BoT Saga Unfolding: Basil Mramba ajiuzulu - Wito

BoT Saga Unfolding: Basil Mramba ajiuzulu - Wito

Nyani,

Nitumie msg uulize maswali yako yote ya namna hiyo kwenye PM nitakujibu.

Kwa ufupi watu wamejipanga na kupangika, in the near future uongozi na hatma ya nchi hii kiuchumi na utawala utakuwa unaamuliwa na baadhi ya watu.

Kinachonishangaza hawa jamaa zetu wajiitao "usalama wa Taifa", hivi hawaoni chochote? Uzalendo kweli umewaishia ndugu zangu? au nyie ni wamarekani? Shauri zenu watoto wenu watakapokuwa House boys na hose girls za hao mnaowalinda!

Fisadi Daima

Mkuu

Katika nchi za Kiafrika inawezekana hatuna Usalama wa Taifa, Tuna usalama wa MAFISADI na ndio maana haya mambo yanaweza kufanyika na watu wasikamatwe kabisa.Hivi wako kwa lipi kama nchi inanuka rushwa namna hii? Wanashauri nini watawala? Wanasubiri miaka elfu mbili ndio watwambie?

Haya pia tumeyashuhudia hata Kenya.
 
"Wanausalama" wa nchi hii ni aibu kubwa na mzigo kwa taifa letu. Huwa wanaweza kuamka na kurudi majumbani mwao jioni na kusema kwamba wamefanya kazi waliyoajiriwa kufanya?? Labda inabidi wabadilishiwe training - ile waliyopata na wanayoendelea kupewa ni ya kulinda their masters, na siyo ya kulinda taifa. Wapo kuwalinda wahujumu uchumi wanaojiita eti ni viongozi wa wananchi.
Nchi inakuwa raped waziwazi na hawafanyi chochote !! Ni wazi kuwa kwa kuwa hawachukui hatua zozote basi na wao walikwisha kuwa compromised na ufisadi. Wanatumia nafasi zao na wao kujinufaisha - hivyo nchi hii haina mtetezi!!
 
It is very sad story, while a lot of children in each corner of Tanzania are starving, in the mean time few people are get richer and richer every day.

Kwa nini huyu Basil Mramba hatoki public na kufanunua kuhusu hizi alligations kama kweli au laa? Jee kwa nini Watanzania tunapelekwa ki zumbu kuku kiasi hiki?

Habari nilizopata bila kuzithibithisha ni kwamba bwana Balali sasa hayupo Washington DC tena, bali anaishi Delaware kwenye Condominium ya kigogo mmoja Mtanzania. I can't believe this. Wakati huo huo muheshimiwa JK yupo yupo tuuu, huku viongozi wake wa ngazi za juu wanaficha kutoa maelezo ya Balali na hali yake.

Ni kumbukumbu yangu kwamba JK aliaidi kuwaumbua viongozi wazembe na wala rushwa. Sasa umbuaji huo uko wapi? Naamini mapigano haya yatafanikiwa kwa kutumia wino na karatasi, na pindi itakapo shindikana basi mbinu mbadala zitatumika.

Upinzania inabidi uaandae grassroot movement kwa election za 2010, na hii itafananikiwa kama vyama vyote vya upinzani vilivyounga vitatumia njia sahihi ya kuchagua candidate wa kusimama 2010. Si zungumziii kuanza kampeni, bali kumuandaa mgombea mapema kadri iwezekanavyo ni mbinu muhimu sana 2010 election.

Kama tutachukua bunge kama Kenya, then haya mambo yatafika mwisho.
 
Hivi ngoja niulize: inakuwakuwaje kikundi kidogo cha watu ukilinganisha na raia wote kwa ujumla kinakuwa na madaraka na uwezo wa kufanya chochote kipendacho halafu sisi tulio wengi tunakaa na kulia lia tu bila kufanya kweli? Hii inawezekanaje?

Ni kwamba sisi hamnazo, wote tunaopiga kelele humu tungekuwa Dar uitishe maandamano uone kama ungeona mtu, wangekuja wamachinga tu. Lakini bora tuendelee tu na makelele haya yanasaidia sana kutoa ma-frustration yetu hasa ukisikia wanayasoma hao mafisadi.
 
