Binti yangu, ni Akheri uwe Single mother kuliko uishi na Mwanaume mpumbavu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
BINTI YANGU; NI AKHERI UWE SINGLE MOTHER KULIKO UISHI NA MWANAUME MPUMBAVU.

Anaandika, Robert Heriel
Baba na Mume.

Kama vile Mimi Taikon, Nyota ya Tibeli nisivyoweza kuishi na Mwanamke mpumbavu, hata angekuwa Mama yenu, vivyohivyo nilimuambia Mama yenu kuwa kamwe asijevumilia kuishi na Mimi kama nitamletea upumbavu pumbavu wa kipuuzipuuzi.

Watibeli hatutauvumilia upumbavu!

Binti zangu nawausia, kama nilivyowafundisha, basi haya nayo muyashike Sana. Yale yote ambayo mnataka kufanyiwa na Waume zenu basi wafanyieni ninyi. Na Yale yote ambayo hamtaki kufanyiwa basi msiwafanyie Waume.
Vivyohivyo na Kwa wanaume.

Tunavumilia na kusamehe Makosa lakini kamwe hatuwezi kuvumilia na kusamehe uhalifu na uovu.

Binti yangu sisemi baba yako nilikuwa Mwema Sana. Au ni mkamilifu. Ila nilikuwa napenda Wema na kupenda kuwa Mkamilifu. Halikadhalika napenda Watu Wema na wapendao ukamilifu.

Nilikuusia uwe Mwema, upende Wema na kuutenda. Ujitahidi kila uwezavyo kuwa Mkamilifu. Usipende kutoa Excuse pale unapokosea au kutenda uhalifu au dhambi. Kwa sababu ubaya na Wema hauna visingizio.

Ni kweli, tunaangalia Wema Kwa Watu kuliko Ubaya, hivyo ndivyo Watibeli tulivyo. Lakini kamwe hatutapenda kuona MTU akijipa kisingizio cha kutenda ubaya.
Epuka MTU aombaye Msamaha Kwa mwamvuli wa ubinadamu, yakuwa; nisamehe, hakika Mimi ni binadamu kukosea nimeumbiwa.
MTU huyo ni Mbaya. Watu wabaya hutumia ubinadamu kama kisingizio cha kuomba Msamaha.
Na watu wenye kisingizio hicho hutafuta ubaya Kwa wale wawaombao Msamaha.

Mtu akikukosea, aseme; Ni kweli nimekosea, nimekuwa mbinafsi, nimekuwa mtu nisiyejali wengine, mpaka nimefikia kukuumiza Ndugu au MKE au Mume wangu, naomba unisamehe nakiri nimekukosea. Nihukumu na uniadhibu utakavyo ilimradi haya yaishe"
Hiyo ndio anaomba Msamaha.
Na sio MTU anayeomba Msamaha akiwa mwingi wa visingizio na kumtupia lawama mwingine au Jambo jingine. Huku akikimbia adhabu na hukumu ya Yale aliyoyafanya. Mwombaji wa Msamaha sharti aone kosa alilofanya ni kubwa kuliko hata adhabu utakayompa.
Na sio kuogopa adhabu hivyo itamlazimu kuomba Msamaha.

Mtoa Msamaha ndio yeye Kwa Wema wake anaweza kukusamehe na kukupa adhabu kidogo au asikupe kabisa. Pia yeye ndiye anatakiwa kuwaza kuwa binadamu tumeumbwa kukosea.

Lakini sio wewe mkosaji. Alaah!

Binti zangu, Baba yenu nimekuwa mwingi wa mawaidha, ni Kwa sababu nawapenda. Sitaki muishi Kwa tabu.
Ni akheri uishi pekeako au single mother ukiwa na mtoto au Watoto wako kuliko uishi na Mwanaume mpumbavu.

Siwafundishi kuwa wajeuri au Kiburi. Na wala asitokee miongoni mwenye akatumia maneno yangu kama nguzo ya kufanya mambo yasiyofaa Kwa Mumewe.
Bali watiini Waume zenu, wapendeni Waume zenu, wahudumieni Waume zenu.

Lakini Kamwe usimtii wala kumpenda wala kumhudumia mwanaume mpumbavu.
Na hii ndio maana kila Siku Baba yenu ninawausia Msome mpate Elimu itakayowasaidia katika uzalishaji Mali, muwe wafanyakazi na wafanyabiashara.
Ili muwasaidie Waume zenu na watoto wenu. Lakini pia mjihami Huko mbeleni endapo mwanaume atageuka kuwa MPUMBAVU akaleta ubinafsi na mambo yasiyofaa.

Ni Bora uwe single mother kuliko uishi na Mwanaume au Mume mpumbavu mwenye Tabia na Matendo kama haya;

1. Mbinafsi.
Kama vile Mimi Baba yenu nisivyoweza mvumilia Mwanamke mbinafsi hata angekuwa Mama yenu, ndivyo hivyohivyo nanyi Binti zangu msikubali kuishi na Mwanaume mbinafsi.
Ni hatari kuishi na Mwanaume mbinafsi. Wanaume wabinafsi wapo kundi la wanaume wapumbavu. Ubinafsi tafsi take ni kujipenda zaidi kuliko pitiliza kuliko kupenda wengine.

