Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,746
- 40,899
Niseme nini isipokuwa Bw. Basil Mramba akiwa Waziri wa Fedha aliruhusu Benki Kuu kulipa malipo ya ajabu kwenye makampuni zaidi ya 22 na hivyo kusababisha upotevu wa Shilingi bilioni 133 kama ilivyooneshwa katika ripoti ya Erns & Young.
Bw. Mramba na Mgonja ndio watu wengine wawili ambao Rais angetengua uteuzi wao mara moja. Badala ya wao kusubiri hadi Rais atengue uteuzi huo, kwanini wasiamue kujiuzulu mara moja na kuwajibika kwa vitendo vyao vilivyolinda na kuchochea ufisadi? Kwanini Bw. Mramba na Gray Mgonja hawakuanzisha uchunguzi wowote Benki Kuu licha ya tuhuma za matumizi mabaya kuzagaa kwenye taasisi hiyo kwa miaka nenda rudi?