,000/= ya Kenya unahitaji 24,500/= za kitanzania. Kwa hiyo shilingi yetu imeporomoka dhidi ya sarafu zote, sio dhidi ya dola tu kama BOT wanavyojaribu kueleza.

Pili nashauri BOT wajielekeze kwenye kiini cha tatizo badala ya kuficha tatizo. Kwanini wanajaribu kuficha? Kwa faida ya nani? Shilingi imeporomoka na hata waliotuma fedha leo ni mashahidi. Kwanini waseme data zimechezewa Bloomberg?
Njia rahisi ya kutatua tatizo ni kwanza kukiri kuwa lipo. Ukikataa tatizo huwezi kamwe kulitatua.

Moja ya sifa ya kuongoza taasisi za fedha ni kuwa mkweli katika kiwango cha juu kabisa, na kufanya mambo kwa nia njema sio kwa nia ya kufurahisha wanasiasa (Honesty and utmost good faith). Moja ya mambo yaliyofanya uchumi wa Uganda kuharibika vibaya na thamani ya sarafu yao kuporomoka sana ni Benki kuu ya nchi hiyo kukubali kutumika kisiasa. Idd Amin alikuwa akimuamuru Gavanor wa benki kuu nchini humo aseme uchumi upo imara hata pale mambo yalipokuwa magumu.

Anyway, kwangu taarifa hii ya kuporomoka kwa sarafu yetu ni jambo nililotegemea kulisikia. Pengine limeshtua watu kwa kuwa imekuwa ghafla sana na kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika historia ya nchi. Ndani ya masaa machache tu dola moja ya kimarekani imepanda kutoka shilingi 2,200/= hadi 2,500/=. Tumepoteza shilingi 300/= kwa kila dola moja ndani ya masaa machache.

Yani kwa mtu aliyetaka kutuma pesa nje ya nchi jana, letz say dola 5000, akachelewa na kutuma leo amepata hasara ya Shilingi milioni moja na nusu. Katika kila dola elfu moja amepata hasara ya laki tatu. Hali hii haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

Zipo sababu kadhaa zinazoweza kuwa zimesababisha mporomoko huu mkubwa kabisa katika historia.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni mfumuko wa bei (Inflation rate). Kwa kaawaida mfumuko wa bei unapokuwa mkubwa, sarafu inapoteza ile nguvu yake ya manunuzi (purchasing power) na matokeo yake inaporomoka dhidi ya sarafu za nje. Hapa nchini mfumuko wa bei umeanza kutishia wanunuzi wa bidhaa mbalimbali. Kwa mfano wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 bei ya sukari ilikuwa shilingi 1,500/= hadi 1,800/= kiwa kilo, lakini leo bei ni kati ya shilingi 2,500/= hadi 3,000/= kwa kilo.

Mfumuko wa bei umekuwa kwa zaidi ya asilimia mia moja kwenye bidhaa ya sukari. Maana yake ni kwamba we are no longer at Moderate inflation, rather tunakaribia kwenye Hyper Inflation from Galloping one. Hali hii inasababisha sarafu yetu kuoporomoka kwa kiasi kikubwa.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuwa na uchumi tegemezi wa knunua zaidi nje kuliko kuuza (import oriented economy). Tunaponunua zaidi nje maaana yake ni kwamba tunahitaji akiba kubwa ya fedha za kigeni. Tunapokuwa na demand kubwa ya fedha za kigeni maana yake pesa za kigeni zinakuwa na thamani kubwa kuliko sarafu yetu (the higher the demand the higher the price), na hivyo sarafu yetu inaporomoka. Na hii inaweza kuwa imecahangia sana kwa sababu ni kweli tunanunua zaidi nje kuliko tunavyouza.

Leo mtu akipata mtaji wa milioni 10, 20 anakimbilia China kwenda kuleta nguo, simu, saa, hereni etc. Thamani tunayouza nje ni ndogo sana kuliko tunayonunua.

Unaponunua zaidi nje unapunguza reserve ya pesa zako za kigeni na hivyo sarafu yako kuporomoka. Lakini unapouza zaidi nje unamaintain reserve ya pesa za kigeni na sarafu yako itapanda kwa sababu wanunuzi wa nje wataitafuta sarafu yako ili waweze kufanya purchase. Kabla BOT hawajabisha waangalie upya thamani tunayouza na kununua nje ya nchi ikoje (Balance of Payments).

