Muagizaji magari pesa anaipata kwa style tofauti.
1. Anapoagiza magari kwa wingi anapewa punguzo la bei japan hivyo kufanya CIF kuwa chini tofauti na wewe.Akija bongo atalipa kodi tofauti na wewe.
2. Ananunua gari kwenye auctions ama minada. Huko gari zinapatikana kwa bei chee sana kwa madaraja tofauti.
3.Anapokuagizia kuja bongo anakuongezea cha juu japo utaona anapata kidogo ila anakunyoosha sababu yeye kanunua mfano gari unayoona ni $5,300 yeye kauziwa labda $3,500. Akija anakupiga za kichwa hakosi 5-6M kila gari ikiwa fully paid.