Updates ya kesi ya bandari majibu ya mawakili wa serikali. 26th July 2023

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
#Updates kesi ya bandari

Sasa ni saa 14: 45 mchana majaji wanaingia karani anataja namba ya kesi ambao ni kesi no.05/ 2023.

Mahakama inakaa kwa utulivu kidogo huku majaji wakiandika.

#Kesi_Ya_Bandari.

Anasimama wakili wa serikali kuomba kuanza kujibu hoja za waleta maombi.

SA = wakili wa serikali

SA Mark : Waheshimiwa majaji

W: Serikalin: Mark; waheshimiwa majajiji naomba mahakama iangalie vitu gani vinapaswa kuangaliwa katika kesi ya kikatiba.

Issue ya 1, 2 Edson atawalisha, issue 4,5 na 6 itawasilishwa na kalalokola, Edwin issue 3,

Waheshimiwa maombi yameletwa chini ya ibara ya 108(2) ya Katiba ya Tanzania na Kifungu cha 2(3) cha JALA Kutumia Originating Summons na kiapo

SA Mark: Kwa sasa tunaomba kibali cha mahakama tukufu ili majibu yetu na kiapo kinzani zitengeneze sehemu ya majibu yetu kinzani. Shauri hili linapinga uhalali wa kikatiba wa kutia sahihi na kuridhia mkataba wa kimataifa (IGA) baina ya nchi mbili. Tunawashukuru wenzetu kwa submission yao kwa sa babu kuna maeneo tunakubaliana nao mfano umuhimu wa kufuata na kuheshimu katiba. Waheshimiwa tumependezwa na wenzetu kutumia kitabu chenye maandiko ya Samata J" kitabu cha Rule of Law Vs. Rulers of Law: kuishi kwa kufuata utawala wa katiba ni wokovu na sio utumwa. Tunaamini wananchi wote wanakubaliana kwamba lazima tuishi kwa mujibu wa Katiba ya nchi.


SA Mark: Waheshimiwa majaji Katiba hii niliyoishika imeipa mahakama jukumu kubwa chini ya ibara ya 107A kama chombo cha juu cha utoaji haki. Anasoma kifungu husika (107A). Nachojarubu kusema hapa: Katika kutoa haki mahakama inapaswa kufuata sheria.

Kazi kubwa ya mahakama ni kufanya uamuzi kudetermine kama kitendo kilichofanywa na serikali kinavunja Katiba yetu ya Tanzania. Kazi kubwa ya mahakama ni kufanya uamuzi kudetermine kama kitendo kilichofanywa na serikali kinavunja Katiba yetu ya Tanzania.

SA Mark: Na ili mahakama ifanye hivyo inapitia pleadings zote zilizoletwa na kuangalia kama imepita Threshold ya kuthibitisha kesi ya kikatiba. Na hiki hakiwezi kufanyika ikiwa waleta maombi hawataleta kifungu cha katiba kilichokiukwa na kuonyesha kiasi gani kifungu husika kimekiukwa. Waheshimiwa ni mahakama yenyewe imetamka hili katika maamuzi mbalimbali hivyo ni vizuri tulaweka msingi huo na ueleweke. Katika shauri la AG Vs Jeremiah Ntobesya. Rufaa ya madai, 65/2016 ukurasa wa 46 mpaka 47 mahakama wakati ikikubaliana katika shauri la KIKATIBA ilitamka.

SA Mark: Mahakama ilisema kama kuna vifungu vimekiukwa, Mahakama kuu inachukua vifungu vya sheria vinavyosemwa, unaviweka pamoja na Vifungu vya katiba ili kuona ubishani. Na mahakama haipitishi wala kulaani shauri lolote linalopitishwa na Bunge kazi yake ni kuangalia kama vifungu vinakiuka katiba.

