Update kesi ya Bandari: Majibu ya mawakili wa wananchi, waleta maombi leo Julai 28, 2023

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
#Updates kesi ya bandari leo 28th July 2023

Majaji wote watatu wanaingia muda huu saa 09: 44 asubuhi.

MAJAJI watatu;

1. Hon. Ndunguru

2. Hon. Ismail

3. Hon. Kagomba

Wote wameinama wanaandika

Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.

MAWAKILI WA SERIKALI;

1. Adv. Chang'a

2. Edson Mwaiyunge

3. Alice Mkulu

4. Stanley Kalokola

5. Edwin Lwebilo
...
MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI;

1. Mpale Mpoki

2. Boniface MWABUKUSI

3. Philip Mwakilima

4. Livino Ngalimitumba.

Walalamikaji wote wamefika wapo ukumbini;

1. Alphonce Lusako

2. Emmanuel Chengula

3. Raphael Ngonde

4. Frank Nyarusi.

Anasimama wakili wa serikali na kusema wako tayari kwa ajili ya REJOINDER kama hakuna pingamizi.

Anasimama wakili senior Mpale Mpoki kwamba wako tayari na anaijulisha mahakama kwamba ataanza wakili msomi Boniface Mwabukusi kuwasilisha majibu yake. Atafuata wakili Msomi Livino na atamalizia Wakili Msomi Philip Mwakilima.

Sasa anamkaribisha Wakili msomi Mwabukusi aendelee.

Anasimama sasa wakili msomi Boniface Mwabukusi ( Mayweather) kwa ajili ya kuwasilisha majibu.

Adv. Mwabukusi: Wakili: Mwabukusi: nitajikita katika issue namba 1, 4 na 5

Wahe. majaji naomba kuelezea kuhusu Capacity to contract. Jambo la msingi sana kwa pande mbili katika mkataba.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walitumia katiba ya Dubai kwamba inaruhusu hiki kilichofanyika, wasilisho hilo sio sahihi kwani ibara ya 120 (1] Cha katiba ya UAE

Kifungu hiki kipo wazi, unapo Montevideo convention, Viena convention. Vinahusu mambo ya kimataifa na sio domestic matter.

Adv. Mwabukusi: Tulitarajia wenzetu watuonyeshe sifa za Dubai kama nchi kimataifa. Mpaka wanafunga mawasilisho yao, hakuna chochote tulichoonyeshwa kinachokidhi matakwa ya viena convention.

Adv. Mwabukusi: Kuhusu hadhi ya ubalozi, hadhi ya nchi m, kama dubai inakiti umoja wa mataifa. Hatujaambiwa sio kwa bahati mbaya, ni kwa sababu havipo.

Waheshimiwa, wenzetu walisema IGA imeeleza kwamba ibara ya 28 ya IGA Imeeleza kuhusu Competence.

Adv. Mwabukusi: In that angle they missed the target.

Wenzetu walisema IGA ni International treaty hivyo inatakiwa kushugulikia kwa sheria za kimataifa sio za ndani. Waheshimiwa majaji.

Adv. Mwabukusi: Kwakuwa wenzetu wameshindwa kuonyesha utu wa kisheria wa DUBAI, hawawezi kutengeneza kitu ambacho kikapata sifa za International teaty.

Adv . Mwabukusi: IGA hii katika ibara 2(1) wenzetu hawajakataa wala kukanusha kwamba huu mkataba wa IGA is a binding agreement unaohusu kuendeleza, kuimarisha, kuendesha na kusimamia bandari za maziwa na bahari.

Adv. Mwabukusi: Ili kuimarisha maeneo ya kiuchumi na shoroba za kibiashara pamoja na miundombinu ambata kuhusiana na Bandari.

Adv. Mwabukusi: Kwa wenzetu kukubali; wamekubali kwamba mkataba huu unagusa Mali asili (Natural resources) za Tanzania ambazo zinagusa sovereign na kunasheria maalumu ziinazolinda permanent sovereign kwenye Natural resources.

Adv.Mwabukusi: Wenzetu hawajapingana na mawasilisho yangu ya sheria za Rasilimali Na.5 ya mwaka 2017 ambayo inatoa sovereignty kwa Watanzania katka rasilimali zao.

Adv. Mwabukusi: Ili kuhakikisha ulinzi wa Rasilimali za nchi. Preamble ya hii sheria ipo wazi ambayo inatoa effect ya article 8(1] 9[f), ya katiba ya Tanzania na wenzetu hawajapinga.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa Sheria hii Na.5 katika Preamble inaakisi ibara 27(1) ya Katiba ya Tanzania kuhusu permanent sovereignty ya Rasilimali zetu.