Huyu Mramba ni mzizi mnene. Katika hali ya kawaida, usingetarajia Rais amteue kwenye baraza la mawaziri mtu ambaye alishawaambia watanzania wale nyasi. Sisi wengine tulipoona yumo kwenye baraza la JK tulilegea na ndio maana hatujawahi kuwa na matumaini na serikali hii.

Haya wewe utakubalije, kama kweli una nia njema, uendelee kukaa na watu kwenye baraza lako la mawaziri ambao karibu wote wametuhumiwa kula hela za wananchi na nchi kwa ujumla, watu ambao wakipita barabarani watu wanakunja nyuso badala ya kutabasamu?
 
Neno moja tu niseme hapa maana kila tusemacho tunarudia tu . JF ni moto sana .Moto unawanyima usingizi maana wanajua slowly haya yataweza mkuwafikia wananchi wa kawaida na yatafika kweli . CCM wako taabani ukiona wanawaita watu kama akina Gwandumi basi ujue wako taabani kabisa .
 
I love your courage mdada wa Kiafrika .Hoji unayo haki .Mramba yule mtu sijui namna gani .

A pauper from Mashati, Rombo.A hard working honest Tanzanian when he was the Director of SIDO in the 80's.A church going Catholic that Mwalimu took a liking to for the above reasons.
Lost his first attempt at becoming a Mbunge in 85 to the Chadema candidate;thereafter nominated,appointed to the cabinate and soon became more corrupt than does before him.

The Bot money is what built this grand hotel in Arusha called KIBO PALACE HOTEL. Enough said
 
Vyombo vya habari vimebaini kuwa Mkurugenzi wa kampuni inayohakiki makampuni yanayochimba dhahabu Alex Stewarts Assayers ni mtoto wa Mhe. Basil Pesambili Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati kampuni hiyo ilpopata mkataba huo Juni 2003. Katika miaka miwili ya mkataba huo, kampuni hii imekuwa inalipwa dola 751,267 sawa na sh. 939 millioni kila mwezi. Kwa muda wa miaka miwili imejikusanyia dola milioni 18 sawa na sh. 22.5 bilioni. Kampuni hii pia ilisamehewa kodi kwa notisi za serikali za Novemba 25 2005 iliyotiwa saini na aliyekuwa Waziri wa Fedha. Ni wazi kuna mgongano wa manufaa (conflict of interest) ya Waziri wa fedha kuipa mkataba kampuni ambayo mtoto wake ni mkurugenzi na pia kuisamehe kodi. Mpaka hivi sasa serikali haijatoa maelezo ya kina kufafanua utata huu ambao unaashiria matumizi mabaya ya madaraka kunufaisha familia yako ambayo ni rushwa. Rais anawajibika kulichunguza suala hili kwa kina na ikiwa taarifa ambazo zimeandikwa katika vyombo vya habari na vielelezo vyake zina chembe ya ukweli, basi waziri awajibishwe kwa kufukuzwa kazi na Tume ya Kuzuia Rushwa ichukue hatua za kisheria kuwafikisha wahusika mahakamani.

Kutoka: http://cuf-tz.com/666.html

Hii habari inaongeza machungu ya 2008, UKWELI UTABAKIA KUWA DAWA YA UJINGA WA VIONGOZI WETU NI KUWATOA MADARAKANI NA KUWAPA WATU WENYE NIA YA KUTUONGOZA KWA UKWELI, hii ni kwa sababu kuna watu walioko kwenye mtandao wa sasa ambao hawawezi kuwajibishana kwa kuwa na wao wamekula kwa namna moja au nyingine 'KWA NINI WATANZANIA TUSIAMUE KWA KAULI MOJA' KWAMBA TUWEKE WATU WAPYA NA KUITOKOMEZA CCM MBALI. KWA KUFANYA HIVYO NI RAHISI KUWAPA MASHARTI NA KUWAFUNDA VIONGOZI WAPYA KULIKO HAWA MATAJIRI NA WACHEZA DILI WAKUBWA.
 