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: ni madeni ya serikiali (Government Debt). Serikali inapokopa sana nje inapunguza security ya sarafu yake. Ni sawa na nyumba yako uliyojenga kwa milioni 100, ukitaka mkopo wa haraka bank na wakajua una shida sana wanaweza kuithaminisha hata kwa milioni 70. Na wewe utakubali tu kwa sababu una shida. Mkopoo wowote unaokopa kwa sababu una shida saaana, led to undervalue your capital asset.

Sasa jiulize je Tanzania tumewahi kuwa kwenye shida kubwa saaana kiasi cha kukopa mkopo unaoweza kuwa umepelekea capital asset zetu kuwa undervalued? Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ndugu Zitto Kabwe mwezi September mwaka huu, Taasisi ya fedha ya Credit Suisse ya nchini Uswisi, ilikiri kuikopesha Tanzania dola milioni 500 (karibu shilingi Trilioni 1.2) kwa masharti ya kulipa kwa miaka mitano, kwa riba ya karibu asilimia mia moja.

Mkopo huo ambao Tanzania inadaiwa kukopa kwa siri unatolewa na kundi mabenki (Syndicated loan) kupitia taasisi hiyo ya Credit Suisse uliibuliwa na Ndugu Zitto na Credit Suisse wakakiri kutukopesha, japo serikali ilikataa kutoa majibu ya tuhuma hizo. Kwa hiyo ikiwa taarifa hizi ni za kweli basi hii inaweza kuwa moja ya sababu ya sarafu yetu kuporomoka (A country with higher government debt is less likely to acquire foreign capital, leading to inflation and currency depreciation).

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]; ni masharti ya biashara (Terms of Trade). Kwa kawaida kama masharti yako ya biashara ni magumu maana yake unafukuza wawekezaji na hivyo unapunguza kiasi cha fedha za kigeni ambacho kingekuja kwako. Tanzania tuna masharti magumu sana ya biashara kwa waeekezaji kutoka nje. Hivi majuzi tulitajwa kuwa nchi ya 137 kwa urahisi wa biashara dunian, huku Rwanda wakitajwa kuwa wa 41.

Maana yake ni kwamba wawekezaji wengi watakimbilia kuwekeza Rwanda badala ya Tanzania. Hata ada za usajili kwa wawekezaji Tanzania ni dola 250 wakati Rwanda ni dola 35. Sasa unategemea mwekezaji apeleke mtaji wake wapi? Wawekezaji wakipeleka mitaji yao Rwanda moja ya faida watakayopata wanyarwanda ni sarafu ya nchi yao kuimarika. Kwa hiyo kabla BOT hawajatoa tuhuma Bloomberg wapitie upya mashrti ya uwekezaji nchini.

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]; ni matumizi holela ya fedha za kigeni ndani ya nchi. Unaporuhusu watu kufanya purchase kwa kutumia fedha za kigeni maana yake unapunguza nguvu ya manunuzi kwa sarafu yako, na matokeo yake sarafu yako itaporomoka.

Leo ukienda maduka makubwa utakuta watu wanafanya manunuzi kwa kutumia Dollar, Euro, British Pound etc. Na serikali ipo kimya tu. Inasubiri sarafu yetu iporomoke ije kukanusha kuwa kusema data zimekosewa huko Bloomberg, wakati ilipaswa kuchukua hatua mapema.

Jaribu kutembelea maduka makubwa kama Mlimani city, Rock city mall utakuta baadhi ya bidhaa zinauzwa kwa dollar. Yani mtu amebandika beji ya dola kwenye nguo anayouza na wala haoni ajabu. Ukienda anakwambia hiyo shati dola 20. Na viongozi wetu wanapita kwenye maduka hayo na wanafanya manunuzi wanaona huo ujinga na hawakemei. This is dolarization of Economy.

Nchi makini huwezi kukuta huu ujinga. Nakumbuka nilipokuwa Kenya kwenye hoteli niliyofikia nje kuna kuna duka la kubadilisha fedha. Kama umeenda na dollar zako au shilingi za kitanzania unabadilisha kwanza, unapewa pesa za Kenya ndio unaenda kulipa hotelini. Ukienda reception na pesa za kigeni hawapokei. Wanakushauri ubadili kwanza. Hii inaonesha namna walivyoi serious kulinda uchumi wao.