Waheshimiwa majaji, ukisoma sheria ya maliasili Na 5 na Na 6 za mwaka 2017. Kwenye sheria na 6. Kifungu cha 6(a,b,c)

Adv. Mwabukusi: Maudhui yake ni kuweka usimamizi wa Rasimali za Watanzania kwa watanzania na wenzangu hawajasema hizi sheria kama zimeshafutwa. Sheria hizi bado ni hai na are so fundamental.

Adv. Mwabukusi: Na are forming basis of protection of our natural resources. Ibara zote tulizozitaja kwenye IGA , inakiuka Katiba ya Tanzania.

Waheshimiwa majaji maudhui ya sheria hii yana ukatiba kwani sheria hizi zinafafanua Katiba ya Tanzania Ibara ya 27[1

Adv. Mwabukusi: Wenzetu wanasema Kwa sababu ni International treaty hivyo Viena Convention kutumika na wao walisahau kuwa sheria husika imeweka pia angalizo.

Katika ibara ya 46(1) cha Viena Convention [Quote).

Anasimama wakili wa serikali aitwaye Kalokola anaweka pingamizi.

SA Kalokola: Objection, waheshimiwa majaji msomi hakutumia Ibara ya 46(1) na hawakutumia ibara husika hivyo hatakiwi kutumia ibara yako.

Adv. Mwabukusi: Mwabukusi: wao walisoma kifungu cha Viena convention in absolute na wakasahau kwamba kuna angalizo kwenye VIENA CONVENTION.

Jaji: Tunakubaliana na wakili wa serikali kwamba hiki kitu ni kipya na wao hawana nafasi ya kujibu.

Adv. Mwabukusi: Taifa letu tume-domesticate charter of Economic rate and Duty of the state, under Article 2(1)(2)a, b kwenye sheria ya Rasilimali. Na.6 ya 2019.

Wakili Mwabukusi anasoma hivyo vifungu.

Adv. Mwabukusi: Yametumika maneno Sovereignty na maneno haya hayapo kwa bahati mbaya. Kesi ya SMZ Vs. Machano Hamisi, page 7 paragraph 1 inayoeleza nini maana ya Sovereignty.

Paragraph ya kwanza na paragraph ya mwisho: (isomwe) kwa msisitizo.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walisema IGA ni frame work na kutakuwa na mikataba mingine midogo kwamba HGA ndio zitaweka masharti haikuwa sahihi.

Kwa sababu ibara ya 12 (2) ya IGA imeeleza wazi na naomba waheshimiwa majaji wakati mnatafakari msome ni kinyume cha wenzetu walivyosema.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walisema masuala yanayolalamikiwa yatakuwa kwenye HGA lakini ukweli ni kwamba kifungu cha 12(2) kimeshaweka masharti.

Jaji: Naomba usome 12(1)d.

#Updates kesi ya bandari.

Anaendelea wakili Mwabukusi kuwasilisha majibu yake.

Adv. Mwabukusi: kifungi hiki kimetumia neno shall na hivyo HGA tayari masharti yake yapo kwenye mkataba wa IGA na nawaalika msome Ibara ya 20[3] ya Mkataba wa IGA.

Adv. Mwabukusi: Hii ibara wenzetu wanasema tutaikuta kwenye mkataba wa HGA wakati tayari imeshatajwa kwenye Mkataba wa IGA. Hivyo HGA tayari ipo kwenye Mkataba wa IGA.

Anasimama wakili wa serikali anaweka pingamizi kwamba Boniface Mwabukusi anaingiza jambo jipya.

SA Kalokola: Objection, tunapinga kinachoendelea, ni kubadili pleadings hawakulalamikia ibara ya 23[3) atuonyeshe wapi wamelalamikia hiyo ibara.

Jaji: SA Kalokola, nenda kwenye Originating Summons soma kwenye paragraph 2 kinasomekaje

SA Kalokola: hakuna ibara hiyo ya 20[3) ya Mkataba wa IGA.

Adv. Mwabukusi: Wao waliwasilisha kuhusu HGA kwamba HGA itafanyika baada ya MKATABA wa IGA na mimi ninajibu kwenye hoja waliyoiwasilisha.

SA Kalokola: waheshimiwa majaji akijielekeza kwenye ibara ya 20, 21 ya mkataba wa IGA Na sio Ibara ya 23(1].