Hivi ngoja niulize: inakuwakuwaje kikundi kidogo cha watu ukilinganisha na raia wote kwa ujumla kinakuwa na madaraka na uwezo wa kufanya chochote kipendacho halafu sisi tulio wengi tunakaa na kulia lia tu bila kufanya kweli? Hii inawezekanaje?

This is a $133million question🙁 Tunahitaji wakenya watufunze jinsi ya kuandamana!!
 
DUH TUNAELEKEA WAPI JAMANI NCHI IMEJAA MAFISADI KILA ANAYETAJWA NA AKINA SLAA IKIMFUATILIA NI KWELI KALA HELA KIBAO.HIVI RAIS ANASUBIRI NINI KUWAFIRE HAWA WATU MRAMBA NA WENZAKE WOTE,tENA NASIKITIKA LEO NIMEONA MAGAZETINI ASUBUHI MEGHJI ANATHUBUTU KUTANGAZA HAWEZI KUJIUZULU NG'O.KWAN HIYO NAFASI ILIUMBWA KWA AJILI YAKE HEBU ATOKE
 
"Wanausalama" wa nchi hii ni aibu kubwa na mzigo kwa taifa letu. Huwa wanaweza kuamka na kurudi majumbani mwao jioni na kusema kwamba wamefanya kazi waliyoajiriwa kufanya?? Labda inabidi wabadilishiwe training - ile waliyopata na wanayoendelea kupewa ni ya kulinda their masters, na siyo ya kulinda taifa. Wapo kuwalinda wahujumu uchumi wanaojiita eti ni viongozi wa wananchi.
Nchi inakuwa raped waziwazi na hawafanyi chochote !! Ni wazi kuwa kwa kuwa hawachukui hatua zozote basi na wao walikwisha kuwa compromised na ufisadi. Wanatumia nafasi zao na wao kujinufaisha - hivyo nchi hii haina mtetezi!!
duh mi sijui kama kweli hizo pesa zilikuwa za usalama wa nchi kama tunavyodanganywa wadanganyika
 
Wakuu mi naomba turudi kwenye tamko la sirikali kuona nani yupo responsible hapa:-

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU KATIKA AKAUNTI YA MALIPO YA MADENI YA NJE (EXTERNAL PAYMENT ARREARS ACCOUNT – EPA) ILIYOKO BENKI KUU YA TANZANIA

Nafurahi kuwaarifu kuwa, kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje yaani External Payment Arrears (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania imekamilika. Kazi hiyo ilifanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Ilianza Septemba, 2007 na kukamilika Desemba, 2007. Juzi tarehe 07 Januari, 2008 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Rais ameisoma, ameifanyia kazi na kuitolea maamuzi.

Historia ya EPA

Katika miaka ya 1970 mpaka 1990 nchi yetu ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa fedha za kigeni. Benki Kuu ya Tanzania ilipewa jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za kigeni kwa niaba ya Serikali. Benki Kuu ndiyo iliyokuwa na mamlaka ya kupanga na kuamua nani agawiwe fedha za kigeni na kiasi gani!

Kwa ajili ya kuwahudumia wafanyabiashara, mashirika na makampuni yanayoagiza bidhaa na huduma kutoka nje, Akaunti maalum ilifunguliwa katika Benki ya Taifa ya Biashara kwa wakati huo. Akaunti hiyo ilijulikana kwa jina la External Payment Arrears (EPA) au Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje, kwa tafsiri ya Kiswahili.

Waagizaji wa bidhaa au huduma kutoka nje waliwajibika kulipa kwenye Akaunti hiyo, fedha ya Tanzania yenye thamani inayolingana na fedha za kigeni zinazotakiwa kulipia bidhaa au huduma hiyo huko nje. Baada ya waagizaji wa ndani kufanya hivyo, kutegemeana na upatikanaji wa fedha za kigeni, wauzaji au watoaji huduma wa nje walilipwa. Benki Kuu iliamua nani alipwe na Benki ya Biashara ilifanya malipo.

