Binti atoa penzi siku 3 bila ridhaa yake, na kesi kashindwa

Binti (Miaka 19) yupo kwa Basi, anatoka zake Dar kwenda Uyulo-Mbeya kumsalimu Shangazi yake, anawasiliana nae kwa Simu akiwa safari, lakini anafika Iringa Simu inakata Chaji.

Binti anamuomba Simu Jamaa aliyekaa pembeni yake aitwaye MAPINDUZI NGALLA, lakini anapiga Simu Shangazi hapatikani. Jamaa anamchombeza Binti kwani unaenda wapi?
Binti anajibu Uyole-Mbeya,
Jamaa anamwambia mmh! pale Uyole usiku kuna wauaji, twende ukalale kwangu Mbalali kisha kesho utamalizia safari yako, Binti anamuuliza kwako unakaa na Familia?
Jamaa anajibu ndio.
👆🏿
Basi Jamaa anamchukua Binti anaenda nae kwake kijiji cha URUNDA- Mbarali, , kumbe Jamaa anakaa peke yake, wanalala chumba tofauti, lakini usiku Jamaa anaenda chumbani kwa Binti, anadai penzi, Binti anakataa lakini Jamaa ana force kingi - anambaka Binti, kesho inafika Jamaa anamfungia Binti ndani, usiku anambaka tena, kesho yake Jamaa anasahau kufunga mlango Binti anafanikiwa kutoka ndani, baadae Jamaa anakamatwa kwa ubakaji.
👆🏿
Jamaa ameshinda kesi. Unajua kwanini? Kifungu -130(1)(2)(b)- ambacho alishtakiwa nacho kinaelezea ubakaji ambao Mwanamke anakubali kufanya mapenzi lakini kukubali kwake kunatokana na kutishiwa kuuliwa, kuumizwa... lakini hii kesi ushahidi wa Binti ulikuwa kwamba alilazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa (consent) yake, hii kitu inaangukia kifungu kingine tofauti -130(1)(2)(a) cha Kanuni ya Adhabu.
Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji MASHAKA imemuachia jamaa aliyekuwa amefungwa miaka 30 na mahakama kuu.
Jaji :- Mashaka
Wakili wa Serikali 1 .Edgar Luoga.
2. Devise Msanga.

Nani alaumiwe?
  1. shangazi aliyepotea hewani.
  2. Mapinduzi[mbakaji]?
  3. Binti[Tunda]?
  4. Mawakili wa Serikali waliokosea vifungu vya sheria?
  5. Mungu aliyeshindwa kumfanya jama adindishe?
  6. Serikali inayosajili mawakili chini ya viwango?
Kuna ushahidi wowote? Tuanzie hapo
 
Katoka mjini kaenda kubakwa kijijini, enewei wa kulaumiwa ni Mungu kashindwa kufanya jamaa asidindishe
dah hahahaha umenifanya hakimu nicheke kwa comment yako hahahaha ok ngoja kuna boya kazurumu viwanja vya watu kama hana hela nimpige mvua za kutosha nikiripoti toka mbele ya kiti cha uhakimu hapa mahakama ya rufaa ni mimi hakimu mr pipa
 
Panapokuwa na pesa, hawa mahakimu wanapinda, huna hata haja ya kuleta vifungu ku justify uharamia.
Huyu ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mahama si ipo huru?
Jaji ameonyesha makosa ya mawakili wa Serikali, swali je , nani alaumiwe?
 
Mahakama iliyo mfunga jamaa walikoseaa sna

Kitendo Cha kukubaliana kwennda kukala kwake Ni makosa eti Kuna waauwaji
 
Nawafikiria sana wanaosema alaumiwe binti kisa kaenda kulala kwa mtu asiyemjua.

Mlitaka alale nje?

Wasafiri wangapi wana pesa ya kutosha kiasi gari lingekwama hapo Mbarali wangeweza kulipa lodge walale?

Wangapi wangeenda nyumbani kwa Mapinduzi kwa kukosa pesa?

Mtu anajiona smart kisa kaandika vitu anavyoviona kwenye movie. Acheni hizo tabia.

Mapinduzi labda aseme nilikubaliana ngono na mdada kama malipo ya kuja kulala kwangu.
 
Binti hakufikiria sawasawa. Iringa ilikuwa ni kama nusu ya safari tu, hakutakiwa kuchukua maamuzi ya kukubaliana na huyo bwana maana muda wa kutosha bado ulikuwepo ili kumpata shangazi.
 
Back
Top Bottom