Jaji: Kuanzisha hoja mpya katika Rejoinder ni kukuza mjadala naomba juelekeze kwenye hoja ambazo sio mpya. Sisi tutasoma nyaraka zote.

Adv. Mwabukusi: Wakati mawakili wa serikali wanawasilisha majibu yao walisema migogoro ya IGA itatatuliwa na mahakama za ndani, lakini ibara ya 20(2]a,e(i)[ii][iii][iv] ya IGA zinaeleza kwamba mabaraza ya kigeni ndio yatashughulikia migogoro baina ya pande mbili.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa majaji, hiki ni kinyume na Katiba ya Tanzania na sheria za nchi zinazohusu rasilimali za nchi.

Kesi na 23 ya TLS ya mwaka 2014 ulioamuliwa mwaka 2019 uamuzi huu haukuzingatia Sheria hizi za Rasilimali za asili Na.5 na 6 za 2017.

Anamaliza wakili Mwabukusi sasa anamkaribisha wakili Livino kuendelea kujibu.

#Updates kesi ya bandari.

Anasimama wakili Livino Ngalimitumba.

Jaji; maana ya jina Ngalimtumba ninini

Adv.Livino: kwa asili sisi ni wakisi na maana ya hili jina maana ake ni Kutatua migogoro.

Mahakama: kichekoooo

Adv. Livino: Wakili : Nitajibu hoja za wakili wa serikali Edwin aliyejibu hoja zangu waheshimiwa.

Kwanza alilalamikia kwamba kitabu cha Rules of Law VRulers of law sikuwapa kopi ili akasome.

Adv. Livino: Ningependa kujibu kwamba alikuwa na muda wa kujiandaa maana alikuja kujibu hoja siku ya pili na Senior wake Wakili Mark alikubaliana na kitabu husika na content zake.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, alieleza kuhusu kanuni zilizowekwa kwenye kesi mbalimbali haswa kunapokuwa na malalamiko kuhusu uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Ni muhimu kulinganisha vifungu vya katiba pamoja na vifungu vinavyolalamikiwa.

Adv. Livino: Alitaka kesi ya AG Vs dickson sana, kesi ya Christopher Mtikila Vs AG 1995.

Na kunukuu maneno yaliopo katika kesi ya mtikila ya 1995 ukurasa wa 34.

Naomba mahakama itambua kuwa katika hizo kesi kulikuwa na issue tofauti na issue tulizonazo leo.

Adv. Livino: Kesi ya Dickson ilieleza kuhusu uhalali wa kifingu cha 145[8] CPA Cap 20 kuhusu issue ya dhamana katika makosa ya jinai.

Kesi ya mtikila, mahaka ilikuwa inatatua hija nyingi, uk.36 par. [g) ilijikita Katika kurekebisha marekebisho ya 8 ya katiba ya Tanzania ya 1977.

Adv. Livino: Kesi zote hizi mbili mahakama ilialikwa kutazama uhalali wa Statutes Act of Parliament na sisi tuko hapa kutazama vifungu vya mkataba na sio statutes na sio bunge.

Adv. Livino: Ni rai yangu kesi alizozinukuu SA Edwin hazipaswi kuwa applied kwenye kesi hii absolute bila kutazama circumstances ya kesi tuliyonayo hapa

Kwa kuwa tunatazama uhalali wa Mkataba, ni kanuni ya wazi kuwa mkataba wowote unaokwenda kinyume na sheria ni mkataba Batili.

Adv. Livino: Kwakuwa tunatazama uhalali wa Mkataba, ni kanuni ya wazi kwamba mkataba wowote unaokwenda kinyume na sheria ni mkataba Batili.

Waheshimwa majaji, mwenzangu alicante kesi ya SMZ Vs. MAchano Hamisi na wenzake, katika ukurasa wa 17 haswa kwenye tafsiri ya Sovereignty.

Adv. Livino: Tunakubaliana kwamba tafsiri husika ni sahihi kwakuwa ndio standard ya sheria za kimataifa.

Ningependa kukumbusha mahakama na wakili wa serikali Edwin kwamba issue zilizokuepo katika hiyo kesi, inapatikana katika page na 4 na 12 ya hiyo hukumu. Mahakama inaeleza.

Adv. Livino: Kwamba watuhumiwa hawa walikuwa wameshitakiwa kwa makosa ya uhaini ya kumuondoa Raisi wa Zanzibar.