Juni, 1985 iliamuliwa kuwa shughuli za akaunti hiyo zihamishiwe Benki Kuu kutoka Benki ya Taifa ya Biashara na zimeendelea kuwepo hapo mpaka sasa. Katika Benki Kuu kikaundwa kitengo maalum cha kusimamia na kuendesha shughuli za akaunti hiyo kilichojulikana kama Debt Management Unit chini ya Kurugenzi ya Sera (Directorate of Economic Policy).

Kwa sababu ya tatizo la upungufu wa fedha za kigeni kuendelea, malimbikizo ya madeni hayo yalizidi kukua mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 1999 deni hilo lilifikia dola za Kimarekani 623 milioni. Kati ya fedha hizo, dola 325 milioni ndilo deni la msingi na dola 298 milioni ni riba yake. Baadae likaongezeka kufikia dola 677 milioni.

Juhudi za Kulipa Madeni

Juhudi za kulipa malimbikizo ya madeni hayo ziliendelea kadri fedha za kigeni zilipopatikana. Kwa nia ya kutaka kutafutia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na kupunguza mzigo wa madeni, Serikali ilianza kutafuta njia nyingine mbalimbali. Mwaka 1994, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ilianzisha Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme). Yaani waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya madeni wanayodai. Wapo wadai kadhaa walikubali na madeni yao yakauzwa chini ya mpango huo. Taarifa za mwaka 2004 zinaonyesha kuwa madeni ya thamani ya dola 228 milioni yalilipwa chini ya mpango huu.
Pili, Serikali ilifanya juhudi ya kupata msamaha wa madeni hayo kutoka nchi wanachama wa Paris Club. Serikali iliomba kuwa pamoja na kutusamehe madeni ya kiserikali toka nchi zao wasaidie tusamehe na madeni ya makampuni yao kwetu. Yapo pia madeni ambayo yamelipwa na makampuni ya Bima baada ya makampuni yaliyouza bidhaa na huduma Tanzania kushindwa kulipwa. Madeni ya dola 216 milioni yalihusika chini ya michakato hii. Hivyo basi, deni la dola 444 milioni lilipungua katika ile jumla ya dola 677 milioni. Kwa hiyo mwaka 2004 deni katika Akaunti ya Malipo ya Nje lilikuwa dola 233 milioni. Yalikuwepo mawazo ya baadhi ya watu kuwa pengine deni hilo lisilipwe au tulikatae. Walikuwepo waliokubali madeni yao yafutwe na wengine waliagiza fedha zao zipewe NGO. Lakini, baadhi ya wadai waliendelea kudai na wengine hata kushitaki mahakamani. Hivyo BoT ililazimika kuendelea kulipa kadri wadai walipojitokeza.

Ulipaji kwa Idhini

Katika utaratibu wa malipo ya madeni ya EPA kanuni zinaruhusu mdai kuamua deni lake kulipwa kwa mtu au kampuni nyingine. Kanuni zinamtaka mdai kutoa hati iliyothibitika kisheria ya yeye kuidhinisha malipo hayo yafanywe (Notarised Deeds of Assignments) hivyo. Pia yapo masharti ya kutimizwa na kampuni au mtu aliyeidhinishwa kulipwa hilo deni. Utaratibu umetumika kufanya malipo kadhaa ya madeni katika Akaunti ya EPA.

Matatizo ya Mwaka 2005/6

Katika ukaguzi wa Hesabu za BoT za mwaka wa fedha 2005/6, Agosti, 2005 kuligundulika matatizo katika ulipaji wa madeni kwa utaratibu wa idhini ya kulipwa wakala wa mdai katika akaunti ya EPA. Kukajitokeza kutokuelewana kati ya Benki Kuu na Mkaguzi Deloitte and Touche' aliyegundua tatizo hilo. Baadaye mkaguzi huyo alisitishwa kuendelea na kazi. Serikali ikaingilia kati na tarehe o4 Desemba, 2006 ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa akaunti hiyo unafanyika kwa kina. Aidha, ilimuagiza atafute kampuni ya kimataifa ya ukaguzi ifanye kazi hiyo kwa niaba yake. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali, ndiye kwa mujibu wa Sheria ya BoT mkaguzi wa Hesabu za Benki Kuu. Hata hivyo kwa mazingira hayo maalum Serikali ilimtaka CAG atafute mkaguzi mwingine wa nje.



