Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Bomu lilirushwa likaangukia hapa

safari kuelekea 2015 inazidi kuwa tete, tumwombe Mungu atusaidie kwani wnzetu CCM uzalendo umezidi kuwashinda... hawataki kabisa utamaduni wa kuachiana madaraka!!
 
hivi lema alikua anaimba taarabu au anahutubia, naona alikua anapozi kama za khadija kopa.
 
Kwa imani zetu tufunge......kwa kufanya maombi hakika hawa wauaji waaadhibiwa na Mungu adhabu ambayo hatujapata ona mfano wake.........wanaweza hata wakawa kwenye mkutano au kikao Mungu akawaadhibu wote....hata kwa tetemeko la Ardhi! Hawawezi kukwepa ghadhabu ya Mungu wauaji wote waliohusika na tukio hili.
Mkuu pole sana ila wewe ndio ungekuwa Mungu hakuna angebaki... teh teh Mungu awarehemu na awape roho ya kujutia dhambi yao hii kuu na hatimaye kuifikilia toba ya kweli ya ondoleo la dhambi.
 
sababu ya kufyatua risasi kwenye boom scene ni nini kama sio O.D.D iyo?=OPERATION DELETE AND DESTROY
SHANTA
 
Mkuu Crashwise hakika tukio lile halitokaa linitoke. Na kwako Mungi, Mungu ni mkubwa sana kwani tulipoondoa miguu yetu pale pakarushwa lile bomu! Humu JF huenda kungekuwa na thread ya RIP Arushaone na Mungi.

Mkuu Arushaone usinikumbushe, maana yake kama siyo wewe kufika pale tusingeondoka.

Labda kwa faida ya wanajf ni hivi:
Mimi nilikuwa sehemu ya mbele, ambapo bomu lilidondokea, Arushaone naye akaja pale akaniuliza Crashwise yuko wapi, nikamwambia twende nikupeleke mahali anapo zi upload picha, ndiyo kuondoka kwetu pale ambapo hata dakika moja haikuisha mlipuko ukatokea. Mkuu ukiangalia picha hapo juu utaona mahali niliposimama mara ya kwanza.
Pengine nisema Mungu alikuleta pale ili tuondoke zetu. Lakini pia mahali risasi zilipoingia kwenye gari ni sehemu alipokuwa crash amekaa kwa ndani. Ni Mungu tu mkuu!
 
Last edited by a moderator:
lukuvi mgonjwa

yule jamaa ni mgonjwa sana;
na ni aibu kwa jitu kubwa kama lile kuongea pumba kusapoti uovu uliogharimu damu za watu.
hivi vigezo gani vinatumika kuwapa uongozi watu washenzi namna hii?!
ila Mungu yupo!ipo siku litamlipukia yeye mwenyewe halafu tuone kama kura za huruma zinatafutwa kwa njia ya kuua watu!
 
Mkuu Arushaone usinikumbushe, maana yake kama siyo wewe kufika pale tusingeondoka.

Labda kwa faida ya wanajf ni hivi:
Mimi nilikuwa sehemu ya mbele, ambapo bomu lilidondokea, Arushaone naye akaja pale akaniuliza Crashwise yuko wapi, nikamwambia twende nikupeleke mahali anapo zi upload picha, ndiyo kuondoka kwetu pale ambapo hata dakika moja haikuisha mlipuko ukatokea. Mkuu ukiangalia picha hapo juu utaona mahali niliposimama mara ya kwanza.
Pengine nisema Mungu alikuleta pale ili tuondoke zetu. Lakini pia mahali risasi zilipoingia kwenye gari ni sehemu alipokuwa crash amekaa kwa ndani. Ni Mungu tu mkuu!
Mkuu, leo wakati napitia picha mbalimbali nilizopiga siku hiyo niliongopa sana baada ya kukuona sehemu ambayo bomu lilirushwa...MUngu mkubwa lakini hakuna kurudi nyuma ni mapambano mbele kwa mbele...
 
Kabla ya bomu mwenzako anakuja kukuita muende kwingine, wauaji tunao humu humu JF, na Boss wenu yuko humu anachungulia uzi unavyo kwenda. Bi mkubwa alisha mtuma Ben mje humu kusambaza Uongo wenu.
 
Nawashauri kuanzia sasa hawa wanaofanya mikusanyiko wawe wanafanya sweep kuhakikisha kwamba maeneo yapo salama. Na vile vile CCTV Camera ziwe zinatumika ijapokuwa na matukio ya muda mfupi. Kungekuwa na camera huyo jamaa angeonekana na angekamatwa.

Mkuu ilo la umuhimu sana chadema wawe wanafunga cctv camera tena HD kwenye mikutano yao ikiwezekana waweke namba tuchangie kununua CCTV CAMERA,Boston walifanikiwa kuwakamata wale walipuaji because ya hzo camera.
 
Mh Dr.W.Slaa pindi utakapochukua hii nchi hakikisha haki inatendeka kwa Watanzania, kabla ya hata kuwafunga wakina Kikwete na genge lake la Mafisadi anzeeni na kumshughulikia huyu Mwigulu Nchemba anadamu nyingi sana za watanzania kwenye mikono yake, kila akishiriki kwenye kampeni huyu Mwigulu Nchemba, mauaji na kutekwa watu lazima vitokee
 
Kwa mkusanyiko kama huu, na Arusha ambayo bado jeraha la Olasti halijapona ilikuwa WAZI kwa vyombo vyetu vya ULINZI na USALAMA kujipenyeza KISAYANSI na hatimae kubaini na kuwashika wale wote wanaolenga kuvuruga AMANI ya nchi hii. Tutangulize weledi tu, wanakamatika hawa...
 
Back
Top Bottom