SA Mark: Waheshimiwa majaji, Shauri hili halichallange kupitishwa kwa sheria iliyopitishwa na Bunge wanachallange makubaliano. Ni vema mahakama hii ikaendelea kutambua, wenzetu wameleta shauri hili chini ya ibara ya 108[2] wakisema mahakama inamamlaka ya mahakama ya kusikiliza yale yote yaliyoletwa. Hatuna ubishi kwenye ibara husika, pia kuna ibara 30(3] ya Katiba pia inaipa mahakama kusikiliza.

Wakili Mpoki anaweka pingamizi anasema: Waheshimiwa tushaamua kuhusu Mapingamizi na wameondoa jana na naona anafanya submission ya "PO" kana haina mamlaka tufunge mabegi yetu tuondoke.

SA Mark: Sio nia yangu kuongelea PO, nachotaka kusema: mahakama iangalie mazingira yote na kujiridhisha kwamba ibara ya 108 ni sahihi na kujiridhisha vifungu bishaniwi Waheshimiwa majaji, nilikiwa nasema ni wajibu wa mahakama kufanya maamuzi kwa Mashauri yanayoletwa chini ya ibara ya 108(2) ya Katiba ya Tanzania, 1977.

Adv. Mpoki: Basi naomba afute maneno yanayosema mahakama ina limited jurisdiction

SA Mark: Tunaomba muongozo katika hili, haya sio maneno yangu, ni naneno ya maamuzi ya mahakama ya rufaa. Yangekuwa yangu ningeyafuta Naomba muongozo

Jaji : PO zilishaamuliwa kwa hiyo tunaregard kama submission endelea

SA Mark: Ninani anayetakiwa kuthibitisha; anayetakiwa kuthibitisha katika shauri la kikatiba ni mleta malalamiko.

SA Mark: Katika shauri CHRISTOPHER Mtikila V. Ag. 1995 TLR 31Page 34 inasema: ukiukwaji wa katiba ni jambo kubwa lazima uwe na ushahidi wa hakika

[7/26, 15:30] Wakili Livino Ngalimitumba: Pia katika kesi ya Center for Strategic litigation & Another Vs. AG and Anather page 40-41, Mahakama kuu ilikuwa na haya ya kusema; Pamoja na ku-cite kifungu cha katiba, ni lazima kusoma kifungu cha katiba kilichokika na namna kilivyoathiriwa na kinatakiwa kuwekwa kwa namna haina shaka.

SA Mark: Shauri ishengima, Francis ndyanabo Vs. AG ,2004 page 14 inasema: (Quite): kimsingi wanaongelea kwamba Kila kifungi cha katiba kinauhalali na yule anayesema kifungu kinamnyima haki lazima afanye hivyo. Tunaiomba hii mahakama isiamue kama IGA inavunja sheria zetu za ndani. Naomba nimkaribishe msomi Kalokola kwa mawasilisho.

Sasa ni zamu ya wakili wa serikali Kalokola.

SA = kifupisho cha wakili wa serikali.

SA Kalokola: Waheshimiwa nitajielekeza kwenye hoja namba 4 iliyotengenezwa na mahakama on where IGA is a contract. Nitajikita na kuongozwa na vitu vifuatavyo: MONTEVIDEO CONVENTION ON THE RIGHTS AND DUTIES OF STATE, Pia VIENA CONVENTION ambayo iliridhiwa na Tanzania, pia nitaongozwa na Mkataba wenyewe. Nitarejea Katiba ya Tanzania, 1977 toleo 2005 na mwisho nitaelezea Katiba ya umoja wa Falme za kiarabu katika kujibu hoja husika. Na mwisho kabisa hati ya madai ya walalamikaji. Waheshimiwa Majaji, kwenye ground ya kwanza walalamikaji wamuita as International agreement. Na ukienda kwenye maombi yao wanautambua kama International Agreement. Na walalamikaji wakatupa ushahidi wao.


