Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 39,300
- 25,396
Ndugu zangu Watanzania,
Soma hapa 👉Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania wanaotoa zawadi za fedha taslimu katika sherehe mbalimbali kuacha utaratibu wa kutupa noti na badala yake kutumia mifumo ya malipo ya kidigitali ili kulinda ubora wa fedha zinazotumika Nchini.
Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2026 na Meneja Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania Victoria Msina wakati akizungumza na AyoTV katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea Mkoani Dodoma.
Msina amesema noti na sarafu hutengenezwa kwa gharama kubwa hivyo zinapaswa kutunzwa kwa uangalifu na kuwa kila noti ina namba maalumu ya utambulisho na Benki Kuu hufuatilia muda wake wa matumizi hivyo kitendo cha kuzitupa chini kuzikanyaga au kuzishika kwa mikono yenye jasho na unyevu hupunguza ubora na maisha ya fedha hizo.
Aidha amesema matumizi ya mifumo ya malipo ya kidigitali ni njia salama na ya kisasa ya kutoa zawadi katika sherehe badala ya kutumia fedha taslimu kwa namna inayoweza kuziharibu, pia amefafanua tofauti ya sarafu zinazovutwa na sumaku na zile zisizovutwa akieleza kuwa hali hiyo hutokana na aina ya metali zinazotumika kuzitengeneza.
“Kweli pesa ni ya kwako umetafuta kwa jasho lako lakini kiustaarabu unaweza kutumia njia nyingine mbadala kama kutumia mifumo ya malipo ukaingiza kwenye benki yake halafu ukumbini ukapeleka risiti ya malipo” amesema Msina.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.