SSH2025_2030
JF-Expert Member
- Jul 9, 2012
- 9,661
- 9,802
Tuseme kazi za bodi ya maziwa haziwez kufanywa na TFDA au TFNC? kwa minajili ile ile ya kubana matumiz ya serikali?
Tuseme kazi za bodi ya maziwa haziwez kufanywa na TFDA au TFNC? kwa minajili ile ile ya kubana matumiz ya serikali?
mkuu wewe umewahi kupata hicho kikombe cha maziwa kutoka bodi ya maziwa?..Hii bodi inahakikisha kila mtu anapata walau kikombe kimoja cha maziwa kwa siku..
mkuu wewe umewahi kupata hicho kikombe cha maziwa kutoka bodi ya maziwa?..
au huku kwetu Tanganyika, hawafiki
Umuhimu wa Bodi ya Maziwa upo, sema tatizo haifanyi kazi inayotakiwa. Kumbuka TZ tuna ng'ombe milioni 23 lakini tuna-process kiasi kidogo sana cha maziwa. Dairy industry iko chini sana. Hivyo kama bodi hiyo ingekuwa inafanya kazi vizuri hata tusingeona maziwa kutoka Kenya, uganda, S.Africa hata S. AmericaNimestushwa na kukutana na gari STL pembeni imeandikwa BODI YA MAZIWA daah! hivi kweli tumefikia hatua ya kuunda BODI MAALUM Kwa ajili ya MAZIWA (naamini wanamaanisha haya maziwa ya KUNYWA kupitia mdomoni) hapo hapo tuna TANZANIA FOOD AND NUTRITION CENTRE (TFNC) nao wanapata bajet nenee!!
Mgao wa magari ya kutosha bila kusahau safari za nje ya nchi. Hapo hapo tuna TANZANIA FOOD & DRUGS AUTHORITY (TFDA) nao vile vile tiripu za nje kama kawa, VX za kutosha. Jamani tuoneeni huruma sisi walipa kodi maskini. TUMEROGWA??
Jaribu kutafuta umuhimu wa maziwa kwa afya ndo utajua kwanin kuna bodi ya mazima!
ni aibu kwa nchi kama hii kutegemea maziwa toka Kenya amabayo robo tatu ni ARID & SEMI-ARID LAND (ASAL) tena maziwa yameundiwa na bodi na wanaapata bajeti toka serikalini na magari ya kifahari (V8), posho za kumwaga na TRIPS za nje za kutosha.
Mdau ameongea vizuri kusema tuna ng'ombe wengi uzalishaji ni mdogo, hii ni changamoto ambayo bodi ya maziwa inatakiwa kuiona na kuifanyia kazi lakini hii itategemea pia serikali kuiwezesha bodi hii ili kusaidia wafugaji vijijini kuzalisha maziwa kwa wingi kwa kuwapa vitendea kazi vya kutosha na elimu ya kutosha kwa wafugaji wengi
Bodi ya maziwa ipo kwa mujibu wa sharia kama zilivyo bodi nyingine katika wizara ya kilimo na mifugo na imeundwa tangu mwaka 2004. Bodi ya maziwa ni taasisi muhimu inabidi kuimarishwa zaidi kwani kulingana na majukumu yake ya kusimamia sharia ya maziwa, kuendeleza tasnia ya maziwa na kulinda afya ya watumiaji maziwa.
Kwa ufupi kazi za bodi ya maziwa ni
· Kuendeleza Sekta ya maziwa Tanzania
· Kudhibiti uingizaji wa maziwa na bidhaa zake toka nje ya nchi ili kulinda wazalishaji masoko ya wazalishaji wa ndani
· Kuwaunganisha wadau wa maziwa nchini
· Kuhamasisha unywaji, uzalishaji na usindikaji wa maziwa Tanzania
· Kushawisi uwekezaji katika sekta ya maziwa
TFDA kwa upande mwingine kazi yake katika upande wa maziwa ni kulinda afya ya mlaji kama ilivyo kwa bidhaa nyingine ambazo sio za maziwa.
TFNC kazi yake kubwa ni kufanya utafiti katika maswala yanayohusu chakula na lishe kwa ujumla