SA Mark: Katika aya ya 5 wanasema, mjibu maombi wa pili ni Waziri amesaini mkataba wa Kimataifa. Kwa hiyo mpaka sasa walalamikaji wanautambua kama mkataba huu ni mkataba wa kimataifa. Hoja inayofuata; Je Mkataba wa kimataifa unaongozwa na sheria zipi; kujua mkataba wa kimataifa unaongizwa na sheria zipi nitataja sheria za kimataifa. Nitaanza na VIENA CONVENTION 1966 ambapo Tanzania ni mwanachama baada ya kuridhia. Ibara ya 2(a) Viena Convention on laws and treaties inajibu tafsiri ya Mkataba wa kimataifa. Unaposema mkataba ni wa kimataifa Tambua kwamba mkataba huo utasimamiwa na sheria za kimataifa. Mkataba huu uliingiwa na Nchi mbili Emirate of Dubai na Tanzania kama mkataba wa Kimataifa. Wakili Mwabukusi alijikita katika kuridhiwa kwa Mkataba na katiba ya kiswahili inatumia neno Mkataba ibara 63(3)e ya Katiba inatumia neno:

SA Kalokola: Wakili Mwabukusi alijikita katika kuridhiwa kwa Mkataba na katiba ya kiswahili inatumia neno Mkataba ibara 63(3)e ya Katiba inatumia neno: Bunge linaweza kuridhia mikataba. Sheria ya kimataifa huu mchakato wa ibara ya 63(3)e ni mchakato unaoitwa ratification of International agreement. Ibara ya 2b ya Viena Conv,1966 inazungumzia ratification hivyo mkataba huo IGA inatakiwa kupitia mchakato wa kuridhiwa kama ibara ya 63(3)e ya Katiba ya Tanzania. Ilikujua hadhi ya mkataba huu, ibara ya 25(2) ya IGA inasema hivi

(Quote): Serikali za nchi mbili ndani ya siku 30 baada ya kusainiwa unahalalisha bindingness under international law. Kila mhusika kwa taratibu zake na sheria za ndani ufanye ratification ili uwe na hadhi ya sheria za kimataifa Na ndio sababu ya IGA kupelekwa Bungeni. Na ndio maana mbele yenu kunamalalamiko ya namna IGA ilivyoridhiwa. Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.

SA Kalokola: Na sheria za ndani hazina nguvu dhidi ya mikataba ya kimataifa
[7/26, 16:03] Wakili Livino Ngalimitumba: Waheshimiwa hoja ya pili kuhusu Capacity to contract. Mwabukusi alitumia ibara 103 ya katiba ya umoja wa falme za kiarabu na ibara ya kwanza alitumia Montevideo convention. Vile vile alitumia ibara ya 123 ya katiba ya Dubai kusema Emirate inauwezo au la kuingia kwa mkataba. Nianze na Ibara ya 123 ya Katiba ya Emirate inasema (Quote) inaorodhesha mambo ya muungano kuhusu members of Emirate wanaweza kufanya makubaliano na nchi zingine. Ibara hii inazungumzia suala la foreign relation kwenye mambo yao ya muungano ni jambo la muungano

SA Kalokola: Hoja ya kujiuliza ni kwamba je mkataba huu umeingia in capacity of Foreign investment au international investment: Mkataba huu IGA unahusisha masuala ya uwekezaji ndio maana wanasema muwekezaji anapewa vyote.

SA Kalokola: Ibara ya 116 ya United Arabs Emirates inasema the Emirates shall exercise all powers not assigned to this Constitution nineno lililotumika kwa mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano: Ni sawa na katiba yetu kuhusu zanzibar na Tanganyika kuna mambo ambayo sio ya muungano ambayo nchi zinatekeleza.

