Biswalo Mganga ana shida gani?

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
1,028
2,448
Hii "Jamuhuri ya mitandao" ina vichekesho vingi sana na vya kusisimua.

Kelele ni nyingi sana kwenye Jamuhuri hii ya mitandao.

Mpaka sasa, DPP amepachikwa shutuma nyingi ikiwemo kubambikia watu kesi na kudhulumu fedha.

Sifahamu kwa hakika kama wanaoyasema hayo ni wahanga wa mkono wa DPP ama ni wafuasi tu wa Twitter na Facebook.

Lakini kwa vyovyote vile, naamini wengi wao ni wafuasi tu wa mitandaoni.

Humu mitandaoni kuna wajuaji wengi sana. Lakini bahati nzuri ni wajuaji wasiojua kitu.

Hata waliofeli fom foo, nao wanamuelekeza DPP jinsi ya kufungua mashtaka na kufanya kazi zake.

DPP ni ofisi yenye watu na mifumo ya uendeshaji wa mashtaka.

Kila faili la mashtaka ya jinai linalokuja mezani kwa DPP lina mlolongo mrefu kutoka TAKUKURU, POLISI, TISS na kwingineko.

Kazi ya DPP sio kuamka tu na kubambikiza watu kesi. Kuna prosecutorial process.

Hawa wajuaji wa mitandaoni wanaojivika ujuvi wasiokuwa nao, ni genge tu la wafuasi wasiojitambua.

Katika miaka mitano, tumeshuhudia jinsi mafisadi yalivyobinywa na kushughulikiwa.

Wauza ngada, majangili, wakwepa kodi na wezi wa mali ya umma walinyooka kama rula.

Haya majizi kwa vyovyote vile yana wafuasi mitandaoni.

Sitarajii kuona majizi haya yakifurahia kazi njema ya DPP.

Vinginevyo watuambie, kibaya ni kipi hasa alichokifanya DPP.
 
Huna akili. Wewe ni goigoi usiefuatilia masuala.Unaelewa kuwa kuna sheria ambayo inazuia DPP kuondolewa kwenye nafasi yake labda awe anaumwa na kushindwa majakumu yake au labda awe amefanya serious crime?

Huyo DPP ameondolewa kwa mujibu wa sheria hiyo?Wewe ni ngumbaru sawa na aliemuondoa DPP kwenye nafasi yake bila ya kuzingatia sheria.Tanzania karibia kila mtu ni goigoi kuanzia wananchi wa kawaida hadi viongozi wakubwa. What a shame!

9876uy.jpg
0987654nb.jpg
 
Huna akili. Wewe ni goigoi usiefuatilia masuala.Unaelewa kuwa kuna sheria ambayo inazuia DPP kuondolewa kwenye nafasi hiyo labda awe anaumwa na kushindwa majakumu yake au labda awe amefanya serious crime?

View attachment 1783057View attachment 1783058
Kwani DPP ameondolewa ama ameteuliwa kuwa Jaji?

Weka sheria inayosema kuwa DPP hapaswi kuteuliwa kuwa Jaji.
 
Bwana Boswaro mbona unataabika sana,kwani kuna nini?sema kama ulitenda haki huna haja ya kuwa na shaka.ila kama ulitenda dhuluma au kushiriki kufanya dhuluma basi subiri malipo yako
 
Hii "Jamuhuri ya mitandao" ina vichekesho vingi sana na vya kusisimua.

Kelele ni nyingi sana kwenye Jamuhuri hii ya mitandao.

Mpaka sasa wamempachika DPP shutuma nyingi ikiwemo kubambikia watu kesi na kudhulumu fedha.

Sifahamu kama wanaoyasema hayo ni wahanga wa mkono wa DPP ama ni wafuasi tu wa Twitter na Facebook.

Lakini kwa vyovyote vile, naamini wengi wao ni wafuasi tu wa mitandaoni.

Humu mitandaoni kuna wajuaji wengi sana. Lakini bahati nzuri ni wajuaji wasiojua kitu.

Hata waliofeli fom foo, nao wanamuelekeza DPP jinsi ya kufungua mashtaka na kufanya kazi zake.

DPP ni ofisi yenye watu na mifumo ya uendeshaji wa mashtaka.

Kila faili la mashtaka ya jinai linalokuja mezani kwa DPP lina mlolongo mrefu kutoka TAKUKURU, POLISI, TISS na kwingineko.

Kazi ya DPP sio kuamka tu na kubambikiza watu kesi. Kuna prosecutorial process.

Hawa wajuaji wa mitandaoni wanaojivika ujuvi wasiokuwa nao ni genge tu la wafuasi wasiojitambua.

Katika miaka mitano, tumeshuhudia jinsi mafisadi yalivyobinywa na kushughulikiwa.

Wauza ngada, majangili, wakwepa kodi na wezi wa mali ya umma walinyooka kama rula.

Haya majizi kwa vyovyote vile yana wafuasi mitandaoni.

Sitarajii kuona majizi haya yakifurahia kazi njema ya DPP.

Vinginevyo watuambie, kibaya ni kipi hasa alichokifanya DPP.

