Waige mfano wa Tamthilia kama ya siri za Familia ambayo ukiitizama hauwezi kuwa bored,inaonyesha watu wamefanya mazoezi na wanajua wanachokifanya.Mi nashangaa siku hizi unakutana kundi la vijana wako kama mateja,wa kike na wakiume wamebeba vibegi migongoni na wana stendi za camera,ukiuliza kulikoni unaambiwa heti wana shoot movie,yaani hii taaluma imeingiliwa,.pia dosari zote zilizosemwa tatizo kubwa ni elimu na upeo,wengi walio kwenye bongo movie elimu yao ni la saba au kidato cha nne division 5,siku hizi ndio ytumeanza kupata graduate wachache ambao nao si kwamba wana wito na kazi bali sababu ya ukosefu wa ajira,Nigeria actors wengi tunao ona wana ama degree moja ama mbili na wamesomea hiyohiyo fani ya uigizaji.
bongo movie bado ina safari ndefu hadi kufikia pale ambapo bongo movie itakuwa haionekani kama kimbilio la walioshindwa shule ,mtu hana elimu yoyote lakini unamsikia anasema iko siku nitatoka tu kupitia bongo movie.Bongo movie nayo inahitaji akili za kutosha ili kuelewa audience wanataka nini,kama unemfeli shule utaishia commedy za kijingajinga tu lakini huwezi kuigiza movie zenye kueleweka ama kuvutia.