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifanya hivyo na matokeo ya mchakato wa kutafuta kampuni hiyo uliochukua miezi mitano (Januari hadi Mei, 2007) ndipo ikapatikana kampuni ya Ernst and Young.
UKAGUZI

Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young wakaanza kazi hiyo Septemba, 2007 na kuikamilisha Desemba, 2007. Wakaguzi hao wamefanya kazi nzuri iliyothibitisha kiwango cha juu cha weledi (Professionalism) cha wakaguzi hao. Tunawapongeza, tunawashukuru. Tunatambua kuwa walipata matatizo mengi hasa ya kupata taarifa zilizo sahihi kwa sababu ya matatizo ya utunzaji wa kumbukumbu. Madeni haya ni ya miaka 27 na zaidi iliyopita. Kumbukumbu zimehamishwa kutoka NBC kwenda BoT. Hata huko NBC shughuli zilikuwa zinafanywa katika matawi mbalimbali nchini tena miaka hiyo hapakuwa na kompyuta hivyo kumbukumbu zote ziliwekwa kwenye majalada. Pamoja na matatizo hayo ukaguzi wa hesabu za mwaka 2005/6 ulikamilika kwa kiwango cha kuridhisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ukaguzi katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 uliochunguzwa, katika mwaka 2005 yalifanywa malipo ya jumla ya Shilingi 133,015,186,220.74 kwa Makampuni 22 ya hapa nchini. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania, Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd., G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KARNEL Ltd.

Aidha, ukaguzi umebaini kwamba kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa makampuni kumi na tatu (13) ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi. Hivyo, Makampuni hayo hayakustahili kulipwa chochote. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania, Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd.

Aidha, ukaguzi umeendelea kubaini kuwa Makampuni tisa (9) ambayo yalilipwa jumla ya Shilingi 42,656,107,417.00 hayakuwa na nyaraka za kuonyesha stahili ya malipo na hivyo kuwafanya wakaguzi washindwe kuhakiki uhalali wa malipo hayo. Makampuni hayo ni: G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KERNEL Ltd.

Wakati huo huo Makampuni mawili, yaani, Rashtas (T) Ltd na G&T International Ltd., kumbukumbu zake za usajili katika daftari la Msajili wa Makampuni nchini hazikuweza kupatikana.

Uamuzi wa Rais

Baada ya kuipitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na ya Mkaguzi wa Nje, yaani, Kampuni ya Ernst and Young, Mhe. Rais amesikitishwa na kukasirishwa na taarifa ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu. Kwa hiyo, ameamua kuwa hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya makampuni na watu waliohusika na vitendo hivyo viovu.

Kwa ajili hiyo Rais ameamua yafuatayo:-

1. Ametengua uteuzi wa Dkt. Daudi A. Balali kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

2. Ameagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa.

3. Shughuli za ulipaji wa madeni katika Akaunti ya EPA zisimamishwe mara moja mpaka hapo taratibu za uhakiki na utaratibu mpya utakapotengenezwa.

4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huu. Rais amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita. Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa kazi hii. Amewataka wahakikishe kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.

5. Rais pia amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kushirikiana na kuwasaidia watendaji wakuu hao wa vyombo vya dola katika kufanikisha jukumu lao hilo. "Watu wengine wenye taarifa za ziada pia wazitoe kwa Timu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wenzake".

6. Kutokana na hatua ya kutengua uteuzi wa Bwana BALALI, Mhe. Rais amemteua Prof. BENNO T. NDULU (Naibu Gavana) kuwa Gavana Mpya wa Benki Kuu. Halikadhalika, amemteua Dkt. ENOS S. BUKUKU (Katibu Mkuu – Miundombinu) kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu (Fedha na Uchumi). Pia amemteua Ndugu Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu. Uteuzi huu unaanza mara moja.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI

IKULU,
DAR ES SALAAM
09 Januari 2008
Source:http://www.kforumonline.com/viewtopic.php?p=1737