Hapa kwetu mtu akija dukani kwako akafanya manunuzi kwa dolar ndio unamuona wa maana, na kukenua meno yote bila kujua unaporomosha uchumi na kushusha sarafu ya nchi yako. Kwahiyo kabla BOT haijawasingizia Bloomberg ihakikishe kwanza inadhibiti matumizi holela ya pesa za kigeni kwenye manunuzi ya ndani. Pesa za kigeni zisiruhusiwe kabisa kwenye domestic market.

[HASHTAG]#Sita[/HASHTAG]; Ni hali ya kisiasa ya nchi (Political stability). Hali ya kisiasa inapokuwa nzuri inavutia wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza mitaji yao hapa na hivyo kuimarisha sarafu yetu (Increase in foreign capital, in turn, leads to an appreciation in the value of its domestic currency). Lakini hali ya kisiasa inapokuwa inatilia mashaka, wawekezaji wengi hukimbiza mitaji yao na hivyo kusababisha sarafu ya nchi kuyumba.

Hakuna muwekezaji anayependa kubughudhiwa na vyombo vya dola. Hivi majuzi tumeshuhudia magari ya Dangote yakifungwa cheni, hii inaweza kusababisha Dangote kuamua kufunga uwekezaji wake nchini ambao ni wa zaidi ya Dola Bilioni kadhaa. Ikitokea hivyo maana yake anahamisha mtaji, na moja ya athari zake ni kwenye kuporomoka kwa saraf yetu.

Lakini ukiacha Dangote, je hakuna wawekezaji wengine walibughudhiwa na kuamua kuhamisha mitaji yao? Kama wapo basi wameathiri sarafu yetu. Kwa hiyo kabla BOT hawajatupa tuhuma Bloomberg, ni vizuri wakaangalia hali ya kisiasa nchini kama inafavor wawekezaji na wakashauri serikali ichukue hatua zinaizofaa.

Zipo sababu nyingi, hizi ni baadhiu tu. Lakini hoja yangu ni kwamba BOT watafakari upya kabla ya kutupa tuhuma Bloomberg. Kuna mengi yamechangia kuporomoka kwa sarafu yetu zaidi ya hizo data kuchezewa huko Bloomberg. Tusifiche tatizo, tuliweke bayana na tusaidiane kulitatua. Tanzania ni yetu sote, tushirikiane kuijenga.

Malisa GJ

Mhe. Dr Mwigulu Nchemba mchumi wa kiwango cha juu kabisa tueleze kweli wa haya maneno mazito
 
Malisa GJ
________
Nimeona taarifa ya BOT ikikanusha kuwa sarafu ya Tanzania haijaporomoka, badala yake ni kwamba kuna watu kwenye financial software ya Bloomberg wameamua kuchezea data kwa makusudi kwa kuweka figure zisizo sahihi ili kupotosha. BOT wanasema kuwa tayari wameshawasiliana na Bloomberg ili kurekebisha makosa hayo.

Malisa GJ

Ongeza;

1. Tusidhibiti kupitiliza usajili na utendaji wa NGOsi zinazoingiza pesa za kigeni kuboresha maisha ya jamii nk.
2. Wakulima wasafirishe mahindi/nafaka kuuza nje bila shurti la kusaga unga nk. Unga una shelf life ya wiki ngapi.??
3. Sirikali idhibiti uingizaji wa vipodozi na vitu visivyo na tija au maslahi kwa wengi.
4. Wakandarasi/ Waelekezi wa miradi mikubwa mfano Flyovers waongeze ajira kwa wazawa na manunuzi ya ndani na wawalipe kwa dola kama wao wanavyolipwa.
5. Wageni na watalii wakipanda Bombardier safari za ndani walipie kwa dollar
 
Yaaa hii sio kuporomoka tu..
Kuna siku itaanguka kabisaaa...
Us $ 1= Tsh laki 1 ( 100,000) hapo to wale walo na macho watapoambiwa tazama na wasione pia.
 
Hiv inch jiran wana rasilimali zip zaid ya kuwashinda Tz.....ni kwa sababu zipi hasa tukawa nyuma kwa kila kitu kama mikia....yaan inaumiza kichwa kwakweli....yaan tuangalie tu...

