Bongo movies...

jambazi lazima livae koti la mvua au suti na miwani,Dar na jua lote hili?afu linashika kibastola cha watoto,kinalia kama ubao umeangushwa paaa!

Hahahaa haaaa uwiii jamani nimecheka
my ribs
 
Bunduki kubwa na ndogo (bastola) zote zina milio inayofanana.
 
Wanagombana masaa kibao mtu kaelekezewa bastola kichwani. Kisha unasikia 'paaa' ..kisha unaona jeraha mguuni na mtu kafa.
 
1. Dj anapiga nyimbo ya Celine Dion usiku club...anapiga nyimbo moja alafu nayeye anashuka kucheza
2. Mdada kaamka asubuhi home ana cosmetics na kimini anapika chai
3. Muvi inatengenezwa saa 48
4. ...muvi nzima Ina eneo zaidi ya moja,mpaka inaisha kuna watu Sita tu.
5. Muvi nzima tunaona ndani tu,nje mwisho kwenye geti
6. Jela zina nondo kama geti la uswahilini
7. Sound quality noma mpaka watu wanaopita nje unawasikia (muvi ndani)...wakiwa baharini ndio utapenda.
8. Kingereza "ayu cleize?"
 
Mtu mgonjwa ambaye anatoa wosia kabla ya kukaya roho sauti yake kavuu. Na akifa anapeleka kichwa upande kwa nguvu.
 
Vivuli vya camera, camera man na boom mic kuonekana mara nyengine ata sauti za watu pembeni husikika mfano chumbani wapo wawili tu ila utasikia geuka mbele ili sura yako ionekane vizuri
 
Mimi huwa nachoka tafsiri ya kiingereza. Yaani kiingereza ni kibovu ni aibu tupu. Si kwamba hatuna wataalamu wa kufanya kazi hiyo, bali ni haraka ya waandaaji, mtu mmoja kufanya kazi zaidi ya 10 katika uaandaji hicho wanachoita wao filamu (ingawa hazina sifa ya kuitwa filamu) na kutotumia wataalamu wa lugha ingawa tunao kibao! Ndipo utakuta wanatafsiri hata kicheko na kilio vitu ambavyo mtazamaji anaona kabisa kuwa mtu au watu wanalia au kucheka lakini wao utaona wanaandika "crying" au "laughing"
 
Hahahaha, ni kama Mulugo alivyosema 'dear lookers' badala ya 'dear viewers'
Mzee wa visiwa vya Zimbabwe huyo. Kama si uwaziri ungekuta naye ni director au muigizaji wa bongo movies
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…