Na page namba 12 paragraph 3 inaeleza kama Zanzibar ni Sovereignty state (Is zanzibar a Sovereign state.

Adv. Livino: Katika hilo naungana na wakili wa serikali kalokola alieleza kuwa muundo wa Emirates of Arabs inafanana kabisa na muundo wa Tanzania.

Hivyo Dubai haina mamlaka ya kuingia mkataba wa kimataifa kwa kuwa sio sovereign.

Adv. Livino: Wakati wakili wa serikali anawasilisha majibu yao alisema hatuwezi kupoteza Sovereignty kwa kuwa Tanzania ilipata uhuru 1961. Namkumbusha kwamba huo mwaka wa 1961 Tanzania haikuwepo.

Adv. Livino: Tanzania iliundwa 1964 Kwa hiyo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika ilipoteza sovereignty zanzibar ilipoteza sovereignty na kuunda Tanzania yenye sovereignty kama nchi moja.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, Mwenzangu alielezea Ibara 6(2) ya IGA kwamba Tanzania inaweza kuinterfere DP WORLD. Sisi tunapenda kusisitiza kwamba ibara hiyo imeweka interference Conditionally.

Adv. Livino: Kwamba interference lazima ieleweke na pande zote mbili na zjnapaswa kukubaliwa na pande zote mbili.

Hivyo Tanzania ikikubali kwamba kuna mgogoro na wenzetu wasipokubali maana yake Tanzania haita fanya interference. Hii inapoka sovereignty kama nchi.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, ni ukweli kwamba uandishi wa kifungu hiki unanyang'anya Sovereignty kinyume na ibara ya 1,8 na 28 ya Katiba ya Tanzania.

Kama nchi inawekewa vikwazo vya kujilinda kwa namna yoyote IGA ni batili.

Adv. Livino: Kuhusu ibara ya 8(2] ya IGA issue ya Land Rights alisema tusome tafsiri na anakubali kwamba sheria za nchi haziruhusu mgeni kumiliki ardhi.

Adv. Livino: Namkumbusha kwamba tafsi aliyoitaja ya IGA kuhusu land Rights. Ni mtizamo wetu kwamba inaongelea Ownership of land na inampa mgeni haki ya Occupancy of land.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, tafsiri ya ibara husika, ni mtizamo wetu kwamba sheria zetu zinaeleza kuhusu occupancy. Ukisoma kifungu cha 8(1)[2] vifungu hivi vinakusudia kumpa title DP WORLD Ku-occupancy land in Tanzania.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, wenzetu walieleza ibara ya 66 ya Viena Convention ambayo inaeleza kuhusu kutatua migogoro kati ya nchi zilizokuwa katika nakubaliano.

Imeeleza kuwa kuna kwenda ICJ na pili ni ARBITRATION na migogoro chini ya IGA itakwenda kwenye mabaraza ya nje.

Adv. Livino: Ni mtizamo wetu kwamba uwepo tu wa vifungu vya IGA vjnavyoelekeza utatuzi wa migogoro katika mabaraza ya nje ni kitendo kinachokinzana na sheria za nchi kama Senior wakili mwabukusi slivyosema hapo awali.

Adv. Livino: Serikali wakati inaenda Dubai kufanya mazungumzo na DP World ilitakiwa kuwa na duty bind ya kuzingatia sheria za nchi yetu na kwa mantiki hiyo IGA inakuwa batili tangu mwanzo kwa kuwa sheria hazikufuatwa.

Adv. Livino: Ibara ya 21(3) ambayo inakataza Tanzania kujiondoa katika mkataba mpaka ridhaa ya DP WORLD ni mtizamo wetu kwamba kifungu hiki kinapoka sovereignty kama nchi

Ibara ya 23[4] isomwe pamoja na 23(4] kwamba mkataba huu hautaruhusiwa kuvunjwa inapoka sovereignty ya nchi.

Adv. Livino: Wenzetu walieleza juu ya Termination ibara ya 54 ya Viena convention. Ni maoni yetu kwamba ibara hii isomwe na ibara ya 60 ya Viena convention.

Waheshimiwa majaji, IBARA 23[4] wa IGA inasema mkataba huu haupaswi kuvunjwa hata kama kuna uvunjwaji wa terms za mkataba.

#Updates kesi ya bandari,

Anaedelea wakili Msomi Livino kujibu hoja zake.

Adv. Lovino: Tunaomba mahakama hii itambue kwamba hata VIENA CONVENTION Imevunjwa ambayo ilikuwa basis ya submission yao.