Mnajua kua planing is a source of the successfull.
Without good planing in any issue or program u want to do never get possitive successful
 
Nafkir tukiwa na good planing ama tukae tufikirie mbinu mbadala or plan B....

Naamin saraf ya nchi yetu itarud na kuwa na thaman kama nchi nyengine ama kuliko....

Ila nashaur Dr...Maguful aendelee kuumiza kichwa afichue wapi hajatumbuaaa.......

Akifanikiwa hasa kutoa majipu yote makomavuuu...tutafanikiwa tu...


Hongera Mr... Rais kwa uchapaji kazi wako..

Mungu Akutie nguvu zaid utumikie tafalako kama unavyotumikia now kwa nia safi.
Tunafaham lengo lako ni mafanikio ya nchi yetu.
Mungu atalifanikisha hilo.
 
Hiyo imeshatoka Matamko ya kukurupuka kuficha aibu ya serikali hayatarudisha dollar chini.

Bado kidogo wataleta noti ya elfu 20
usiangaike na dollar tunajiandaa kujiunga na petro-yuan!
=====
Changamato za kuboresha uchumi zinahitaji mbinu nyingi. China kuna kipindi ili devalue ela yake kama mbinu ya kurahisisha ununuaji wa bidhaa zake soko la kimataifa. Ilifanikiwa sana, mpaka US akalalamika WTO! Kwa mipango yetu ya kuwa na viwanda 100 kila mkoa lazima tuanze na mikakati ya kuuza bidhaa kwenye masoko ya kimataifa. Tuiunge mkono serikali na pale pakuisaidia tuifanye hivyo haraka kimawazo hata kwa mali.
 
Naongeza sababunyingine ya dola kushuka.
Kuondoka kwa Govana wa zamani ambaye alijua benki kuu ni nini na kumweka professa wa Law badala ya ntu wa fedha ama uchumi. Lol ! Nchi hii tunapenda kujiingiza kwenye matatizo wenyewe.
Kwani GAVANA mpya ameshaanza kufanya kazi au unakurupuka mkuu?
 
Kuna hoja za msingi kwenye mada. Ngoja nami nijaribu kwenda hoja kwa hoja.
1: Mfumoko wa bei. Kwanza mleta mada hakuna mahali ameonesha mtiriko wa mfumoko wa bei kwa kipindi cha hata mwaka mmoja. Je takwimu zinaonesha kuwa mfumoko wa bei umepanda ama umeshuka? Pili huwezi kutumia bidhaa moja tu (sukari) ukasema kuwa mfumuko wa bei unaelekea sijui hyperinflation. Je vip kuhusu bei ya unga wa mahindi, mchele, mafuta ya kupikia hivi navyo bei zake zilikuwaje na kwa sasa zikoje? Ni kweli kuwa bidhaa za vyakula zinabeba mchango mkubwa sana kwenye mfumuko wa bei lakini haimaniishi kuwa uchague bidhaa ile tu ambayo unataka na uache zingine. Hata hivyo mfumuko wa bei pia unahusisha bidhaa zisio za chakula kama mafuta ya petroli na dizeli, hivyo tusichague yale tunayotaka tu yasikike hata kama hayana ukweli.

2: BoP. Ni kweli ni muhimu kuuza nje lakini tukumbuke kuwa kuwa na 'deficit c/a' sio kuwa ni kosa. Kwanza kwa nchi zinazoendelea, kununua zaidi kuliko kuuza ni jambo la kawaida kwani nchi zinapaswa kuwa na mitambo, vipuli na zana mbalimbali. Marekani kwa mfano, imekuwa na BoT deficit toka mwaka 1975 hadi sasa na kwa mwaka jana iliuza bidhaa nje zenyethamani ya 2.2 trilion (USD) wakati ilinunua bidhaa kutoka nje zenyethamani ya 2.7(USD). Kununua zaidi kuliko kuuza pia hakumaanishi nchi haiwezi kutengeneza hizo bidhaa humu ndani bali wakati mwingine ni kwa sababu za "comperative advantage" waliyonayo wengine. Swala la msingi hapa linapaswa kuwa kwenye ishu tatu, mosi tunanua bidhaa gani, kwanini tunanua na tunanua kutoka wapi. Kama tunanua bidhaa kama matrekta kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, na tunanunua kutoka kwa wala wanaouza kwa bei nzuri, basi hakuna shida. Marekani licha ya kuwa na trade deficit ya 500 bln (usd), ukweli kuwa sehemu kubwa ya manunuzi ya bidhaa hizo imekwenda kwenye kampuni za kimarekani zilizopo china. Hivyo kwenye GDP yake hizo value hazisomi lakini kwenye GNP yake zinasoma, kitu kinachowasaidia wananchi wake kuwa na pato kubwa.