Kama kushughulikia majizi ni "jambo baya" basi hewala. Na iwe hivyo!
Watu waliodaiwa fedha na Biswalo Mganga mwenyewe kwa maagizo kuwa wametumwa na Mwendazake wapo.

Ile plea bargain haikuwa wazi kwa watuhumiwa wote kama unavyodhani bali iliwalenga wanaodhani wana fedha nyingi.

Hata waliotoa hela na kuachiwa wanasema fedha waliyotoa ni zaidi ya ile iliyorwkodiwa kuwa imekwenda Benki Kuu kwa Akaunti ya DPP. Kwa hiyo aliyeandikiwa katoa Tsh 1.5 Bilion aweza akawa ametoa Tsh 2.0 Bilion.

Biswalo mwenyewe na vijana wake anao waamini ndiyo wamehusika katika kubeba hizo fedha.

Jiulize kwa nini Kompyuta za DPP Ofisi ya DSM ziliibiwa mara baada ya kupokea fedha za watuhumiwa?

Hapo ndipo suala la kumuundia Special Tribunal Biswalo Mganga kwa mujibu wa kifungu 3-8 cha Sheria Namna 27 ya 2008 ya National Prosecution Services inapokuwa ndiyo njia mwafaka ya kumaliza sintofahamu hiyo.

Mimi mwenyewe nina ndugu yangu anayekiri kumpa Biswalo hela zaidi ya zilizoripotiwa. Kama Tribunal itakuja undwa hawa ndiyo mashahidi na wako tayari ku testify
 
Jamaa Hana shida yyte yeye alikuwa spika Tu, maiki na waya vilikuwa kwingine , jamaa Hana hata shida , anawachora Tu, maamuz yote yalikuwa under high command ambayo mama Samia ni mmoja wapo, so unawezaje kunilaumu mimi.

The same to Ndungai, unamlaumu Ndugai ana uwezo gani wa kuingiza watu kibabe bungeni, hiyo nin kazi ya high command ambayo mama Samia ni inner part. Mimi ni mtekelezaji tu.
 
Huna akili. Wewe ni goigoi usiefuatilia masuala.Unaelewa kuwa kuna sheria ambayo inazuia DPP kuondolewa kwenye nafasi hiyo labda awe anaumwa na kushindwa majakumu yake au labda awe amefanya serious crime?

Huyo DPP ameondolewa kwa mujibu wa sheria hiyo?Wewe ni ngumbaru sawa na aliemuondoa DPP kwenye nafasi yake bila ya kuzingatia sheria.Tanzania karibia kila mtu ni goigoi kuanzia wananchi wa kawaida hadi viongozi wakubwa. What a shame!

View attachment 1783057View attachment 1783058
Asante mkuu.
 
Yaani sijajua mantiki ya bandiko lako. Concept ni kuwa ofisi yake inahusika na yale ambayo rais samia alisema kuwa kuna ubambikizwaji wa kesi na akaagiza kesi hizo zifutwe.

Najua ni rahis kugundua kuwa DPP aliishindwa kufanya majukumu yake ipaswavyo mfano inshu ya Mmoja wa COVid 19 ambayo alimtoa usiku kuja kuapa bungeni asubuhi kinyume na sheria.

Kama tunahitaji Kiongozi anaefuta haki na sheria ni vema asiwe Biswalo kwa kuwa yeye anafuata maelezo toka juu.
 
Mimi mwenyewe nina ndugu yangu anayekiri kumpa Biswalo hela zaidi ya zilizoripotiwa.
Tutajuaje kama unayoyasema ni kweli au unadanganya tu?

Hebu weka hapa jina la huyo ndugu yako pamoja na taarifa zake zote (case number, hati ya mashtaka na mahakama aliyopelekwa).

Tuwekee pia na nakala ya HATI YA MAKUBALIANO YA KUKIRI KOSA ili tuone nini kilichoandikwa humo na kukubaliwa.

Maneno mingi sana nyinyi... blah blah tu.
 
Watu hawana shida na majukumu ya DPP,, bali wanashida na utendaji wake. Wanamtuhumu kwa kuwabambikia watu kesi.

Wanmtuhumu kujivika madaraka ya kupokea fine na kuziweka kwenye account yake kinyume cha sheria (Ufisadi).

Tuhuma hizi zipo mitandaoni wengi tumeziona, tungefurahi hizi tuhuma ungezijibu. Lakini ukituhumu wanaokutuhumu haikusafishi wewe, bali inaleta shaka zaidi kuwa pengine ni kweli uliyafanya haya.
 
Over
 
Yaani sijajua mantiki ya bandiko lako. Concept ni kuwa ofisi yake inahusika na yale ambayo rais samia alisema kuwa kuna ubambikizwaji wa kesi na akaagiza kesi hizo zifutwe.

Najua ni rahis kugundua kuwa DPP aliishindwa kufanya majukumu yake ipaswavyo mfano inshu ya Mmoja wa COVid 19 ambayo alimtoa usiku kuja kuapa bungeni asubuhi kinyume na sheria.

Kama tunahitaji Kiongozi anaefuta haki na sheria ni vema asiwe Biswalo kwa kuwa yeye anafuata maelezo toka juu.
Hata yeye amewahi kusema hadharani kwamba anauwezo wa kumpa kesi mtu yoyote na asifanywe kitu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom