Bodi ya Maziwa Tanzania ya nini?

Bodi ya Maziwa Tanzania ya nini?

Jaribu kutafuta umuhimu wa maziwa kwa afya ndo utajua kwanin kuna bodi ya mazima!
Viwanda vya maziwa vinafufuliwa kwa hiyo bodi itakuwa na kazi ya kuratibu uzalishaji na usambazaji wa maziwa. Kisheria ni lazima maziwa yote ni lazima yanunuliwe na viwanda na kusindIkwa ili yauzwe madukani lakini hapa nchini tunauziwa maziwa barabarani kutoka kwenye madumu! Ndiyo maana maradhi kama TB na brucellosis yanaendelea kuwepo.
 
Ya akina mama wenye mtindi mkubwa
Hapana hapana mkuu, hii inadhalilisha, sidhani ati wanapenda kuwa walivyo. Tafadhali, tusishambulie mtu kwa maumbile ninamashaka kama itasaidia mjadala
 
Hizo bodi zinachekesha, ni fragmentation isiyohitajika, kwani hauwezi kusema nutrition bila kuhusisha maziwa, na pia bodi nyingi na regulators wengi zilianzishwa bila tathmini yoyote kuhusu utendaji wa zilizopo. Kama ni muhimu ziwepo, basi tungeona ufanisi wa utendaji wao!
 
Ha ha ha haaaaa,nasubiri bodi ya makongoro,kuna wapenda supu pia
 
bodi Tanzania zimekuwa nyingi sana kuna bodi zisizo na kichwa wala miguu;
1. Bodi ya Pamba
2. Bodi ya Kahawa
3. Bodi ya Pareto
4. Bodi ya MAZIWA
5. Bodi ya Kahawa
6. Bodi ya MAZAO MCHANGANYIKO
7. Bodi ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA)
8. Bodi ya Bonde la Mto Kilombero
9. Bodi ya Ziwa Victoria
10. BODI YA SUKARI!!!
11. Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
12. Bodi ya Filamu Tanzania
***Sasa tujiulize hizi bodi zimetupa nini mpaka sasa?
 
bodi Tanzania zimekuwa nyingi sana kuna bodi zisizo na kichwa wala miguu;
1. Bodi ya Pamba
2. Bodi ya Kahawa
3. Bodi ya Pareto
4. Bodi ya MAZIWA
5. Bodi ya Kahawa
6. Bodi ya MAZAO MCHANGANYIKO
7. Bodi ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA)
8. Bodi ya Bonde la Mto Kilombero
9. Bodi ya Ziwa Victoria
10. BODI YA SUKARI!!!
11. Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
***Sasa tujiulize hizi bodi zimetupa nini mpaka sasa?

kuna mamlaka pia
mamla ya misitu
bodi ya utalii
mamlaka wizara ya mali asili ziko nyingi mno
na bodi tele
 
Nimestushwa na kukutana na gari STL pembeni imeandikwa BODI YA MAZIWA daah! hivi kweli tumefikia hatua ya kuunda BODI MAALUM Kwa ajili ya MAZIWA (naamini wanamaanisha haya maziwa ya KUNYWA kupitia mdomoni) hapo hapo tuna TANZANIA FOOD AND NUTRITION CENTRE (TFNC) nao wanapata bajet nenee!!

Mgao wa magari ya kutosha bila kusahau safari za nje ya nchi. Hapo hapo tuna TANZANIA FOOD & DRUGS AUTHORITY (TFDA) nao vile vile tiripu za nje kama kawa, VX za kutosha. Jamani tuoneeni huruma sisi walipa kodi maskini. TUMEROGWA??
Bodi ya maziwa ya nini? Si ya maziwa ! yaani ma- milk yale yanayotoka kwa ng'ombe, mbuzi ngamia n.k Au ya mkusanyiko mkubwa wa maji kwenye bonde kama vile ziwa Victoria na Tanganyika na mengineyo......just kidding
 
Mie kwangu naona iko sahihi. Kwanza tofautisha kati ya vitu vya muhimu na vitu vya muhimu zaidi. Mfano mtoto mdogo akizaliwa afu kwa bahati mbaya mama akafaliki huwa nalishwa nyama au dagaa? Hapo ndipo utajua kuwa maziwa ni kitu cha muhimu. Nakumbuka kuwa hasa watoto wanapotumia maziwa kwa wingi huwa na afya bora na uelewa mkubwa darasani
Maziwa ni muhimu bila shaka. Lakini kuna njia nyingine nzuri kabisa za kuonyesha umuhimu wa maziwa bila kuwa na bodi.
 
Hata kama kiongozi.
Kazi hiyo ingeweza kufanywa na TFNC tu badala ya kuiundia bodi yake.

Alafu utambue vyenye umuhimu kiafya sio MAZIWA tu.

Unaweza tafakari kwa nini kuna bodi ya KAHAWA, KOROSHO, PAMBA, SUKARI, nk?

Unajua kwamba maziwa ni zao litokanalo na mifugo na linahitaji kutafutiwa uwekezaji, masoko ya kutosha, na uhamasishaji wa watu kujikita ktk kufuga ng'ombe wa maziwa ili kuongeza uzalishaji ktk kutimiza mahitaji ya soko?

Hivi umewahi jiuliza kwa nini maziwa mengi yaliyosindikwq yanatoka nje ya nchi?

Maziwa kama yalivyo mazao mengine ni zao litokanalo na mifugo ambalo linahitaji uwekezaji mkubwa ili liweze kuzalisha ajira za kutosha. Ili kufikia kusudio hilo lazima kuwe na chombo cha kuratibu na kusimamia zao hilo nacho ni BODI YA MAZIWA

Tafakari kwa kina utaona umuhimu wa bodi kama hizi

Updates

Unafikiri kuna umuhimu wowote wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU? kwanini kazi hiyo isifanywe na WIZARA YA FEDHA kushirikiana na TCU na vyuo husika? je nao ni ufujaji wa fedha?

Endelea kutafakari
 
Back
Top Bottom