Mtizamo wangu ni kama ifuatavyo:-

Serikali ilitoa Standing Order kwa BOT kulipa madeni ya EPA kadri fedha za kigeni zinavyopatikana.Unatoa standing order inaamisha kuwa benki inatekeleza tu haina haja ya kuconsult serikali(Pay Master General wala Waziri).Kwahiyo sioni sababu ya kuwaingiza Mhe Mramba na Mgonja(in his capacity kama Paymaster General).Kama responsibility ilipewa BOT then the BOT Board of Directors(hapa Mgonja yupo na sio Balali peke yake),Director of Economic Policy na watu wa kitengo cha Debt Management Unit. Hawa ndio wako direct responsible.Kwa jinsi hii summary inaonyesha kilichotokea ni Clear Fraud kati ya BOT na waliolipwa.Mimi pia ningependa sana either Mramba au Megji wajiuzulu lakini sidhani kama wako directly responsible.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ndio mwenye jukuma la ku audit BOT, je kwa nini hakufanya hivyo yeye mwenyewe?Kama hakuwa hana uwezo(Technical Competence) wa kufanya hivyo, je ni kwa nini alikubali Delloite(CAG Agent)akubali kufukuzwa(kukatokea kutoelewa!!!!!! na BOT. Kwani Delloitte walipewa kazi na Board ya BOT au CAG?
CAG naye yuko responsible kwa kushinda kualert of a possible serious Audit breach on time.

Haya yalikuwa ni madeni ya muda mrefu mno inakuwaje BOT na Serikali kukubali kulipa kwa idhini(through Notarized Deeds of Assigmment). Huitaji kwenda shule kujua hii ndio ilikuwa loophole ya kuzitoa hizi fedha maana zilishakuwa unclaimed kwa muda mrefu na hata hao genuine wadai waliisha yafutilia mbali hayo madeni.Toka 1970 hujalipwa, huwezi kuendelea kuweka kwenye vitabu vyako.Haya makampuni 22(nina huakika hizi kampuni zote zilisajiliwa after 2004), yalitoa records hizi za madeni yaliyokufa hapo hapo BOT, wakaingia Samora, wakatengeneza letter head na deed of assignement, malawyer of Malegesi Calibre waka notarised hela ikatoka.Simple kama kumsukuma mlevi.

Roho inauma sana jamani.
 
Mramba awa bubu

na Irene Mark

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha wakati ukifanyika ubadhirifu wa mamilioni ya shilingi kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Basil Mramba, amekataa kuzungumza lolote kuhusu sakata hilo.
Mramba ambaye hivi sasa ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, alikataa kueleza lolote kuhusu suala hilo ambalo Jumatano ya wiki iliyopita lilisababisha aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali apoteze wadhifa wake huo.

“Tafadhili, naomba unisamehe. Sipo kwenye nafasi ya kuzungumzia suala hilo. Kama ni ile EPA ya Economic Partnership Agreement nitasema, lakini siyo hiyo,” alisema Mramba.

Wakati Mramba akipata kigugumizi kuzungumzia suala hilo, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kwa upande wake amesema hana wasiwasi wowote kuhusu hatima yake katika suala hilo.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Waziri Meghji alieleza kushangazwa na watu wanaomhusisha na tuhuma hizo, huku wakijua kuwa hausiki nazo kwa namna yoyote.

Waziri Meghji alisema anatambua vyema kwamba, uamuzi wake wa kuwanyima baadhi ya watu misamaha ya kodi, ikiwa ni pamoja na hatua nyingine za kiudhibiti alizozichukua, ni sehemu ya mambo iliyomjengea maadui ambao sasa wanataka kuitumia kashfa ya EPA kumtaka awajibike.

“Sina wasiwasi, niko imara kwa kuwa natambua kwamba sijatenda kosa lolote katika sakata hili zima… najua kuna watu ambao wanafanya mambo haya kwa sababu tu ya maamuzi niliyochukua ya kuwanyima exemptions (misamaha ya kodi),” alisema Meghji.