3: Kuhusu kukopa nje. Kwanza nadhani hii hoja inaenda kinyume na kile alichotaka kusema. Thamani ya fedha ya nchi kama zilivyo bidhaa zingine, huamuliwa na mahitaji yake na upatikanaji wake. Katika muda mfupi. ukopaji wa fedha kwa fedha za kigeni, unaongeza mzunguko na upatakianaji wa fedha za kigeni. Kama nchi inapata mkopo wa dola milioni 500, maana yake ni kuwa kwa muda mfupi mzukungo wa dola utaongezeka. Hata hivyo, kwa kipindi kirefu haswa kama mkopo haukuwekwezwa kwenye uzalishaji, wakati wa mrejesho ndipo kutakuwa na kushuka kwa thamani ya fedha kwani itabidi kulipa dola amabazo kwa wakati huo hazipo. Kwa maelezo haya, hata kama serikali ingekuwa imekopa hizo fedha, bado isingesababisha kuporomoka kwa thamani ya fedha yetu. Hivyo hii hoja kwa sasa haina mashiko, isipokuwa tu kama tutaongelea ulipaji wa madeni ya nyuma.

4:Mazingira ya biashara. Hapa kuna hoja nzuri na ni jambo zito sana katika uwekezaji haswa kwa wageni. Lakini je, hayo mazingira yamebadilika kwa muda gani? Je wawekezaji wameshafunga biashara zao na kuondoka?

5: Matumizi holela ya fedha za kigeni. Hili jambo limeshazungumzwa sana lakini mamlaka husika hazitaki kulifanyia kazi. Ni ukweli kuwa ni lazima watu walazimishi kuitafuta fedha ya ndani. Hii bishara ya ku 'quote' dola kwa shilingi pia ni ya kupiga marufuku. Hata hivyo hizi ni jitahada kwa ajili ya muda mrefu zaidi na sio kwa ajili ya muda mfupi.

6:Hali ya kisiasa. Ni ukweli kuwa kumekuwa na changamoto kubwa sana kwenye ishu za kisiasa. Ili nchi zikue na kuchangia kuimarika kwa fedha ya ndani, 'inclusive economic institutions' ni lazima, na ambazo zinakuwa sapotedi na taasisi imara za kisiasa. Ni muhimu kuwa na sera zinalinda wawekezaji, kuruhusu nguvu ya soko kuamua pamoja na kuwa na mifumo ya wazi ya kushughulikia maswala mbalimbali.

Mwisho:
Ieleweke wazi kuwa thamani ya fedha ya nchi kuwa ndogo kuliko nchi nyingine sio jambo baya haswa kama itatumika vizuri. Kushuka kwa thamani ya fedha ya nchi yetu inapaswa kuwa chachu ya kuuza nje zaidi, kwa kwa dola chache walizo nazo wageni,wanaweza kuapata vitu vingi zaidi kutoka kwetu kuliko thamani yetu kama ingekuwa juu. China inafaidika zaidi na thamani ya fedha yake kuwa chini kuliko ile ya marekani kwa sababu wao wanauwezo wa kuzalisha zaidi. Hivyo kinachotakiwa hapa pamoja na mambo mengine, tuongeze uzalishaji wa bidhaa zainauzwa nje ili tutumie hali ya fedha yetu kuwa na thamani ndogo kama fursa.