Adv. Livino: Wahe.majaji,wenzetu walieleza kuhusu nchi yetu kutii masharti ya kimataifa na serikali pamoja na Bunge ilitekeleza hilo.

Ni msimamo wetu kwamba ibara ya 14 ya Viena convention inatamka kwamba sovereignty ya mataifa iheshimiwa na Sheria za ndani ziheshimiwe.

Adv. Livino: Hivyo ni mtizamo wetu kwamba malengo ya kufanya ratification ya IGA kwa mujibu wa sheria za kimataifa na ndani hayakuzingatiwa.

Tunaomba mahakama hii itamke kuwa mkataba wa IGA imevunja pamoja na Viena Convention.

Wakili wa serikali Kalokola anaweka pingamizi kwamba; wenzetu hawakuomba order ya mahakama kwamba IGA imevunja Viena convention.

Jaji : Kwamba usingeomba order kungekuwa na tofauti?

Adv. livino; naondoa prayer husika waheshimiwa.

Adv. Livino: Wakili wa serikali Mr. Edwin alitaja ibara 4(2) ya IGA kwamba hakuna Binding obligation ya Tanzania kutoa taarifa kuhusu fursa za Tanzania. Ningependa kumwambia kwamba Mkata wote wa IGA is a binding document. Na hiyo inaonekama katika ibara 4(2) ya IGA.

Adv. Livino: Wakili wa serikali alisema ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania kwamba ibara hii inaongelea VITA. Alieleza kwa IGA haijaeleza masuala ya Vita.

Ningependa kusema kwamba Dunia imebadilika. Uvamizi wa sasa sio lazima wavamizi wakanyage ardhi ya Tanzania.

Adv. Livino: Uvamizi ni pamoja na uvamizi wa misingi ya uchumi pamoja na vyanzo vya mapato yake kama Rasilimali za nchi ikiwemo Bandari.

Kwa hiyo tunaposema usalama wa nchi na kutambua adui wa nchi. Hatupaswi kuangalia ardhi pekee na nimaelekezo ya kanuni za utafsiri wa Katiba.

Adv. Livino: Kwamba isitafsiriwe kwa namna ambayo inapoteza maslahi ya nchi. Kuna kesi ya Julius Ishengoma ipo naomba musome page 16 ambapo mahakama inaeleza namna ya kutasmfsiri vifungu vya katiba.

Adv. Livino: Ilisema mambo yafuatayo, Katiba itafsiriwe in a Liberal manner, jealously, our people enjoy their rights, will of the people must prevail.

Adv. Livino: Dhumuni letu kwamba katiba itafsiriwe kwa mawanda hayo na tunapoitafsiri ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania kuhusu usalama wa nchi tunamaanisha tusiishie maneno tu yaliyopo hapo kwenye katiba tunapaswa kuakisi mabadiliko ya nchi.

Adv. Livino: Tuko ibara 2(1) ya Katiba Tanzania inaeleza mawanda ya Tanzania (Quote) lakini neno anga halijatajwa hapa.

Na ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania haijataja anga. Swali ni je, Watanzania hawahusiki na anga na hivyo tusideal na anga.

SA Edwin: Objection, Ibara ya 2(1) haikutajwa hivyo tunaomba asiitumie

Livino: Naondoa kwa kuwa mahakama ilisema itasoma nyaraka zote.

Kwa kumalizia ni kwamba mahakama ijielekeze katika nyanja mbalimbali katika kutafsiri Masuala ya Katiba.

Adv. Livino: Kwa kumalizia wakili wa serikali alitaja taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo TBS , uhamiaji n.k lakini ukweli ni kwamba hayo ni maneno yake mwenyewe na wala hayapo kwenye IGA.

Anamaliza Wakili Livino sasa anamkaribisha Philip Mwakilima.

#Updates kesi ya bandari.

Anasimama wakili Philip Mwakilima kujibu hoja

Adv. Mwakilima: Waheshimiwa majaji: nitajikita katika issue na.6 kama IGA ilifuata sheria ya Manunuzi(Procurement Act) na naomba sehemu niliyofanya katika mawasilisho ya awali iwe sehemu ya Rejoinder hii.

Adv. Mwakilima: Wakili Kalokola akirespond kiapo cha walalamikaji kuhusu neno DPW na neno linatakiwa kusomwa ni DP Word.

Adv. Mwakilima: Kutokana na principle za overriding objectives ibara 107A (2)e ya Katiba ya JMT,1977 as amended inaitaka mahakama ijikite katika kutenda haki kwenda kwenye substance na sio legal technicalities.