Jaji: Neno shall kule Dubai lina context sawa na huku

SA Kalokola kwa context ya Tanzania shall ni lazima kwa upande wao sijajua

Jaji: ndio utuambie sasa

SA Kalokola: Mh Jaji nachotaka kusema parties are competent to contract Kwa mujibu wa sheria zao Waheshimiwa kwenye hoja hiyo, ninawajibu wa kusema kuhusu Katiba yetu, wajibu wa mahakama hii ni kutafsiri sheria zetu na DUBAI Pia mahakama yao ndio chombo cha kutafsiri katiba yao

SA Kalokola: Nilikuwa natarajia kwamba wenzetu kama wanataarifa kuwa mahakama ya Dubai imetamka kwamba kitendo cha DP WORLD kuingia makubaliano na sisi kimevunja sheria zao.

Na mwisho waheshimiwa; Katika shauri la TLS vs. Ministry of Foreign Affairs of International & AG, Cause 23/2014 mahakama hii ilipata nafasi ya kujadili hili.

[7/26, 16:25] Wakili Livino Ngalimitumba: Katika ukurasa wa 29 aya ya [1] ya Viana Convention. Kwamba kama mkataba umesainiwa..... (Quote). Mahakama inatuambia kukiwa na mgogoro kati ya wadau wa mkataba au mtu wa tatu, utatuzi unapaswa kufanyiwa katika mabaraza ya kimataifa.

Ibara ya 66 (a) ya viena convention inatoa namna ya usuluhishi wa migogoro ya mikataba ya kimataifa katika mabaraza ya kimataifa kwa usuluhishi.

SA Kalokola: waheshimiwa nasema mkataba wa kimataifa una International Forum za utatuzi wa migogoro na sio sheria zetu za ndani kama sheria ya mkataba sura 345. Subsequent project will be governed by our domestic law waheshimiwa kama ibara ya 21 ya IGA.

Jaji anatoa amri kwamba kwa maslahi la afya zetu, na watu kusimama muda mrefu kesi hii itaendelea kesho asubuhi saa 09:00.

Kesho Asubuhi mawakili wa serikali wataendelea na majibu yao.

Pia soma: Mbeya: Yaliyojiri katika Kesi ya kupinga mkataba wa Bandari na DP WORLD - Julai 26, 2023
 
Pana
26 July 2023

KESI YA BANDARI MAHAKAMA KUU MBEYA tarehe 26 July 2023

WAKILI MWABUKUSI - TUMEFANYA MAWASILISHO YETU YAANI SUBMISSION LEO ILI KUWASHAWISHI MAJAJI

Panapofuka Moshi zima moto chini iiiiiii alisikika msanii mmoja iv
 
Wakili wa serikali wakiwa na waandishi wa habari wakihojiwa nje ya mahakama kuu kuhusu mwenendo wa kesi

Mawakili wa serikali wadokeza njia ya suluhisho la kisiasa yaani muafaka - political solution kwa sakata la bandari, waomba wananchi warudi mezani kuongea na mheshimiwa rais kwani Mheshimiwa Rais ameonesha nia kusikiliza maoni

1690388924504.png
 
SA Kalokola: .....Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.
 
UTARATIBU WA KUCHANGIA KESI YA KIZALENDO DHIDI YA SERIKALI JUU YA UUZWAJI WA BANDARI ZA TANGANYIKA:


NMB: 24710018584
JINA: ALPHONCE LUSAKO MWAMWILE


TIGO PESA: +255718760649
JINA: LUSAKO MWAMWILE


UMOJA NI NGUVU


UPENDO NI KUFAANA.
Tutawachangia vijana wazalendo kama nyie
 
SA Kalokola: .....Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.
 
Sasa Kwa majibu haya ya mawakili wa serikali ambao ndo serikali wanategemea huko nje si ni majanga matupu. Tulia huko huko mbeya alisema bunge limepitisha makubaliano tu Leo mwanasheria wao anawageuka Tena.

Ni ngumu Sana kutetea uongo ukawa ukweli
Japo ilitakiwa kesi iendeshwe kwa Kingereza IGA ipo kwa Kingereza.
 
Back
Top Bottom