BOT: Bei ya mahindi imepanda mara mbili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Wakati raia wakiendelea kulalama juu ya kupanda kwa bei ya nafaka, wakulima na wafanyabiashara huenda wakawa miongoni mwa watu walionufaika zaidi na zao la mahindi baada ya bei ya jumla ya zao hilo kupanda zaidi ya mara mbili ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Ripoti ya Mapitio ya Uchumi ya Agosti 2022 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa bei ya jumla ya gunia la kilo 100 la mahindi kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2022 ilikuwa Sh 87,383 ikipanda kutoka Sh 43,371 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka jana.

Hiyo ikiwa ni sawa na kusema kwamba, wakulima na wafanyabiashara wameweka mfukoni Sh44,012 zaidi kwa kila gunia moja au sawa na kusema bei hiyo ya mahindi imeongezeka zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na bei ya mwaka jana, huku ripoti hiyo ikieleza kuwa kupanda kwa bei ya mahindi kumechangiwa na kuongezeka kwa mahitaji ya zao hilo, hasa nje ya nchi na kutokuwepo kwa mvua za kutosha katika msimu huu, jambo lililosababisha wakulima kupata mazao kidogo.

Ongezeko ya mazao mengine ndani ya kipindi hicho kwa gunia moja: Mchele (Tsh. 67,365), Maharage (Tsh. 21,047), Mtama (Tsh. 26,184)

“Kuongezeka kwa bei kumechangiwa na mahitaji makubwa ya nchi jirani na kushuka kwa mavuno kutokana na mvua chache,” imeeleza BoT katika ripoti hiyo.
 
Wakulima na walimu wa shule za msingi ni miongoni mwa watu waliopitia nyakati ngumu sana toka uhuru wa nchi hii..

Analima kwa shida, anauza kwa kupangiwa bei. Ni bora sasa wapumue kidogo.
 
Wakati raia wakiendelea kulalama juu ya kupanda kwa bei ya nafaka, wakulima na wafanyabiashara huenda wakawa miongoni mwa watu walionufaika zaidi na zao la mahindi baada ya bei ya jumla ya zao hilo kupanda zaidi ya mara mbili ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Ripoti ya Mapitio ya Uchumi ya Agosti 2022 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa bei ya jumla ya gunia la kilo 100 la mahindi kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2022 ilikuwa Sh 87,383 ikipanda kutoka Sh 43,371 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka jana.

Hiyo ikiwa ni sawa na kusema kwamba, wakulima na wafanyabiashara wameweka mfukoni Sh44,012 zaidi kwa kila gunia moja au sawa na kusema bei hiyo ya mahindi imeongezeka zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na bei ya mwaka jana, huku ripoti hiyo ikieleza kuwa kupanda kwa bei ya mahindi kumechangiwa na kuongezeka kwa mahitaji ya zao hilo, hasa nje ya nchi na kutokuwepo kwa mvua za kutosha katika msimu huu, jambo lililosababisha wakulima kupata mazao kidogo.

Ongezeko ya mazao mengine ndani ya kipindi hicho kwa gunia moja: Mchele (Tsh. 67,365), Maharage (Tsh. 21,047), Mtama (Tsh. 26,184)

“Kuongezeka kwa bei kumechangiwa na mahitaji makubwa ya nchi jirani na kushuka kwa mavuno kutokana na mvua chache,” imeeleza BoT katika ripoti hiyo.
Kwahiyo wao kama taasis kubwa wamechukua hatua gani?
 
Ndio wanashtuka sashivi? mbona bidhaa zimepanda bei kitaaambo kabisa wakati watu wanalalamika wao wako kimyaaa na yule leprofesseeri wao mlevi hadi anajikojolea, nchi inapitia wakati mgumu sana na wala hakuna anayejali mamayao anakula mimate tu ya mmakonde kule maputo, hili nalo ni janga kubwa.
 
safi sana qyvmamaqe mpaka akili ikae sawa

mama yuko maputo ananywisha watu juisi
 
Tulio mjini ni muda wa kujianda kurudi kwa Babu na Bibi kuandaa mashamba maana jembe halimtupi mkulima

Hivi sera ya "kilimo kwanza iliishia wapi wakuu"?
Siku Watanzania hasa viongozi tukiwa sirias nchi itaendelea, na itaachana na ishu za tozo za mitandao ya simu + benki

Hiyo sera ya kilimo kwanza ndio ilikuwa mkombozi.

Uzuri wa Tanzania hata hali ya hewa iwe vibaya vipi, lakini mvua zitanyesha hata kidogo. Tatizo kukosa utekelezaji wa mipango ya kilimo.

Kilimo kinaweza kuitoa kimasomaso Tanzania, ila sapoti ya serikali ni muhimu sana!
 
Back
Top Bottom