Adv. Mwakilima: Hivyo typing Error inapaswa kutoathiri haki za wateja wetu.

Katika kiapo kinzani wamekiri kwamba hakukuwa na Mchakato wa kutoa Tenda na pia hawapingi kwamba sheria inayotuongoza mcahakato wa Tenda ni Procurement Act.

Adv. Mwakilima: Ni kwamba wanakili kuwa sheria hiyo imevunjwa.

Waheshimwa majaji wenzetu walitaja kifungu cha 4(1) ya Procurement Act, wakili akiwa amekuja na tafsiri kwamba IGA ni International treaty.

Adv. Mwakilima: Waheshimiwa majaji kifungu husika, there is no any conflict between PROCUREMENT ACT and International treaty. Pia IGA haina sifa ya kuwa International treaty.

Adv. Mwakilima: Kama kalokola alivyosema Zanzibar na Tanzania ni sawa Dubai na Emirates of Dubai. Kwa misingi hiyo hakuna International treat

Kama mahakama itakubaliana na sisi kwamba kifungu cha 64 cha Sheria ya Manunuzi (Procurement Act) Mkataba wa IGA Umekinzana na sheria hii.

Adv. Mpoki: Waheshimiwa imetuchukua siku nne, na research imefanyika. Kuna msemo unasema if you can't convince them confuse them.

Mahakama: kicheko kidogo

Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji, tunasubiria uamuzi wenu. Thus all.

Anamaliza wakili Mpoki sasa mahakama inakaa kimya kwa muda.

Majaji Ndunguru: naomba kabla sijatamka tarehe ya maamuzi; kwa niaba ya majaji wenzangu nawashukuru sana Mawakili pande mbili.

Jaji: Kwa kile mlichokionyesha, sisi tumeona the highest level of professionalism namshukuru sana.

Jaji: Naomba pia kipekee nimshukuru wakili Boniphace Mwabhukusi kwa kucheza vizuri sana akiwa ndani ya mahakama na akiwa ulingo wa siasa huko nje. Mwabukusi ameitendea haki taaluma yake.

Baada ya kusema hayo niseme kwamba mahakama hii itatoa hukumu yake siku ya tarehe 7 August 2023 siku ya jumatatu.

Majaji wanatoka.

Askari anapiga salute

High cort kwa sauti juu sana.

Mdude Nyagali 7 x 70 kutoka hapa mahakamani.
 
Mungu awalinde hawa wahehe na wanyakyusa toka mbeya na Iringa. Asiwasahau wakristo na waislamu wenye nia njema ya kuokomboa nchi hii. Heshima na hadhi yao itazidi ya Nyerere aliyetuunganisha na majahili, nakuja wasiojielewa na wenye kujikomba kwa waarabu milele. Mijitu inamnyenyekea mwarabu mpaka akili wanaziweka makalioni mbwa Koko kabisa hao
 
Jumatatu siku ya hukumu, kwa maoni yangu kila kitu kipo wazi, utetezi mkubwa kabisa upande wa mawakili wa serikali ni kule kusema HGA itakuja na majibu, wasijue vipo baadhi ya vifungu kwenye IGA ambavyo tayari ni binding hata wakienda kwenye HGA havitabadilika.

Apart from that, zipo sheria nyingi za ndani ambazo zimevunjwa na ule mkataba wa IGA, zipo wazi havifichiki, sitegemei kuona mahakama ikija na maamuzi tofauti yatakayoiweka ardhi yetu rehani, na thamani ya utu wetu itupwe jalalani, naamini mahakama itasimamia haki za mtanganyika kipitia sheria zetu, hasa Katiba 1977.
 
upuuzi mtupu,
DPW wameshaingia na maandalizi yanaendelea....nyie potezeni muda huko kwenye kubishana or mkataba na makubaliano nini.

waelemishwe tofauti kati ya mkataba na makubaliano.
kazi iendeleee
 
Jaji baada ya kusema hayo niseme kwamba mahakama hii itatoa hukumu yake siku ya tarehe 7 August 2023 siku ya jumatatu.

Shukrani kwa kazi ya kutukuka kuripoti kesi hii ya kihistoria ya wananchi .

Umefanya jukumu kubwa kupita vyombo vya habari kongwe Tanzania ambavyo vimeonesha upetevu ( indolence) katika majukumu ya kuripoti habari hii kubwa
 
Back
Top Bottom