2. Mshirikina na mchawi.
Kamwe usije ukakubali kuishi na Mwanaume mshirikina na mchawi. Siku ukisikia tuu anamambo hayo Anza taratibu za Talaka mapema. Mimi kama Baba yako nasema; omba Talaka. Na hiyo hakuna Mijadala sijui vikao.

Kuishi na Mwanaume mshirikina na mchawi na ukajua, alafu ukakubali kuendelea kuishi naye jua nyote ninyi ni washirikina na wachawi.
Watibeli hatuwezi kuishi na watu wachawi na washirikina.
Mtu yeyote ambaye anakuambia mambo ya sijui umelogwa au Uchawi Uchawi MTU huyo ni mshirikina. Na washirikina ni kikawaida ni wapumbavu.

3. Anayekutishia kukuacha au kukufukuza.
Mumeo Ajue kuwa siku atakayetishia kukuacha au kukufukuza siku hiyohiyo nakuamuru muache. Mimi kama Baba yako nimekuambia. Watibeli hatutishiwi Nyau.
Tunajua uwezo wetu, tunajua thamani yetu, tunajua nini tunachoweza kukifanya ili mahali pawe pazuri, furaha na Amani.
Tunaakili za kutosha na zaidi tunamjua Mungu.
Ikiwa hatukutendea ubaya wowote, tumekuwa Wema kwako lakini hautaki kuwa nami, Kwa nini nikulazimishe kana kwamba unanifanyie hisani au unanisaidia. Hatulazimishi Mapenzi na mambo mazuri Kutoka Kwa wengine.
Hata kama itatuuma lakini kamwe hatutalazimisha. Tumefundishwa kuukabili ukweli hata uwe WA namna gani.
Hivyo ndivyo binti za Tibeli mnapaswa kuwa.

Ndio maana ninawaambiaga mtimize Ile amri ya kufanya kazi ili msijeingia katika Utumwa.

4. Anayetaka umtii hata katika Uovu na uhalifu.
Mtii na mheshimu mwanaume anayemtii na kumheshimu Mungu.
Kadhalika Sisi Watibeli tunawapenda na kuwajali Wanawake wanampenda Mungu, waadilifu.

Sio umheshimu na kumtii mwanaume asiyemtii Mungu. Huo ni ushetani. Ni kumtii shetani.
Mwambie mwanaume kama unataka nikutii basi amtii na kumcha Mungu.

Huwezi mtii mwanaume Mzinifu, mwingi, muuaji, anayetamani wake za Watu, asiyeheshimu wazazi wake, asiyefanya kazi, anayeabudu mashetani.
Hakuna heshima ya hivyo.

Ni Wanawake wapumbavu wanaoheshimu wanaume waovu.

Ni Sawa na Wazazi wanaotaka kuheshimiwa Wakati wao hawamheshimu Mungu.

Jitu linadhulumu watu, linatapeli Watu, linaiba Mali za Watu, linafitinisha Watu alafu unaliheshimu na kulitii. Binti za Tibeli hawapo hivyo. Usikubali kuishi na Mwanaume mdhulumati, huyo ni mpumbavu.

Siku ukigundua Mumeo ni mdhulumati omba Talaka, usilishe Watoto wako na mapato ya dhulma, mapato ya machozi ya Watu wengine.
Ndio maana nikakuambia ni lazima Binti Tibeli mfanye kazi halali ili msijeingia majaribuni.
Ni Bora ule ugali mlenda na watoto wako kuliko kuishi na Mwanaume mdhulumati, muuaji, mwanaume mpumbavu.

Mwambie ukitaka nikuheshimu na kukutii basi mheshimu na kumtii Mungu. Full stop.
Kama hafuati amri na maagizo ya Mungu. Na kama haamini katika Mungu basi Mila na desturi na uadilifu.

Mwambie kama humheshimu na kumtii Mungu aliyeumba mbingu na nchi unategemea Mimi ndio nikuheshimu na kukutii kisa unaleta elfu 20 za chakula humu?

Hakuna kucheka na Kima.

Baba yenu nimesema,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Namuomba Allah ainusuru familia yangu dhidi ya fitna,husda,shari na kila chenye kuleta wasiwasi kwa nafsi...nami aniongezee nguvu na ujasiri wakuiongoza familia yangu katika mwenendo wa uadilifu.
Na Mungu akubariki sana wewe, familia yako na azibariki kazi za mikono yako.
Mimi na mke wangu kipenzi pia tunawaombea kheri, fanaka na amani tele
 
BINTI YANGU; NI AKHERI UWE SINGLE MOTHER KULIKO UISHI NA MWANAUME MPUMBAVU.

Anaandika, Robert Heriel
Baba na Mume.



Baba yenu nimesema,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Jamaniii ile kaswida ya vumilia mwanangu Kwa mume usije ondoka,Huna mume huna Raha,huna mume huna Raha,aso mume ana wanga aeeeeeeee


HAYA ASANTE KWA WARAKA TUMEUPOKEA SISI WA KANDA ZA TANGA HUKU

Sent from my TECNO LE6 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu nina majonzi;
Crush wangu leo kavishwa pete ya uchumba na mwanaume wake.... nimehuzunika sana. Nifanyeje? Au nimpigie mpenzi wangu nimwombe ushauri?
 
Back
Top Bottom