Bodi ya Maziwa Tanzania ya nini?

Bodi ya Maziwa Tanzania ya nini?

Tuanze na hii bodi ya Maziwa a.k.a NYONYO katika kudhibiti matumiz ya serikali kisha twende pale TANTRADE maana ni kama "utani" flani hivi yaani wao kazi yao kubwa kuandaa maonyesho ya SABA SABA (June/July) wakishamaliza mpaka mwakaniiiii) wanabakia kukodisha mabanda kwa makanisa pendwa na vyuo "feki") Daah Nchi hii jamani.
 
Usisahau pia hua kuna siku ya unywaji wa maziwa hii hufanyika kila mwaka
 
Pia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hawa jamaa sijuagi wanashughulikia MICHEZO gani hapa nchini
 
Afu haohao bodi ya maziwa utakuta hawajui ata kuchunga ng'ombe
 
Non sense!
Hivi ukiwa na mtoto mdogo ambaye bado hajafikia umri wa kunywa hiyo lishe mnaodai ma baati mbaya akaambiwa asitumie amaziwa ya mama huwa wanakula sembe eh!!!!. Mambo mengine ni kujiongeza tu mwenyewe. Watoto wanao lelewa bora liende ni shida hadi mtaani. Darasani ndo kabisaa. Mabichwa yao kama yametiwa kwenye deep freezer
 
shida kubwa ya watanzania hasa wabunge ni kupitisha mambo kishabiki bila kuangalia manufaa kwa taifa. Hii Bodi ya Maziwa iliptishwaje kilaini kuanzishwa. inasikitisha sana jamanii
 
Pia tuongeze bodi nyingine mfano:
1.bodi ya ugali,
2. bodi ya mtama
3. bodi ya soya,
4. bodi ya dengu,
5. bodi ya maharage,
6. bodi ya choroko,
7. bodi ya mboga za majani kwa ujumla
8. bodi ya malazi,
9. bodi ya mavazi,
6. bodi ya saloon na mikorogo,
7. bodi ya nyama ya ng'ombe
8. bodi ya nyama ya mbuzi
9. bodi ya nyama ya kondoo,
10. bodi ya kitimoto,
11. bodi ya nyama ya kuku,
12. bodi ya nyama ya bata
13. bodi ya ndege kwa ujumla (birds in general)
14. bodi ya mayai,
15. bodi ya kuku
16. bodi ya machungwa
17. bodi ya mchicha
18. bodi ya sukuma wiki
19. bodi ya spinachi
20. bodi ya matembele
21. bodi ya chines
22. bodi ya uwele
23. bodi ya vitumbua
24. bodi ya maandazi
25. bodi ya ufuta
26. bodi ya samuli
27. bodi ya siagi
28. bodi ya ulezi
29. bodi ya mananas
30. bodi ya ndizi
31. bodi ya mapera
32. bodi ya parachichi
33. bodi ya kabechi
34. bodi ya ukwaju
35. bodi ya ubuyu

Nimesahau zingine.unaweza kuongeza zingine unazozikumbuka ili tz yetu ipige hatu mbele

Eti bodi yaaziwa!!!! aahahahahaaaaaa!!! tz bana..Mtu haishi kwa maziwa tu isipokuwa kwa aina zote ya chakula kama baadhi zilizotajwa hapo juu ili kuujenga. mwili. Sasa ukisema unaunda bodi eti ya kushugulikia maziwa peke yake kama lishe bora, vipi chakula vingine? kwakuzingatia umuhimu wa makundi ya chakula; Piga ua ni lazima Rais aanzishe bodi kwa kila aina ya chakula jukumu lake ni kwaelimisha wananchi umuhimu wa kila kundi la chakula kama bodi ya maziwa inavyofanya. La sivyo hakuna haja na bodi ya maziwa kwakuwa tayari tuna tfda na ile ya nutrition.

Tusisahau pia Bodi ya Msoga
 
Halafu na ubovu wote huu bado mtu mzima anataka bado media attention mara kaondoka na helikopta, mara karudi kukabidhi mjengo ooh mara huyo South sasa kaibuka na kumtembelea jembe!! AIBU AIBU AIBU!! enzi zako mapato yalikuwa yanapotela wapi?
 
tuseme tu ukweli hali ilikuwa mbaya enzi za awamu ile! wapigaji walikuwa wengi hebu fikiria eti pale WIZARA YA MALIASILI & UTALII watu wanaaacha jengo lao wanaenda kupangisha jengo nje ya pale (binafsi) na wizara ilikuwa na WAZIRI "KIJANA" kutwa/kucha ama marekani au hotelini Arusha (vikaoni)
 
Hata kama kiongozi.
Kazi hiyo ingeweza kufanywa na TFNC tu badala ya kuiundia bodi yake.
halafu utambue vyenye umuhimu kiafya sio MAZIWA tu.

Unajua majukumu ya TFNC wewe????Hivi bila maziwa mtoto anaweza kusurvive?
Kama tuna bodi za pamba au tumbaku inayolimwa mikao kama miwili hivi kwa nini uone shida kwa bodi ya maziwa yanayozalishwa na kuuzwa nchi nzima?
Tatizo lako hauoni umuhimu wa maziwa.
 
Back
Top Bottom