Kwa hivyo Kwamanda Bageni aliuwa peke yake na alijipa amri yeye mwenyewe?
Ile kesi kichekesho na aibu kwa wapelelezi (wachunguzi). Majaji waliotoa hukumu hawana kosa walifanya uamuzi(hukumu) kutokana na kilicho wasilishwa na wapelelezi.
Upelelezi wa hovyo, wa mchongo.
Wapelelezi ni polisi walio wachunguza polisi wenzao.
Sasa wale Askari waliotuhumiwa ni wa ngazi za kati na chini.
Askari polisi gani atamchunguza IGP au CDF?
Nani atamchunguza aliyempa IGP amri au kazi ya kutangaza Ile curfew ya October 29, 2025?
IGP ndiye aliyetoa tangazo la amri ya kutoka nje baada ya saa 12 jioni.
Na baada ya amri hiyo ndipo mauaji yalianza kuongezeka kwa kasi.
Mambo mengine mnataka kutuletea matatizo tu tukihoji, mtuteke na kutupoteza.
Bora mnyamaze labda tutasahau.