Barua za Wizara ya Fedha ambazo Tanzania Daima imeziona zinaonyesha kuwa, Septemba 15 mwaka 2006, Waziri Meghji aliandika barua kwenda kwa kampuni ya ukaguzi wa kimataifa iliyokuwa ikikagua mahesabu ya BoT ya Deloitte & Touche akitetea malipo ya dola za Marekani 30,732,658.82 kwenda kampuni ya Kagoda Agriculture ambayo sasa inahusishwa na ubadhirifu kupitia kashfa hiyo ya EPA.

Katika barua hiyo, Meghji amekaririwa akisema kwamba fedha hizo zilikuwa zimetolewa kwa matumizi maalum ya siri kwa idhini ya serikali na akawataka wakaguzi hao kutambua kuwa suala hilo lilifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi.

Hata hivyo, barua nyingine inaonyesha kuwa, siku nne baada ya kuandika barua hiyo (yaani Septemba 19, 2006), Waziri Meghji alibadili uamuzi huo na akaiandikia kampuni hiyo ya ukaguzi barua nyingine ya kufuta barua yake ya awali.

Meghji katika barua yake hiyo ya pili anakaririwa akisema kwamba, barua yake ya kwanza ilikuwa imeandaliwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali ambaye kimsingi ndiye aliyempa ushauri wa kuiandika ile ya kwanza.

Katika barua yake hiyo ya pili, Meghji aliandika kwamba, alikuwa amelazimika kuifuta barua yake ya awali baada ya kutambua kuwa, malipo hayo kwa Kagoda Agriculture hayakuwa sahihi kwa taratibu za kiserikali.

Meghji alieleza kushangazwa kwake na kuibuka kwa mjadala katika intaneti, ambao umekuwa ukimhusisha na sakata hilo la EPA ilhali ikijulikana bayana kwamba matukio yaliyobainisha kupotea kwa shilingi bilioni 133 yalitokea wakati yeye akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

“Mimi nashangazwa sana na mjadala huu unaopinduliwa hivi sasa. Watu wanaijadili kashfa hii kama vile mimi ndiye nilikuwa Waziri wa Fedha mwaka 2005 wakati hayo yakitokea,” alisema Meghji kwa uchungu.

Waziri Meghji alisema pia kwamba, yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuamuru kufanyika kwa uchunguzi katika akaunti hiyo ya EPA, Desemba 4, 2006 miezi kadhaa kabla suala hilo halijafika kabisa bungeni.

Wakati sakata hilo likiendelea, imebainika kwamba, Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyopo sasa hivi watamaliza muda wao Jumamosi ya wiki hii na hivyo kutoa fursa kwa bodi mpya kuanza kazi.

Taarifa ya BoT kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana inaeleza kwamba, bodi hiyo mpya inayoanza kazi Jumatatu ya wiki ijayo baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Fedha, chini ya uenyekiti wa Gavana mpya, Profesa Benno Ndulu, imeshajipanga kwa ajili ya kuanza kutekeleza kazi iliyopewa na Rais Jakaya Kikwete ya kukutana na kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wa BoT walio chini ya mamlaka yake, ambao walihusika kwa namna moja au nyingine katika sakata la EPA.

Wakurugenzi wa bodi hiyo iliyoundwa Novemba 2007 ni, Profesa Ndulu ambaye ni Mwenyekiti na Gavana, Dk. Enos Bukuku, Juma Reli na Lila Mkila.

Wengine ni Profesa Haidari Amani, Ali Mufuruki, Dk. Natu Mwamba, na mwingine atakayetoka Zanzibar, ambaye bado hajateuliwa.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kutoka Jamhuri ya Muungano na Katibu Mkuu Hazina kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao wote wanaingia kwa nyadhifa zao.

Mjumbe wa mwisho wa bodi hiyo ni Bosco Kimela, ambaye ndiye anakuwa Kaimu Katibu wa Bodi.

Taarifa hiyo ya BoT imesema kwamba, mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa, Gavana Ndulu ataitisha mkutano mara moja na kuanza kuyafanyia kazi maelekezo ya rais kwa bodi hiyo kufuatilia kashfa ya EPA.