Mleta mada ametufanya tufikiri kuhusu thamani ya fedha yetu. Hata hivyo sababu nyingi alizozitaja haziwezi kuwa visababishi vya karibu (immediate cause) bali kwa muda mrefu hna 'solution' zake pia ni za muda mrefu.
Nawasilisha.
Hongera sana na naungana na wewe mkuu.
 
usiangaike na dollar tunajiandaa kujiunga na petro-yuan!
=====
Changamato za kuboresha uchumi zinahitaji mbinu nyingi. China kuna kipindi ili devalue ela yake kama mbinu ya kurahisisha ununuaji wa bidhaa zake soko la kimataifa. Ilifanikiwa sana, mpaka US akalalamika WTO! Kwa mipango yetu ya kuwa na viwanda 100 kila mkoa lazima tuanze na mikakati ya kuuza bidhaa kwenye masoko ya kimataifa. Tuiunge mkono serikali na pale pakuisaidia tuifanye hivyo haraka kimawazo hata kwa mali.
Mbona tumeanza ku devalue mapema sana hata kabla ya viwanda vyenyewe kuanza kujengwa.

Wachina wali devalue pesa yao baada ya kuwa na surplus ya bidhaa sisi hata soko la ndani halijitoshelezi.
 
nahisi ulikua unasoma huku unatembea so hata ulikua huelew sukar ametumia kama mfano mbona bidhaa ziko nyingi tu au ulitaka azitaje zote unga bei unashndana na mchele

biggest cause ya inflation rising price of neccesity commodity ambazo ndo vyakula nahisi ecos 101 ulikua huielew ulimtesa sana mwalimu wako wa macroeconomics
Hivi wanaompinga malisa mbona hawajibu kwa hoja ni porojo tu
 
Fani uliyoisomea ndo mlango wa kujulia fani nyingine, kama umesoma stadi za kazi usiishie tu hapo kwenye kujua stadi za kazi, soma vitu mbali mbali, jifunze bila kuchoka na siyo kutulia tu kwenye fani moja kama chetezo linalosubiri ndoa ya mkeka, inawezekana usijue kila kitu ila jifunze kila kitu pengine upate walao ABC. Heshimu kila wazo la mwingine, Every voice and opinion is worth to be heard.
Who is GJ Malisa and what are his credentials??? Mbona kama anarukia fani za watu?
 
Mkuu mipango tuache kuibeza serikali katika harakati zake za kujenga uchumi. Rais Magufuli watanzania wataamua ifikapo 2020 katika uchaguzi mkuu.

Umenipoteza Mkuu! Niweke wazi usitie mafumbo, jaribu kuwa direct and specific kwenye hoja yako, hususan kuhusiana na analysis ya huu uzi..

Kuibeza serikali vipi yaani... ?2020 Kwa hio sote tupotee sio ? Sasa hapo nani anambeza mwenzake?,

1/10th of my life expectancy will be gone at that stage if I’m lucky to live 60+ unajua life expectancy ya mtanzania ?

I want to be productive when I’m able not on kubana mikanda, then, we all be spiralling down fall to under the ground, if we follow your approach..⚰️ until death to us apart!

Na ile ya wazee wako iliyopotea 50 + years of incompetency, Redicule and you know well tanking to this level ,

Lazima watu waseme, penye mapungufu na serikali by the way isn’t govern on emotions!

Please set aside your emotions try to make sense of what you are saying,

Hoja kwa hoja with backed up facts! Mbona rahisi hicho
 
Who is GJ Malisa and what are his credentials??? Mbona kama anarukia fani za watu?

Kama humjui Malisa basi soma katiba ya nchi inamtambua kwani kwenye ibara ya 18(1) inasema hivi

...Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake...

Kwa sababu Malisa ni mtu basi wewe ni nyani ambaye hutambuliwi na katiba na unadhani kila mmoja ni nyani kama wewe asiyestahili kutoa mawazo yake.
 
Numbers never lie.....ngoja niendelee na safari yangu ya kwenda Zimbambwe
 
Kwa hiyo MCHUMI Malisa anataka kutuaminisha Tanzania inaelekea kwenye 'Hyper inflation? Kasomea uchumi chuo gani?
Kwenye currency, maduka ya kubadilisha fedha bei zikoje? Tsh 2500 za 'Bloomberg' ya Malisa & co, au 2,248?
Vijana wadogo mnajikita kwenye siasa za viwango vya chini mkizeeka lazima muwe wachawi.
Wewe bado unauliza maduka ya kubadilisha fedha bei zikoje wakati tayari exchange rate kwa wanaotuma fedha nchini kutoka ughaibuni ni TZS 2548? Acheni kujitoa ufahamu wakati nchi inaserereka!
 
Back
Top Bottom