Tuhuma za ufisadi na ubadhirifu wa BoT zilitolewa hadharani kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2007/08 na baadaye akapanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kulichunguza suala hilo.

Katika tuhuma hizo, Dk. Slaa alinukuu taarifa kadhaa kutoka katika mtandao wa intaneti zilizokariri baadhi ya majina ya watu, akiwamo Ballali na akaorodhesha jinsi ambavyo wamekuwa wakihujumu fedha za umma kupitia BoT. Hata hivyo, kwa nyakati tofauti hoja hizo za Slaa zilionekana kutiliwa shaka na viongozi kadhaa wa juu serikalini.

Hata hivyo, siku chache baadaye, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kwa nyakati tofauti walikiri kuwa serikali ilikuwa na taarifa kuhusu tuhuma katika akaunti ya EPA na wakaahidi kuwa tayari serikali ilikuwa imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuitafuta kampuni ya kimataifa ya ukaguzi kuzifanyia kazi.

Kwa upande wake, wakati kikao hicho cha bajeti kikiendelea, Lowassa, alikaririwa akisema kuwa tuhuma hizo zinashtua na kuwa serikali ilikuwa inazifanyia kazi kwa umakini.

Kana kwamba haitoshi, Septemba 15 mwaka jana, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga Temeke, Dar es Salaam, Dk. Slaa alitaja orodha ya majina 11 ya viongozi kadhaa wa serikali, akiwatuhumu kwa ufisadi likiwamo jina la Ballali.

Kuundwa kwa EPA kulitokana na upungufu wa fedha za kigeni serikalini kati ya miaka ya 1970 na 1990 hivyo, BoT ilipewa jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za kigeni kwa niaba ya serikali.

Kabla ya jukumu hilo kukabidhiwa rasmi BoT, kazi za EPA zilifanywa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC). Lakini, Juni 1998 iliamuliwa kuwa zifanywe na BoT.




 
It is funny to say Mr president is sorrounded by corrupt Ministers, and forget it is him who chose them to be where they are!

it is also funny to say "he has to go" and not being brought to justice!
 
It is funny to say Mr president is sorrounded by corrupt Ministers, and forget it is him who chose them to be where they are!

it is also funny to say "he has to go" and not being brought to justice!

We're conveniently forgeting that Slaa's list also mentioned him as a FISADI.
 
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU KATIKA AKAUNTI YA MALIPO YA MADENI YA NJE (EXTERNAL PAYMENT ARREARS ACCOUNT – EPA) ILIYOKO BENKI KUU YA TANZANIA

....Serikali ikaingilia kati na tarehe o4 Desemba, 2006 ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa akaunti hiyo unafanyika kwa kina. Aidha, ilimuagiza atafute kampuni ya kimataifa ya ukaguzi ifanye kazi hiyo kwa niaba yake. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali, ndiye kwa mujibu wa Sheria ya BoT mkaguzi wa Hesabu za Benki Kuu. Hata hivyo kwa mazingira hayo maalum Serikali ilimtaka CAG atafute mkaguzi mwingine wa nje.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifanya hivyo na matokeo ya mchakato wa kutafuta kampuni hiyo uliochukua miezi mitano (Januari hadi Mei, 2007) ndipo ikapatikana kampuni ya Ernst and Young.

kwanini hiki kilichofanywa na Meghji watu hawataki kutambua na kuappreciate? Siyo tu alibadili uamuzi wake awali bali aliagiza hayo yote hapo juu.
 
Mwanakijiji,
..Nilitegemea ungemuuliza Waziri Meghji kuhusu involvement ya Mgonja ktk EPA na kwanini hajiuzulu? Kwanini hukufanya hivyo?
 
kwanini hiki kilichofanywa na Meghji watu hawataki kutambua na kuappreciate? Siyo tu alibadili uamuzi wake awali bali aliagiza hayo yote hapo juu.

Mama Zk, kilimponza kupingana na hoja ya Slaa kiwazi wazi! Yeye pale angesema kweli shida ipo na tunaishughulikia badala ya kuungana na Balali, Six and the compony kusema tuhuma ni za uongo wakati alijua ni za kweli!
 
Back
Top Bottom